#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

1: Mtu ambaye ameshindwa kujua kuwa chanjo iko exempted kwenye madhara kwa mchanjwaji kulipwa na kampuni inayotengeneza chanjo na hiyo ni SERA kwa chanjo zote hata hanisumbui. Na huyu ni Profesa na mkurugenzi mkuu wa tasisi ya utafiti...
Prof Kabudi, Prof Kitila Mkumbo, Prof Mgaya na Mchumi Wa Daraja la Kwanza Dkt Mwigulu wote ni products za jalala according to Kabudi
 
Sio majaribio yametekelezwa? Mamilioni walipata chanjo nchini Israeli. Vifo vya Covid vya wazee vimepungua sana (kabla ya chanjo walijaa hospitali). mamilioni wengine wamepata chanjo Ulaya na marekani. Kila sehemu tunasikia matokeo ya kawaida ya chanjo: Idadi ya maambukizi zinashuka, watu wachache sana wanpata madhara (jinsi ilivyo kila chanjo).
chanjo gani hiyo ya kulazimishana?!!!

inamaaana sisi tumekuwa watoto wadogo?!!

inamaaana kuna mtu mwengine anapenda sana uhai wetu sisi watanzania kuliko sisi wenyewe?!! kiasi kwamba wanatulazimisha tupate chanjo ili tuendelee kuishi?!

hapana sisi watanzania hatutaki hizo chanjo za majaribio, .
 
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti dawa za chanjo (NIMR) Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona haikufuata taratibu zinazotakiwa....
Kwani miaka yote ya Uhuru tuliwahi kutengeneza chanjo yoyote wanaccm wenzangu.

Tukumbuke hili swala linahusu maisha ya Raia tunaowangoza kwa hiyo uongozi wa chama na serikali tuwe makini na tukumbuke lawama mpaka hapa tulipo hatuwezi kuzikwepa baathi ya Nchi jirani zimeshaanza kupokea chanjo.

Je sisi tutakuwa mgeni wa nani kwani hatuna chanjo inayodhibitika kidunia
 
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti dawa za chanjo (NIMR) Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona haikufuata taratibu zinazotakiwa.

Na kwamba ilitakiwa ifanyiwe majaribio ya kutosha kupitia kwa wanyama kama vile sokwe na panya kujiridhisha na baadae kwa kundi dogo la Binadamu katika baadhi ya nchi na kama ikiwa na matokeo mazuri ndipo inatolewa kwa kundi kubwa la watu na kutangazwa rasmi na kwamba mchakato huo unaweza kuchukua miaka kumi.

Pia amepongeza msimamo wa serikali wa kuendelea kula limao na tangawizi na kupiga nyungu kwa sana huku tukiendelea kusubiri NIMR wakamilishe utafiti wao wa chanjo dhidi ya COVID 19 ili tupate chanjo bora kuliko hiyo iliyoanza kutumika bila kupitia michakato yote aliyoitaja, akidai kwamba chanjo hizo zinazotolewa hazifai.

Sasa kama kula ndimu, tangawizi na kupiga nyungu ndiyo kinga dhidi ya Corona utafiti huo ulifanywa kwa muda gani na NIMR?

Na ikiwa tutasubiri miaka kumi kupata chanjo sahihi kwa mjibu wa NIMR ni madhara kiasi gani yatakuwa yamejitokeza?
Nawasilisha!

Chanzo: HabariLeo
Prof. Mgaya namheshimu sana. Lakini akubali kuwa tafiti za chanjo zilizofanyika duniani zimefanywa na wataalam kama yeye. Sasa hoja yake ya kuzidharau inaanzia wapi? Teknolojia zinaongezeka kila leo duniani. Tafiti za kuchukua miaka 10 ili kuokoa maisha zimepitwa sana na wakati. NIMR nawapongeza kwa dhati kwa kutupatia products (natural) ambazo zinatufaa katika kipindi kifupi (chini ya miezi 6). Tafiti za Ki-Sayansi zinapingwa kwa tafiti za kisayansi na si vinginevyo. Porojo za Kisiasa uchwara tuziache katika hoja kubwa jamani
 
chanjo gani hiyo ya kulazimishana?!!!

inamaaana sisi tumekuwa watoto wadogo?!!

inamaaana kuna mtu mwengine anapenda sana uhai wetu sisi watanzania kuliko sisi wenyewe?!! kiasi kwamba wanatulazimisha tupate chanjo ili tuendelee kuishi?!

hapana sisi watanzania hatutaki hizo chanjo za majaribio, .

Hakuna aliyelazimisha ila kila ukifanyacho kwa mtizamo mkubwa baadaye unaweza kuathiri wenzio.

Ni sawa na kuwa na mgonjwa wa kipindupindu na ni paranoid hataki kumeza dawa na unajua baadaye anaweza kuambukiza wengine au yeye kufa.
Je utamwacha? Kwa kuwa ni yeye?

Baadaye, utasikia mbona nyie wenye akili timamu hamkutumia busara zenu kumsaidia mgonjwa. Utajisikiaje?

