NIMR yatengeneza dawa ya kupunguza makali ya Corona

NIMR yatengeneza dawa ya kupunguza makali ya Corona

DAWA iliyofanyiwa kazi na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imetoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona.

Dawa hiyo iliyopewa jina la NIMRCAF, inatokana na mchanganyiko wa vyakula; na katika majaribio imeonesha ina uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vya corona.

Akielezea mchanganyiko huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili cha NIMR, Dk Justine Omolo alisema ni fomula ya tiba lishe, ambayo ina mchanganyiko wa pilipili kichaa, tangawizi, limao na kitunguu saumu, asali na maji. Alisema dawa hiyo inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona, kwa kutibu dalili zinazotokana na ugonjwa huo.

Kwamba tayari imeshaonyesha matokeo chanya. “Mchanganyiko wa tiba lishe hiyo sio dawa ya corona, lakini inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona kwa kuwa inatibu dalili zinazoambatana na ugonjwa huo,” Dk Omolo.

Alisema mpaka sasa tiba lishe hiyo, imeshaleta matokeo chanya kwa kuwa imesaidia wagonjwa wengi wa corona. Alisema kwa sasa mahitaji yamekuwa ni mengi, tofauti na awali.

“Mwanzo tulikuwa tukitengeneza chupa 1,000 na tumekuwa tukisambaza hospitali kwa wagonjwa kwa siku chupa 120 hadi 200, lakini sasa mahitaji yamekuwa makubwa na imeonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa,” alisema

Alisema kutokana na mafanikio hayo, serikali imewaongezea vifaa ambapo kuanzia wiki ijayo wataanza kuzalisha chupa 5,000 kwa siku. Alisema chupa hiyo yenye ujazo wa nusu lita, inauzwa Sh 10,000 na ni dozi ya mtu mmoja ambayo inanyweka kwa siku tano, ambapo mgonjwa atalazimika kunywa mara tatu kutwa.

Dalili za ugonjwa huo wa corona ni joto mwilini na kikohozi kikavu; na baada ya wiki moja kikohozi hicho, kinaweza kusababisha tatizo la kushindwa kupumua.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO) kwa wagonjwa 56,000, ulibaini kuwa asilimia 80 ya wale walioambukizwa, hupata dalili zisizo kali kama vile kukohoa, joto mwilini na mara nyingine homa ya mapafu, asilimia 14 hupatwa na dalili kali, kama vile tatizo la kupumua.

Asilimia sita hukumbwa na tatizo la mapafu kushindwa kufanya kazi na viungo vingine mwilini na hata kusababisha kifo. Miongoni mwa dalili nyingi zilizoripotiwa na wagonjwa, asilimia 88 walidai kuwa na joto mwilini, asilimia 68 kikohozi kikavu na asilimia 38 waliripoti uchovu.

Tatizo la kupumua liliwapata asilimia 19 ya wagonjwa, asilimia 13 waliripoti kuumwa na kichwa na asilimia nne waliripoti kuharisha.

Omolo alisema kwa mtu ambaye hana dalili, anapaswa kutumia dawa hiyo mara moja kwa siku na hiyo itamsaidia kujikinga na ugonjwa huo wa corona, ambao takwimu za WHO zinaonesha hadi Mei 6, mwaka huu, ulikuwa mewakumba watu 3,588,773.

“Watu wanapaswa kujua kwamba virusi vya corona au Covid 19 ni mojawapo ya homa, hivyo basi vina dalili nyingi zinazofanana na homa ya kawaida’’, alisema

“Lazima uwe makini iwapo unahisi tatizo la kupumua. Ni muhimu kutafuta msaada wa matibabu haraka.

Tiba lishe hii haina madhara, watu waitumie ili kujikinga na janga hili la corona, “ alisisitiza Watalamu wanasema zipo njia nne za kudhibiti vimelea vya magonjwa hasa virusi ambavyo havina tiba.

Njia ya kwanza ni chanjo na ya pili ni kuzuia virusi visiweze kujishikiza kwenye seli zilizopo mwilini.

Njia ya tatu ni kudhibiti visizaliane au kuongezeka mwilini na njia ya nne ni kuongeza protini mwilini ili kusaidia kupambana na virusi hivyo. Kwa mujibu wa Dk Omolo, NIMRCAF ina vitamini C kwa wingi na vitamini K, na kitaalamu mchanganyiko unaopatikana katika tiba lishe hiyo unaitwa ‘Polyphenols’.

Mchanganyiko huo unazuia damu kuganda.
Alisema seli zinazopokea virusi vya corona, zipo kwenye mapafu na virusi vikiingia humo, husababisha damu kuganda na kuleta matatizo kwenye mfumo wa upumuaji.

“Mgonjwa akitumia tiba lishe hii, ndani ya nusu saa lazima atasikia nafuu. Wagonjwa wengi waliokuwa hoi walipoitumia, wamepata matokeo mazuri na wengine wamepona kabisa,”alisema Alisema walianza utafiti wa dawa hiyo muda mrefu, kabla dunia haijakumbwa na janga la corona.

Walifanya utafiti huo kwa kushirikiana na watalamu mbali mbali wa tiba asili. Walikuwa katika kutafiti tiba ya Ukimwi. NIMR imekuja na dawa lishe hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya WHO kutoa taarifa yake, ambayo ilieleza kuwa wanatambua na kuthamini mchango wa tiba asili kutoka Afrika.

WHO ilieleza kwamba dawa hizo, pia zinapaswa kupewa nafasi sawa katika kufanyiwa majaribio, kama dawa kutoka maeneo mengine duniani.
 
Taasisi ya Utafiti NIMR imefanikiwa kutengeneza dawa lishe itakayowasaidia wenye maambukizi ya Corona kukabiliana na virusi hivyo.

Mkuu wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema dawa hiyo inasaidia kufungua kifua kwa wale wanaobanwa pumzi na kuwapa wepesi wa kupumua.

Prof Mgaya amesema dawa hiyo ina mchanganyiko wa Tangawizi, kitunguu maji, kitunguu swaumu, limao na Pilipili kichaa.

View attachment 1442912



Source: Channel ten habari!
Sasa watu wamebanwa pumzi na mafua alafu kuna mchanganyiko wa pilipili kichaa. Mh huyo mtoto wa Mzee Mgaya mwambie tunashuru.
 
Nanukuu:

“Mwanzo tulikuwa tukitengeneza chupa 1,000 na tumekuwa tukisambaza hospitali kwa wagonjwa kwa siku chupa 120 hadi 200, lakini sasa mahitaji yamekuwa makubwa na imeonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa,” alisema

Mwisho wa kunukuu!!

My take:
Kwa kauli hiyo, ni dhahiri tuna wagonjwa wengi sana wa covid19 ambao ni rasmi, isipokuwa hawajatangazwa tu,

Kama kwa siku za mwanzo walikuwa wanagawa dawa obvious kwa watu 120+, ina maana kwa siku tano ni watu 600, na sasa mahitaji yameongezeka, yaani wagonjwa wameongezeka!!

Wadau, tujikinge, corona is real!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzungu ameshindwa ngozi nyeusi ndio ataweza?
Ndio.Ataweza
Siyo kuwa hawafahamu bali hauwezi kuweka hatimiliki (patent) kwenye chakula na hivyo haina maslahi.
Duh.. pilipili kichaa tena? Mtu anayebanwa kifua si atakohoa sana?
Dah pilipili kichaa tena?
Pilipili kichaa tena?
Pilipili kichaa, tangawizi na kitunguu saumu vinaongeza mzunguko wa damu.
Sasa hapo wana utofauti gani na waganga wa kienyeji. hizo elimu zao za Phd zimeonyesha utofauti gani na darasa la 7.

maana kila mtanzania sasa hivi anajua kwamba ukila limao na tangawizi inapunguza ukali wa corona.
Siyo kubahatisha, tangawizi na kitunguu saumu vinachembe chembe zinazotanua kuta za mishipa ya damu (vasodilation) na hivyo kusaidia damu nyingi kuweza pita kwenye alveoli (air sacs) kurahisisha damu nyingi kusafishwa. Corona huwa inasababisha ute ute kujaa kwenye mapafu (alveoli)na hivyo kupunguza uwezo wake kusafisha damu.
 
Kwa nini miezi yote hiyo walikuwa kimya hadi wamesikia waganga wa darasa la 7 wamesema na wao ndio wanakuja kucopy na kupaste sasa hivi
Siyo kuwa hawafahamu bali hauwezi kuweka hatimiliki (patent) kwenye chakula na hivyo haina maslahi.



Pilipili kichaa, tangawizi na kitunguu saumu vinaongeza mzunguko wa damu.
Siyo kubahatisha, tangawizi na kitunguu saumu vinachembe chembe zinazotanua kuta za mishipa ya damu (vasodilation) na hivyo kusaidia damu nyingi kuweza pita kwenye alveoli (air sacs) kurahisisha damu nyingi kusafishwa. Corona huwa inasababisha ute ute kujaa kwenye mapafu (alveoli)na hivyo kupunguza uwezo wake kusafisha damu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh.. pilipili kichaa tena? Mtu anayebanwa kifua si atakohoa sana?
Aliyebanwa kifua akikohoa husaidia mapafu yake kutanuka kidogo badala ya kuendelea kusinyaa. Moja ya zoezi linalopendekezwa ni kuvuta pumzi ndani kwa nguvu kwa kutumia mdomo na kutulia kwa sekunde kadhaa, halafu kutoa nje.

Rudia hivyo mara tano na safari ya sita baada ya kuvuta pumzi, kohoa kwa nguvu ili kuwasaidia mapafu yako. Angalizo: Jitahidi kwa kadri ya uwezo wako usilale kitandani na kuruhusu gonjwa hili kukubaliana, fanya mazoezi.
 
Hii nchi ya ajabu sana, imelemewa hadi inajiona inataka kufa.

Karne ya 21 unakaa chumbani unachanganya majani kisha unalitangazia taifa eti umegundua dawa.

Wazungu pamoja na elimu na uzoefu wao wanasema chanjo au dawa ya corona huwezi kuipata ndani ya mwaka mmoja.

Huu ni upunguwaani wa hali ya juu sana.

NIMR wasidhani kutemgeneza dawa ya kutibu binadamu ni sawa na kutengeneza mbege au ulanzi.

Hi togwa ya NIMR ni kufuru kubwa sana kwa watanzania.

Tanzania tunapotea.
20200509_112925.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila Nchi ina utaratibu wake, kule Sweden hawana habari na corona wanapiga kazi
 
Hii nchi ya ajabu sana, imelemewa hadi inajiona inataka kufa.

Karne ya 21 unakaa chumbani unachanganya majani kisha unalitangazia taifa eti umegundua dawa.

Wazungu pamoja na elimu na uzoefu wao wanasema chanjo au dawa ya corona huwezi kuipata ndani ya mwaka mmoja.

Huu ni upunguwaani wa hali ya juu sana.

NIMR wasidhani kutemgeneza dawa ya kutibu binadamu ni sawa na kutengeneza mbege au ulanzi.

Hi togwa ya NIMR ni kufuru kubwa sana kwa watanzania.

Tanzania tunapotea.View attachment 1444555

Sent using Jamii Forums mobile app
Watawanywesha wagonjwa mkorogo usiokuwa na viwango,hatuna uhakika na matokeo yatakayowapata watakaounywa.

Nadhani kuna umuhimu wa kuwawekea bima watakaopewa hizo dawa ambazo serikali inazileta kwenye tiba ya Corona,ili ikitokea yasiyotarajiwa angalau fidia zitolewe.Tusichezee maisha ya Watanzania.
 
Wameweka muda wa kuexpire uwe mdogo ili wabongo wasiichakachue
 
Back
Top Bottom