Afadhali wewe umeliona hili, watu humu wamenishambulia sana na kunifanya kama situmii akili. Nilishasema, nitamsamehe lakini lazima a-face concequences, nikimuacha hatakoma huyu, ataendelea kuniletea dhereu. Mimi ni mstahimilivu, na ananijua, lakini pale ninapooneshwa dhereu tena za wazi, huwa nakasirika kupita kiasi na maamuzi yangu yanakuwa ni mazito. analijua hilo!
Hata mimi huwa akinionya jambo kwa kunieleza kwa makini madhara ya kufanya jambo hilo naacha mara moja. nakumbuka kuna siku ilikuwa nisafiri kwenda Congo DRC kikazi akanishauri nisiende kutokana na hali ya usalama ya kule. nilifuata ushauri wake na nikatafuta sababu na ile safari akapewa mwenzangu na mimi nikabaki Dar. yule mwenzangu aliyesafiri alifika salama, lakini wakielekea kwenye eneo la kazi, gari liliowabeba lilipinduka na wenzake wawili walipoteza maisha, yeye na dereva wa gari lile walipona lakini waliachwa na majeraha mengi mwilini. Taarifa zile zilituifikia, na zilitushtua sana. Nilimetumia muda mwingi kumtahadharisha juu ya uamuzi wake wa kusafiri ilhali alitakiwa kuwa bed rest, lakini akakaidi. Je hizi si dhereu?