#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkurugenzi mtendaji wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema taasisi yake inafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania zikiwemo 4 za kufukiza kama zinatibu Covid 19.

Utafiti wa dawa hizo za asili ambazo zimetumika toka enzi za mababu zetu zinafanyiwa utafiti na wanasayansi wetu kupitia baadhi ya hospitali zetu, amesema.

Prof Mgaya amesema chanjo za magharibi zinazotumika sasa huko duniani hazijathibitisha kukinga covid 19 kwahiyo nazo ziko kwenye utafiti ila zikileta madhara hakuna taasisi itakayolipa fidia.

Prof Mgaya amewataka wananchi watakaofanikiwa kuona kichupa cha chanjo za ulaya wasome kwa makini maandishi yote wataona namna wawekezaji wanavyokana kulipa fidia endapo tatizo lolote litatokea.

Prof Yunus Mgaya alikuwa skiwakilisha mada chuo kikuu cha Dar es salaam katika kongamano linaloongozwa na Dr Rioba na kurushwa mubashara na TBC.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyu Prof ni kama anacheza na akili za watu kuwalazimisha kinamna kutumia nyungu, kuwaambia watu kinga za ulaya hazijathibitishwa na hawalipi fidia kwa madhara yatakayotokana na matumizi yake ni ujanja ujanja, mbona hajasema kama wao watalipa fidia kwa madhara yatakayosababishwa na nyungu, yaani mgonjwa wa Corona akipiga nyungu au akinywa juice ya malimao na asipopona mumlipe fidia.
 
Mzee unashinda kwenye tv kuanzia asubuhi mpk saa sita usiku [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Hahahaaaa. Tv iko kiganjani bwashee issue yoyote inayorushwa mubashara inaniambia faster!
 
Ni jambo jema lakini hizo challenge nyingine??. Kujifaragua tu, kwa hiyo yeye hiyo anayofanya majaribio ni chanjo na ameandika kuwa yuko tayari kumlipa yeyote atakaepata madhara kwa hizo clinical trials. Ana hela ya kutosha eeehh??

Labda kama anachofanya ni dawa ya kawaida na si chanjo. Inahitaji kutofautisha hilo pia. Na ni stage ipi amefikia.

Na hawa washemiwa wawe wanasoma mambo ambayo yanaweza kuleta utata kwao kabla ya kuyatoa.

Exemption ya vaccine kwenye compensation ni kitu kiko wazi kwa makampuni yanayotengeneza chanjo na si Covid peke yake.

Atuletee hiyo consent form yake.


20210307_182539.png
 
Hawa Watu wanasahau kwamba hili ni tatizo la kidunia.

Na hakuna nchi itakayokataa tiba au kinga yoyote itakayogunduliwa na yeyote ali mradi tu iwe na maelezo na ushaidi wa kutosha kuthibitisha ina uwezo huo....porojo hazitotufikisha popote.
 
Niliangalia na kusikiliza hicho kipindi.. Siasa nyingi,kutokujiamini,kujishuku... Muda mwingi watoa mada waliwaponda wazungu... Waliitwa majina.. Sikutegemea Dr(PhD) Ryoba naye angeingia kwenye mkumbo huo... Kiingereza aliita 'kibeberu ', wazungu..mabeberu.. Ilikuwa mipasho,badala ya hoja za kisomi
 
Sawa, wao walete hizo za wazungu sisi tunaomini za wazungu tutazitumia, wanaomini hizo zao za kishirikina wazitumie kimpango wao. Kuhusu suala la fidia hatujali maana hata nyumba zetu zikiungua idara ya zimamoto hawalipi fidia, vifaa vyetu vikiungua kwa umeme wa TANESCO huwa hatulipwi fidia, wala mazao yetu yakiharibika huwa hatulipwi fidia na wizara ya kilimo. Hivyo hilo suala la fidia wala asijali maana hakuna utaratibu wa kulipa fidia hata hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom