Nimfanye nini huyu Mwanamke?

Nimfanye nini huyu Mwanamke?

Lakini lazima nimuonyeshe kwamba amenikosea, na hivyo lazima apate adhabu japo kidogo!

Utampa adhabu gani? Si ndo utanuua kabisa naye? Na pengine utamuathiri kisaikolojia. Hapo alipo hajakuona na hajui ukirudi utamfanyaje. Hyo ni adhabu tosha. Time heals, msamehe tu na ndipo Mungu atakapofungua mibaraka.
 
ukirudi msigombane mpe pole kwa yote yaliyotokea.....atakuwa amejifunza kutokana na makosa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lazima muelewe kwamba sia nia yangu kumtesa, lakini ni lazima a-face consequences

Aface cösequencd mara ngapi? Hyo ya kupoteza mtoto nikubwa sana kuliko consequence nyingine yoyote. Na ni adhabu kubwa kuliko adhabu yoyote aliyowah kuipata ktk maisha yake. Mweke ktk hali ya kuweza kujipanga kupata mwengine. Unayotaka kumfanyia hayatasaidia.
 
huna budi zaidi ya kumsamehe
ukimpanikisha akijumlisha na msiba wa kakake aweza fanya kitu ambacho utakuja jutia baadae
just relax ww sio Mungu huenda mtoto angezaliwa but asingeishi hatujui
jipange upya mwache apone tafuteni mtoto mwingine.
 
Huyu ana hasira tu hapa jamvin,ila akifika kwa mamsapu akipewa unyumba atatulia tuliii kama sio yeye,we subiri tu atapewa vitu na maneno matamu kama halua na tende.
 
...Msamehe tu kwa sababu naye hakupenda ujauzito huo uharibike. Muombeni Mungu atawajaalia ujauzito mwingine na hatimaye kujifungua salama salmini. Kila la heri.
 
yaani iyo adhabu ya kupoteza mtoto unaona haimtoshi mpaka umuongezee nyingine? Kuwa na huruma we mwanaume. Msaidie mkeo kurudi kwenye hali nzuri ili aweze kupata ujauzito tena.
 
Hizi double standards huwa zinanifurahisha sana, yaani mwanamke anakuwa dhaifu only for her own convenience. Kila siku mnapiga mikelele me=ke ila zinapokuja ishu kama hizi, mnaleta ishu za mwanamke dhaifu sijui nini, Mi nadhani inabidi ifikie mahali tuset standards tu either ke ni kiumbe dhaifu au ke=me kuliko hii michanganyiko iliyopo sasa hivi.

Mimi nakuhakikishia siwezi kujidhalilisha na kujiita kiumbe dhaifu, kwani Mwenyezi Mungu alipowagawia akili binaadamu hakuweka upendeleo kuwa me ampe nyingi kuliko ke.

Au udhaifu kwa kutumia maguvu? Labda hiyo, lakini ametupa uwezo kwa kipengele chengine cha kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na kumleta duniani kwa salama.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wewe Revolutionist kwa kweli una roho mbaya na ya kikatili. Unataka uabudiwe na mkeo?

Eti aliyekufa kesha kufa kwani hatutambui hilo? Lakini kama mzazi wako amekulea kwa upendo huwezi kuchukulia kirahisi namna hiyo, au alikutupa wewe ndiyo mana huna imani?

Ingekuwa aliyekufa ndiyo basi tungekwenda kuwatumbukiza tu mashimoni lakini wapi umeona dunia nzima wakifanya hivyo?

Wewr uliyeomba ushauri angalia hou mwengine unaoushabikia wa akina Revolutionist una athari kijamii, jee wewe utapenda kuwafanyia hivyo wazazi wako?
 
Ua a man lyk eny othr of us..best thn is 2be wt ua lovly wife n suport hr plz...n achana wt thoz negatve thouts,
 
Lazima muelewe kwamba sia nia yangu kumtesa, lakini ni lazima a-face consequences

hee! We mzee vp? Consequence kubwa kuliko hizo unazotaka wewe ni kitendo cha kupoteza mtoto/mimba. Hawa wenzetu huwa wanaumia sana coz wanakimbizana na muda. Labda uniambie huwa unabahatisha kutoa sperm ko unasikilizia maumivu ya kutafuta zingine! Mfano hata Ukiwa hospital mtoto akifariki, mwanamke muda wote analia tu,ila janaume ukiliambia utaskia: mipango ya Mungu tutazaa mwingine. Kuwa mvumilivu na hawa ndugu zetu na jipange kumfariji na siyo hayo mambo yako unayofikiria.
 