Kwa hiyo watu wanatimiza wajibu wao.
 
Wewe na nani? wengine tuko tayari hata kuinunua kwa bei yoyote ile
sisi watanzania hatutaki chanzo ambazo ni za kulazimishwa! hivi hao wanao tushinikiza kutumia hiyo chanjo ndio wana thamini zaidi uhai wetu kuliko sisi wenyewe?! tafakari kwa makini.
 
1: Mtu ambaye ameshindwa kujua kuwa chanjo iko exempted kwenye madhara kwa mchanjwaji kulipwa na kampuni inayotengeneza chanjo na hiyo ni SERA kwa chanjo zote hata hanisumbui. Na huyu ni Profesa na mkurugenzi mkuu wa tasisi ya utafiti.

2: Mkurugenzi mkuu, ambaye hajui kuwa kuna emergency permit provision ya vaccine baada ya watu kukaa na kufanya analysis dhidi ya kusubiri miaka 15-18 ili chanjo iingie sokoni. Na utaratibu huu upo, kitu kama hicho pia kilihusisha chanjo ya Ebola ilipoonyesha ufanisi.

Angekuja na facts kuwa sababu zilizotumika kisayansi hazijitoshelezi au NIMR tumegundua:

A: Kwenye drug discovery/molecules and development kuna hiki kitu kwenye zile chanjo na hazifai.

B: Uwezo wake tulielezwa ni kiasi hiki na sisi kwa uwezo wetu tumegundua uwezo wake ni kiasi hiki, hivyo hazifai.

C: Kuna molecule hii inaleta shida hii, hivyo hazifai.etc.

D: Kwenye clinical trails, chanjo ilionyesha WEAKNESS hii na haikurekebishwa mpaka inaenda sokoni.

Na tukumbuke kadri muda unavyoenda, wakati sisi tunalala sana, wenzetu wanazidi kugundua more sophisticated tools kumaliza kazi zao mapema na kwa ufanisi.

Lakini, wanakuja mbele yetu kama wanasiasa tu. Please, let's invest in science and technology.

Tuache ku-mbwela mbwela tu.
Asante sana kwa genuine comments
 
Prof Mgaya amesema kuwa hii chanjo inayotumika sasa inatumika kwa ajili ya majaribio na mpaka sasa haijathibitishwa kuwa na mafanikio.

Hivyo Tanzania itakuwa tayari kutumia chanjo dhidi ya covid 19 baada ya kupata uhakika ni chanjo gani ambayo inatoa kinga dhidi ya Covid 19.

Chano Azam tv.
 
sisi watanzania hatutaki chanzo ambazo ni za kulazimishwa! hivi hao wanao tushinikiza kutumia hiyo chanjo ndio wana thamini zaidi uhai wetu kuliko sisi wenyewe?! tafakari kwa makini.
Ondoa porojo zako hapa. Watu wanazungumza Sayansi wewe unaleta za kuleta ili mradi umeandika. Leta hoja kwa nini tukatae chanjo, madhara yake au athari tokezi kisayansi siyo porojo zisizo na mashiko
 
Hakuna aliyelazimisha ila kila ukifanyacho kwa mtizami mkubwa baadaye unaweza kuathiri wenzio.

Nu sawa na kuwa na mgonjwa wa kipindupindu na ni paranoid hataki kumeza dawa na unajua baadaye anaweza kuambukiza wengine au yeye kufa.
Je utamwacha? Kwa kuwa ni yeye?

Baadaye, utasikia mbona nyie wenye akili timamu hamkutumia busara zenu kumsaidia mgonjwa. Utajisikiaje?

Kwa hiyo watu wanatimiza wajibu wao.
Jaribu kufanya kautafiti kadogo tu;

1. je, hizo nchi zilizo gundua chanjo na kisha kuanza kuchanja watu wake, je? maambukizi ya corona na vifo vimepungua? au ndio kwanza maambukizi yanazidi na vifo vinazidi.

mataifa yanayo ongoza kwa kutoa chanjo mpaka sasa ndio yana ongoza kwa maambukizi na vifo kuliko Tanzania.

Mataifa yenyewe yaliyo gundua chanjo bado wanabishana juu ya uhakika wa chanjo zilizo gunduliwa. bado ni "trial and error" wacha sisi watanzania tutulie kwanza, kamwe hututo kubali kuingia kichwa kichwa.
 
Ikiwa hivyo ndivyo ni jambo jema cha msingi tujipe muda.
 
Jaribu kufanya kautafiti kadogo tu;

1. je, hizo nchi zilizo gundua chanjo na kisha kuanza kuchanja watu wake, je? maambukizi ya corona na vifo vimepungua? au ndio kwanza maambukizi yanazidi na vifo vinazidi...
Hii si sababu ya kutosha.
Wakati unafanya huo utafiti.
Fikiria:
1: Population ya taifa husika
2: Size ya taifa husika
3: Ugonjwa ulisambaa kiasi gani kabla ya chanjo?
4: Priority amepewa nani kwanza?
Hii si zima moto.
 
Back
Top Bottom