Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Kwanini Kusiwe Na Watu Huru Ambao Wanaweza Kupiga Mahesabu Na Kujua Kinachoongelewa Hapa Zaidi Ya Kulimbana Katika Magazeti ?
 
The latest report of the government controller and auditor-general (CAG) has raised audit queries on a total of 8,128,375,237/- paid by the BoT to Mkono & Company Advocates in stated legal fees up to the end of last year.

Kwa nini ndugu yangu Mkono asilalamikie ripoti ya CAG ambayo ndiyo source ya Slaa? Vile vile Mkono ana sifa ya kushtaki, kama kweli anaona Slaa hakumtendea haki, kwa nini asiende mahakamani?

Badala yake anatwist kuwa Slaa kamtukana rais na kutaka vyombo vya dola vimshughulikie. Mzee huyu ana element ya udikiteta; akipata madaraka makubwa zaidi atanyanyasa sana watu.
 
Mkono reacts to corruption allegations

22 Sep 2007
By Judica Tarimo

The MP for Musoma Rural, Nimrod Mkono, yesterday defended himself against grand corruption allegations levelled against him and several other people, who include government leaders.

Chadema MP, Dr Wilbroad Slaa, had given a list of individuals who were involved in massive graft, among them Nimrod Mkono, whom he said had been paid 8,128,375, 237/- for defending the Bank of Tanzania against a 60bn/- suit lodged by Valambia, who has already passed away.

Asked whether he planned to go to court, Mkono said: `If I go to court, what will this Father (Slaa) pay me?

Even this small newspaper (Mwanahalisi, which gave full details of the Mwembe Yanga meeting), they have got nothing.

They cannot pay me. What I want to say is that what this Father said at the people`s court of Mwembe Yanga were pure lies
.`

He added: `The people Slaa addressed at Mwembe Yanga were jobless, why didn`t he go to the university where academics could question his statements?

Why didn`t he call a press conference like this one where he could reply to queries? He went at Mwembe Yanga in order to mudsling the government and myself.`

He said the aim of the opposition parties, which were currently holding public rallies dwelling on graft in government circles, was to seek cheap popularity rather than expose gross embezzlement of public funds.

He said his defending of clients like Ditopile Mzuzuri and Chavda were only part of his professional duty, although a picture was being painted of making him an accomplice of the clients whom he was defending.

`I am quite surprised. My clients, the BoT, are not complaining that they are paying me a lot of money. It is odd that the opposition leaders are taking this issue as an agenda,` a restless Mkono said, as he at times shifted to another seat or stood up and down.

`I am not speaking for the others, but the accusations levelled against me by Slaa in his recent public rallies are baseless,` said Mkono.

Mkono rejected allegations that he was the director of several companies-Liberty Shoes, Azania-Noble, Tanfarm, and Makinyimbo.

`If you go to the Business Registration and Lisensing Authority (BRELA) you will never see my name among directors of those companies.

I am neither a director nor shareholder of those firms. The Opposition`s claims are wrong. They lack facts and thorough research,` said Mkono.

`This is is a great shame for Slaa, who is a respected former Catholic priest. He is telling lies to the public,` said Mkono.

However, the lawyer could not be drawn to diclose the exact amount which his law firm, Mkono and Advocates, had been paid by the Bank of Tanzania.

He said the BoT was required to pay his team of seven lawyers 500 US dollars per hour each for the three laywers working in Dar es Salaam and another 1000 US dollars per hour each to four advocates operating from Ireland and Czechoslovakia.

`On average, I spend 8 hours daily on the case. My client (BOT) is ready to pay the money,
` he said.

He said: `If the government is not ready to release money for defending against claims lodged by Valambhia, then the court will order the arrest of BOT Governor Daudi Balali.

Which is the best alternative? Should we leave Balali to be jailed or pay 141.2bn/- to Valambhia`s relatives?` questioned Mkono.