Asiyesikia la mkuu,msamehe tu,naamini hakutegemea kama ujauzito ungetoka.Akili yote iliishia kwenda kumzika kaka yake.BIBLIA INASEMA "ENYI WAUME ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI MAANA NI VIUMBE DHAIFU"

Fe Lady ! Hata wanawake wengi wanavitumia hivyo vifungu vya verses kama kichaka cha kujifichia kwa mabaya wayafanyayo kimaksudi mazima!
 
inawezekana hujui umuhimu/uchungu wa huyo kaka,ila mkeo ndo alofiwa anajua.

Ingawa mkeo alifanya maamuzi kutokana na maumivu ya kufiwa alokuwa nayo hupaswi kuwaza umfanyeje mkeo, in short umfariji, afterall watoto hutoka kwa Mungu ndo
muamuzi atawapa mwingine.

Jua kila mtu anahandle tatizo kwa namna yake. Jinsi ulivyolikabili wewe ni tofauti na jinsi mkeo anavyolikabili.


Nimefiwa na mama, when I was young, na nilifiwa na baba ambaye nilimuuguza mwenyewe na akarudi nyumbani akiwa amepona lakini akazidiwa ghafla na kufariki, but I didin't panic, nilijipanga na kwenda nyumbani kuzika. so what is abig dill kufiwa na kaka! All of us we will die one day, none of us wil live forever!
 
Lakini lazima nimuonyeshe kwamba amenikosea, na hivyo lazima apate adhabu japo kidogo!

hivi kwenye hizo ndoa zenu mnaishi kama mke na mume au kama Bwana na kijakazi?
Kwa sababu tu ulifiwa hukupanic unatarajia mkeo awe hivyo hivyo? Mmeoa malaika? Au mkeo ana moyo wa chuma? Kipindi hiki wewe ulipaswa uwe karibu na mkeo umfariji, unaposema utamrudisha kwao ili iweje? Au utamwadhibu ili ufaidike nini?
Wewe ndo rafiki na mfariji wa mkeo, sawa kakosea hamwezi kuzungumza? Kwani kwa tukio hilo mkeo hajajifunza hapo? Mrudishe kwao wenzio wamfariji(kumbuka anaugulia misiba miwili sasa) kama hujarudi jamvini kulalamika. Acha ubinafsi wa kuwaza mtoto/mimba hebu angalia afya ya mkeo kwanza!

Watoto hutoka kwa Mungu kaka.
 
Mbona mimi nilifiwa na aliyenizaa kabisa na wala siku-panic!

Wewe si mkeo, uwezo wako wa kuhimili matatizo kama msiba hauko sawa na wake,so usilazimishe maamuzi yenu yafanane. Hakuna haja ya hasira wala ubishi mwingi,mimba imeshatoka,angalia mbele na msaidie mkeo,halijamfurahisha hilo na kama ni kuumia yeye kaumia zaidi aliyeibeba....huh!
 
Wewe si mkeo, uwezo wako wa kuhimili matatizo kama msiba hauko sawa na wake,so usilazimishe maamuzi yenu yafanane. Hakuna haja ya hasira wala ubishi mwingi,mimba imeshatoka,angalia mbele na msaidie mkeo,halijamfurahisha hilo na kama ni kuumia yeye kaumia zaidi aliyeibeba....huh!

Ohhh dearest. . nimefurahi kweli kukuona.You've been missed!!
 
Ohhh dearest. . nimefurahi kweli kukuona.You've been missed!!

he he he he,missed you more dearest,nimeona tumalize mwaka pamoja, am so happy to be here today,ila sijawahi kuacha kusoma thread zako,kila nilipopata muda....Unaendeleaje dearest??
 
he he he he,missed you more dearest,nimeona tumalize mwaka pamoja, am so happy to be here today,ila sijawahi kuacha kusoma thread zako,kila nilipopata muda....Unaendeleaje dearest??
Hehehehe asante dearest.Sasa mwaka ukiisha unatuacha solemba tena au utakuwepo?

Mi mzima kabisa, hofu kwako ambae hata ukitajwa hutokei.Lolz
 
Hehehehe asante dearest.Sasa mwaka ukiisha unatuacha solemba tena au utakuwepo?

Mi mzima kabisa, hofu kwako ambae hata ukitajwa hutokei.Lolz

Duh,kuna siku nimetajwa sikutokea?? basi nisamehe sikuona dearest, mwaka ukiisha bado tutakuwa pamoja tu...lol...nina pa kwenda basi??
 
Back
Top Bottom