#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

Heri yako kwa sababu hana ngozi nyeupe.
 
Hizo wanzofanyianutafiti ni ule uji wa limau,tangawizi,kitunguu suamu na pilipili kichaa? yale makitu kama una vidonda vya tumbo ni zaidi ya adhabu
 
]Umepewa taarifa na mtaalamu wewe unajibu kwa hoja ya dharau. Kama una uhakika na uwezo wa hizo chanjo, jiandae kuchanjwa
 
Sasa huyu aliongea based on research ipi?

1615139755198.png
 
Kwa hiyo wao NIMRI watatoa fidia kwa hizo dawa zao?

Nimrifac na covidol zimeletea watu shida sana.

Afu wanauza gharama kubwa sana, nafuu hata ya hizo za wazungu. Kila mtu ashinde mechi zake.

Kama za Ulaya poa, kama za NIMRI poa pia.

Wao waendelee na tafiti lakini pia wasitufanyie majaribio sisi Watanzania. Waende Madagascar huko.
 
Wakati duniani watu wanafanya juu chini chini juu kusambaza chanjo kuepuka a new variant (third one) sisi tunakataa chanjo. Nasema ivi, Tanzania ipo njiani kuzalisha kirusi kisichosikia hili wala lile. Dunia itashika adabu yake kwa maamuzi ya TZ.
 
Mwandishi angemuuliza toka NIMR imeanzishwa walishawahi kutengeneza chanjo au dawa iliyopo sokoni, ambayo imethibitishwa na taasisi huru ya madawa kwamba iko salama kwa matumizi ya binadamu.
Labda angekuwa anatokea Kenya huko. Hawa waandishi wa Tanzania kwa sasa hawana uwezo huo.
 
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti dawa za chanjo (NIMR) Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona haikufuata taratibu zinazotakiwa.

Na kwamba ilitakiwa ifanyiwe majaribio ya kutosha kupitia kwa wanyama kama vile sokwe na panya kujiridhisha na baadae kwa kundi dogo la Binadamu katika baadhi ya nchi na kama ikiwa na matokeo mazuri ndipo inatolewa kwa kundi kubwa la watu na kutangazwa rasmi na kwamba mchakato huo unaweza kuchukua miaka kumi.

Pia amepongeza msimamo wa serikali wa kuendelea kula limao na tangawizi na kupiga nyungu kwa sana huku tukiendelea kusubiri NIMR wakamilishe utafiti wao wa chanjo dhidi ya COVID 19 ili tupate chanjo bora kuliko hiyo iliyoanza kutumika bila kupitia michakato yote aliyoitaja, akidai kwamba chanjo hizo zinazotolewa hazifai.

Sasa kama kula ndimu, tangawizi na kupiga nyungu ndiyo kinga dhidi ya Corona utafiti huo ulifanywa kwa muda gani na NIMR?

Na ikiwa tutasubiri miaka kumi kupata chanjo sahihi kwa mjibu wa NIMR ni madhara kiasi gani yatakuwa yamejitokeza?
Nawasilisha!

Chanzo: HabariLeo
 
Hujui kuwa Tangawizi na Limao imekuwa ikitumika miaka mingi kuponyesha mafua na magonjwa yanayohusiana na upumuaji?? Waulize wazee wako bahati mbaya umekalia kugoogle tu! Watumie wazee watakupa maarifa mengi sana.
 
Hujui kuwa Tangawizi na Limao imekuwa ikitumika miaka mingi kuponyesha mafua na magonjwa yanayohusiana na upumuaji?? Waulize wazee wako bahati mbaya umekalia kugoogle tu! Watumie wazee watakupa maarifa mengi sana.
Mkuu kama ndio hivyo ni kwa nini tumekua tukitumia mabilioni kila mwaka kuagiza madawa ya mafua, upumuaji, athma na magonjwa ya mfumo wa hewa badala ya kutumia tangawizi na limao?

Kwa nini serikali imekua ikitumia hela zote hizo huku dawa ya hayo magonjwa inajulikana miaka mingi?
 
Back
Top Bottom