NIMR mko wapi?

muda mzuri wa kujikojolea ni wakati mvua inaponyesha
 
Ni aibu ya nchi. Rais bogus, wasomi nao bogus wanatumia approach za karne zilizopita kupambana na maradhi. Hawa ndiyo walitakiwa wajikite kwenye utafiti ili kujua ugonjwa wa corona umeathirije watanzania na kwanini. Kama vifo vilivyotokea watafiti ni kwanini vimetokea na vimetokea kwa watu wenye profile gani ya maisha, ni nini hasa kimesababisha wafe nk, na wale waliopona ni kwa nini walipona, walikuwa na nini cha ziada nk. Kwa ujumla walitakiwa wakusanye data muhimu ili angalau kuja na mapendekezo. Ila kwa upande mwingine tusiwalaumu sana kwani wakiamua kufanya kazi kitaalam si ajabu watafukuzwa na kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi. Huyu rais wa sasa kichwani zimepungua. Ona alivyoivuruga wizara ya afya kwa kuondoa wale wataalam wote na kuwabakiwa na kilaza mwenzake huyo mwanamke.
 
Exactly, ilibidi wajikite kuangalia disease profile ikoje Tz and suggest the reason behind! Huyu Jiwe ni failure in all aspects of his undertakings
 
Mimi si mwajiliwa lkn nina ufahamu wa haya mambo kidogo! Labda ni kweli wanaangalia matakwa ya mtu mmoja! Ni maangamizi makubwa
 
Kwenye mahojiano ya media unakuta mtaalamu, hata daktari anakwenda kuzungumzia mila, desturi na practice za asili yetu. Naona ajabu kwamba kizazi kimoja au zaidi tokea huko, kama vile hatujasogea mbele na tunaishia kutazama nyuma. Hata wazee wetu walifanya. Matokeo yake naamini kwa vyovyote vile wazee hao walijua zaidi ya tunavyojua sana, kwa sababu hawakuacha ujuzi huo kwa maandishi, na kwa miaka mingi mifumo yetu rasmi ya kitafiti haijatilia mkazo, na pengine kupuuza ujuzi huo. Sayansi kwa kawaida inaangalia nyuma kujifunza na kusogea mbele, sio kuangalia nyuma tu bila progress, bila kutengeneza ufahamu mpya. Ukiwa daktari ukaishia kusema hata wazee wetu walifanya, unakubali tumepoteza entire generations' worth of progress.
 
Wanakula sikukuu

kIongOzI Wa BaaDae
 
👇YES..!👍👍👍👍👍
... wajanja kweli kwenda na "mdundo wa ngoma". Walishajua inayo-hit kwa sasa ni ama nyungu au mitishamba kwanini wasiogelee humo humo? Wajanja kinoma.
 
We unafikiri research/kudevelop dawa moja budget yake ni pesa ya maandazi eeh,inahitaji huge investment ...serikali yako ime invest bei gani kwenye hizo tafiti au mnabwabwaja tu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali imetoa budget kiasi gani ,kwenye tafiti za afya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa umewashauri kisayansi!

Baada ya kuwazodoa na kuwakoromea, umeamua sasa kuwapa madini...nafikiri ndio lilikuwa lengo lako ili kuvuta attention yao.

Ni kweli walichofanya hakiendani na taaluma yao pamoja na maabara waliyo nayo, ila kusema ni bora wangekaa kimya kama wenzao wa Kenya na Uganda hilo sikubaliani nalo aslani.
Mwanzo wa safari yoyote ni hatua. Wasingefanya walichofanya usngepata nafasi ya kuwakosoa na kuwapa huu ushauri mzuri.
 
ila kusema ni bora wangekaa kimya kama wenzao wa Kenya na Uganda hilo sikubaliani nalo aslani.
To me, naamini kuna level ukifika au your position in the society kuna mambo hupashwi kuyafanya! Una PhD in epidemiology /molecular biology/biostatistics etc kuna mabo tunategemea kutoka kwako. If you do not meet those expectations, then you are doomed! Ndio NIMR!
 
Unaitendea haki 'nickname' yako..Retired
Unaonesha ni matured na mtu wa elimu bora ya siku hizo.

Mkuu nikuambie tu kuna sababu nyingi kushindwa kufanya inavyotakiwa;
- 'products' za elimu yetu ya sasa ni wale ambao badala ya kusoma na kuelewa wanatafuta material ili kufaulu mitihani, usitegemee wafanye jambo la kitaalam zaidi ya hiyo mitishamba waliyotengeneza.

- Ajira zetu siku hizi haziangalii uwezo wa mlengwa badala yake wanaajiri kwa "connection"

Hiyo ndiyo Tanzania ya leo!
Kama NIMR haindeshwi kisiasa basi kuna wataalam wasiokidhi vigezo vya hiyo taasisi.
 
Hii na zingine ukuziona? Kabla ujawatupia lawama.Ushaenda kwao kupata hizo taarifa
 

Attachments

  • Screenshot_20200521_075441.jpg
    48.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075428.jpg
    61.1 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075423.jpg
    40.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075654.jpg
    35.9 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200521_075418.jpg
    50.2 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075457.jpg
    39.5 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200521_075454.jpg
    42.4 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075445.jpg
    46 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200521_075651.jpg
    33.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075601.jpg
    57.6 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075557.jpg
    66.8 KB · Views: 2
  • Screenshot_20200521_075552.jpg
    63.4 KB · Views: 1
Kuwa na PhD sio kwamba uko bright au unajua vyote au umemaliza.Zile ni elimu tu za darasani.Ujawahiona msomi wa chuo kushindwa mitihani wa shule ya msingi.Wengi tu hapa tukipewa mitihani ya shule ya msingi lzm tufeli.Ndivo ilivo elimu.Elimu inakuwa ni maarifa uliyonayo si nje ya upeo wako
 
Nadhani tatizo lipo deep down kwa wabongo ambao wanajua dawa asili ni mitishamba na haihitaji researches.. kitu ambacho hawajui ni kwamba hata miti shamba inahitaji kujulikana mechanism of action , dosage , side effects ( both short & long term)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…