Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

Hekaya za Abunwasi............................................
 
Chief acha umalaya, kwa nini uwape lift kina dada tu, acha ufataki utakufa.
 
Ni wiki chache zimepita tangu nihamie kwenye kibanda chungu nilichojenga nje ya mji. Kwa sababu ya umbali wa ninakokaa na foleni za magari, inanilazimu kuondoka nyumbani kumi na mbili kasoro kuwahi traffic jam. Siku ya kwanza nikiwa kwenye gari yangu nilikutana na huyu binti aliyesababisha leo niombe ushauri. Alikuwa anajitembelea pembeni ya barabara akielekea kazini. Kwa kuwa sikumfahamu, nilimpita.
Kesho yake muda kama huo nilikutana naye tena, aliniangalia sana, lakini nikampita. Siku ya tatu nikamkuta tena kwa huruma nikasimama, na kumkaribisha lifti mpaka mjini ambako kila mtu alielekea kzn kwake. Basi tangu siku hiyo ikawa ndo kupeana lifti na mazungumzo ya ndani yalikuwa ni salamu tu.
Juzi amehamia jirani mwingine mdada ambaye amejenga nyumba karibu na kwangu kabisa. Baada ya kutambulishana na jirani huyu, akaomba nayeye awe anapata lifti ya kwenda kazn. Nilimkubalia.
Cha kushangaza, leo nilimpa lifti jirani yangu huyu mpya ambaye alikaa siti ya mbele ya gari. Hatua chache mbele kidogo nikakutata na huyu mdada wa siku zote, kama kawaida nikasimama.
Akaja, akafungua mlango wa mbele, baada ya kugundua kuwa kuna dada mwingine amekaa siti ya mbele, akafyonza na kufunga mlango kisha akazira na kukataa kupanda gari.
Nauliza waungwana kosa langi ni lipi? Na nimtendeje huyu dada? Nahisi maenidhalilisha kwa jirani yangu!

Wasalaam,
HP
Nakujibu kutokana na uzoefu binafsi. Huyo ni changudoa. Na ukimuendekeza kuna siku atakuumbua utajuta sana. Machangudoa kitabia hawana heshima hata chembe, na silaha yao kubwa hasa kwa mtu anayeonekana ana 'heshima zake' ni blackmail.
 
kwann siti yake ya mbele umpandishe mwingine loh! na mwenzio alishaizoea na pengine alishasema mungu amemletea mume jamani.............umeua ndoto za mwenzio jamani cpati nega usiku wake mana nina uhakika hajalala kabisaaaaaaaaaa mawazo chungu mzima ............angalia asije mpiga jirani yako kipapai kwa kuzani anamzibia riziki
 
Chief acha umalaya, kwa nini uwape lift kina dada tu, acha ufataki utakufa.

Kutoa lifti ni umalaya??? Hii sijapata kusikia! Lifti ni kitu cha kawaida na watu wa jinsia zote huwa wanaomba lifti, ila kwa huyu dada kesi yake imekuwa ni tofauti kabisa ndiyo maana nikaileta kwenu.
 
Hilo halikuhusu wala lisikupe presha,utapata presha kama utakuwa na lengo na mmoja wao!
 
sometimez huruma zetu zina2ponza, we mpotezee 2 and next tym hta ukikutana na wa aina gan we huruma weka kando. kma vp apande daladala. pole mkuu ndo binadamu walivyo!
 
Khaaa ! Mimi hapo kidogo nahofu kwann uwe unawapa lift wadada 2 ? Mtaan wenu hakuna masela.
 
hii ni kali!
Nimesoma hadithi nyingi, huwa zinaelekeana lakini ya kwako hii ni ya aina yake!
Wanawake wana wivu sana na ni roho mbaya kichizi!

Lakini wewe mwenyewe huenda hujatulia, unaweza kukuta unajieleza mambo mazuri tu, usikute ushalikoroga sana na huyo mdada wa watu siku za nyuma!...kwanini asonye wakati hajui kuwa huyo ni dada yako au shangazi yako?
Anaijua tabia yako huyo mkuu!..badilika!

tatizo ni wanawake unaokutana nao.do not generalize kuwa wanawake wanawivu wakijinga kama huo upuuzi wa huyo dada.wivu wa mume ni wakawaida hata mungu alimwambia mwanamke utakuwa na wivu kwa mumewe ila sio kiboyfriend.sema baadhi ya wanawake.me binafsi sina wivu.....mwombe mungu upate mwanamke ambaye hana wivu utaenjoy
 
inaonekana gari yako ina tinted kama usiku.!achana nae,u have nothing to lose
 
Du mzee kama kweli nia yako ilikuwa ni kumsaidia tu nahaujamuelekeza upande mwingine huyo achana naye kabisa maana hamjuani sasa tatizo liko wapi, ila basi kama ulisha changanya habari ukaingia sector zingine tubu kwanza kwa Mungu na kwake pia alafu ubadilikee mtu wangu hali hiyo sio! Na kingine umeoa? kama umeoa Chunga sana maana huyo anaweza kuhatarisha nyumba yako.
 
Achana nae kaka....japo hajafanya ustaarabu. Hakupaswa kusonya.
 
Pole sana braza. Shukrani ya punda mateke. Usipokuwa na gari tabu, ukiwa na gari tabu! Angggrrrh! Ipotezee, huyo demu hafai hata kwa kurumangia mtu wangu.
 
Back
Top Bottom