Dismissing fears that the legal fees might eventually outstrip the suit amount, given the fact that the end of the case was nowhere in sight, he said: `It is better that we fight to the end rather than give up, even if it means paying a lot of money.

There is a Kipare saying which states that you can sell a cow to meet legal bills for a case concerning a stolen hen.`


Talking to The Guardian, Dr Slaa decried embezzlement of the `highest order` by members of the ruling party.

`Rather than take us to court, CCM is again using tax-payers money to clarify claims on genuine embezzlement occurrences in public institutions. This is corruption of the highest order,` he said.

CCM Publicity Secretary Aggrey Mwanri has announced a countrywide campaign to counter the allegations.

However, Dr Slaa faulted the planned CCM mission as ill-motivated and nonpractical.

`Since the governemnt is formed by the ruling party, which is well-equipped in terms of an anti-corruption watchdog (PCCB), intellegence units and related organs, we expected that CCM would utilise these organs to investigate the scandals,` said Slaa.

When contacted yesterday, Deputy CCM Publicity Secretary, Aggrey Mwanri said the envisaged CCM public education campaign sought to clarify the embezzlement allegations using the same channels which were utilised by the Opposition.

`If the Opposition went to the wananchi to spread distorted and unfounded allegations, what channel should we use to clarify these issues? CCM is going to the same wananchi to educate them on the truth of the matter,` he said.

On whether CCM planned to send Dr Slaa and others to court, Mwanri declined to comment, but insisted that the opposition parties should submit written evidence to back up their claims.

* SOURCE: Guardian


  1. The more I read Mkono's statements, the more I find him troubling.
  2. How did he come up with the rate of $500 and $1000 an hour, does he operate in US or in Tanzania, why not TShs? Does Ditopile pay the same rate, or it applies only to BoT- the cash cow.
  3. Why use lawyers in Ireland and Czechoslovakia while the case was in Tanzania High Court?
  4. I still don't know why he does not want to take legal action? Even if they don't have money to pay him, it is a sure way of clearing his name.
  5. Is he a pare?
 
Mkono ni kapu la mjanja na kwa kuwa mambo haya ndiyo kwanza yanaanza basi mengi yataanikwa hapa .Itabidi sasa tuangalie hesabu kwa uwazi na magazeti yaseme. Ni kweli mkono anakwepa kuongelea ripoti CAG ambayo ndiyosource ya kila kitu ambacho Slaa anacho . Mbona hakuna hata mmoja wao anayetaka kenda mahakamani ? Kama hawataenda mimi na Slaa tutaenda tuwaitie huko huko.

Mkono wazungu kumwabudu JK ni kwamba wao wana mambo yao ya kutuibia kwa jina la uwekezaji na hawana nia nyingine njema so lazima kusifia na wapate kamradim kao wsatuache hoi.JK ni Rais wetu tunamjua zaidi na serikali yake na si kwamba wazungu wanamwabudu basi hata mimi nimwabudu hata kama najua alichukua hata nyumba na bado akakataa na kuja kukiri baadaye baadaya kuupata urais.
 
Hakuna nchi ulimwenguni ambayo ni tajiri au masikini kama sisi ambayo inakubali kuwakilishwa mahakamani na mawakili wa kujitegemea kama Nimrod mkono, ndio sababu serikali kama sikosei ina attorney General ambaye ndiye anatakiwa kuiwakilisha serikali katika kesi mbali mbali na kuwaweka mawakili kutoka ofisi yake.

Kama serikali ikiona kuna umuhimu huo huwa inaweka viwango maalum ambavyo vitalipwa kwa mwanasheria yoyote ambaye atapewa jukumu hilo vikizingatia uchumi wa nchi husika. Lakini kama mshitakiwa ni kiongozi wa serikali na anashitakiwa binafsi anayo ruhusa kumwajiri wakili wa kumtetea binafsi kama akipenda kwa gharama yake mwenyewe.

Suala ni je ilikuwaje Balali atetewe na Mkono? alikuwa anamtetea yeye binafsi au BOT? Kama alikuwa anamtetea yeye binafsi nani analipa hizo gharama? Kama zinalipwa na BOT au serikali nani aliidhinisha na kwa sheria ipi? Kama alikuwa anatetea BOT nani aliidhinisha hiyo contract na nani walikubali malipo hayo yafanyike? Je ni viwango gani vilitumika kutathmini kiasi cha kulipwa kwa Mkono au wakili mwingine yoyote ambaye ni private? Je huyu wakili ambaye ni private anapewa access ya nyaraka ambazo ni sensitive kwa wale walioajiriwa na serikali tu?

Mkono ambaye ni mbunge na mwanasheria atakuwa mtu wa kwanza kufahamu kama kanuni na sheria za nchi zilikiukwa katika kufanikisha malipo haya, Je Bunge letu linafahamu ni kiasi gani imelipwa kampuni moja tu na sio kampuni nyingine za mawakili kiasi kikubwa namna hii cha pesa?

Kamati ya bunge ambayo ndiyo inapitisha bajeti ina jukumu la kuunda tume kuchunguza mwenendo mzima wa malipo haya na kumchunguza mbunge Mkono na ikijulikana yeye kwa njia moja au nyingine kukiuka taratibu na kujipatia pesa kwa malipo ya mtu binafsi kutoka serikalini itabidi azirudishe pesa alizolipwa na serikali au BOT na Balali amlipe mwenyewe binafsi kama mteja wake na sio kutumia vibaya pesa za walipa kodi.

Binafsi sifikirii serikali inaweza kuridhia malipo kama haya ya kiwendawazimu.
 
Kwa nini ndugu yangu Mkono asilalamikie ripoti ya CAG ambayo ndiyo source ya Slaa?

Exactly ndio haswa swali langu, the real ishu ya Dr. Slaa inaanzia kwenye kamati ya bunge iliyomchunguza kwa kutumia katiba ya jamhuri, na kuripoti kuwa ishu nyingi za Mkono na BOT zina utata,

Sasa kwa nini bunge lilimuachia bila ya kumfikisha mahakamani? au angalau kumuita na kumhoji under oath, kama walivyomfanyia Kitine?

Tanzania bwana, yaani mambo mengine haya ni aibu hata kuyasema in public, maana serikali yetu inafikia mahali inakuwa kama Banana Republic, yaani ishu kama hizi una-explain vipi kwa mtu mwenye akili timamu!
 
Mkono kama mwanasheria anajua fika uzito wa hizi tuhuma ndiyo maana anatapatapa. Maswali yanayoulizwa humu JF kama huyu mzee akiyaona sintoshangaa kusikia naye mgonjwa mahututi hospitali. Na hao waandishi wa habari wa bongo waje wajifunze kuuliza maswali kutoka hapa.

Way to go JF, mpaka kieleweke!
 
.....

Binafsi sifikirii serikali inaweza kuridhia malipo kama haya ya kiwendawazimu.

Samahani Dua, itabidi niulize tu tena najua mnaweza kuwa mmeshaliongelea.... je, malipo yake akiwa hapo hapo Tanzania bado yanafanyika kwenye hizo 'dolla' au hicho kiwango tayari ni comparison tu ya 'madafu' anayopata ?! Ahsante.

SteveD.
 
Na hao waandishi wa habari wa bongo waje wajifunze kuuliza maswali kutoka hapa.

Way to go JF, mpaka kieleweke!

Hilo wazo huwa najiuliza, kwanini waandishi wasije hapa JF wakaona watu wanavokata issue wapate desa la kuwashukia mafisadi?

Ama wanakuja ila wanaishia 'Usalvatory' ili wakumbukwe katika kiti cha enzi?
 
Binafsi sifikirii serikali inaweza kuridhia malipo kama haya ya kiwendawazimu.

Ndo hapo utakapo shangaa ya Mussa!

Ndugu yangu Dua, hayo unayo dhani kwamba serikali haiwezi kuyaridhia ndiyo hayo inayo yafanya, na iko tayali kuyalinda kwa garama zozote zile at the expense ya wewe mlala hoi!

Ndo maana nadhani we really need a change! huku kuchoteana na kulindana kunaimaliza Bongo yetu!
 
Samahani Dua, itabidi niulize tu tena najua mnaweza kuwa mmeshaliongelea.... je, malipo yake akiwa hapo hapo Tanzania bado yanafanyika kwenye hizo 'dolla' au hicho kiwango tayari ni comparison tu ya 'madafu' anayopata ?! Ahsante.

SteveD.

Sasa hiyo shilingi itatengemaa lini wakati hata wabunge wetu wana-charge
gharama zao kwa kutumia pesa ambayo siyo ya Tanzania, na malipo yenyewe mengi ni malipo hewa. Nchi yetu hawa vizwezwe wanaipeleka wapi?
 
Mkono: Ninalipwa dola 500 kwa saa
Ashangaa Dk. Slaa kutokamatwa

Irene Mark
Tanzania Daima

TUHUMA zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), dhidi ya viongozi kadhaa wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinachukua sura mpya kila kukicha na jana mmoja wa watuhumiwa aliibuka na kutoa majigambo huku akiwaingiza watu wengine kadhaa katika shauri hilo.

Aliyefanya hivyo alikuwa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na mwanasheria maarufu nchini, Nimrod Mkono (CCM), ambaye mbali ya kutangaza kuwa amekuwa akivuna kiasi cha dola 500 za Marekani kwa saa (karibu sh 650,000) kutokana na kazi yake ya uwakili, aliwalaumu mawakili wawili akiwataja kuwa watu wanaoonea wivu mafanikio yake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkono aliwavuta katika wavu wa tuhuma hizo mawakili wawili maarufu wa kampuni moja jijini, na kubainisha kuwa wamekuwa wakimtumia Dk. Slaa, kutokana na vita kati ya kampuni yake (Mkono) na wao kuhusu kesi moja inayohusisha mabilioni ya shilingi.

Mkono alisema sababu za yeye kuingizwa kwenye orodha ya wabadhirifu, ni ushindi alioupata wa kuiendeleza kesi ya Devram Valambhia na Kampuni ya usafirishaji ya Equipment.

Kesi hiyo imekuwa ikiendelea kwa miaka 20 sasa na Mkono jana alikiri kuwa analipwa mabilioni ya fedha kutokana na kuisimamia.

Katika mkutano huo, Mkono alidai kuwa Dk. Slaa anatumiwa na mawakili wa kujitegemea, Moses Maira na Mabere Marando, ambao walishindwa katika jitihada zao za kuipata kesi hiyo yenye malipo makubwa.

Hata hivyo, alipozungumza na gezeti hili jana, Marando alikanusha tuhuma hizo zilizotolewa na Mkono na kueleza kuwa hajawahi kushindwa katika kesi hiyo.

Marando alisema wakati wanaisimamia kesi hiyo (yeye na Maira) waliishinda serikali baada ya gavana kukutwa na hatia na kupewa hukumu ya kifungo au kulipa faini, na aliokoka kwenda jela baada ya kulipa faini ya sh 400,000 mbele ya Jaji Massati.

“Sioni sababu ya Mkono kulipwa mamilioni ya fedha kila mwezi kutoka serikalini wakati kesi ilishamalizika,” alisema Marando.

Mkono aliwaambia waandishi wa habari kuwa, yeye ni wakili ghali kwani huwa analipwa dola 500 kwa saa kila siku wakati wa saa za kazi kama wakili katika kesi hiyo, hali inayosababisha chuki dhidi ya mawakili walioshindwa.

“Hii chuki yote mnayoiona inatokana na kesi ya Valambhia inayoshughulikiwa na kampuni yangu… mwaka 2003 Mabere na Maira walipoona wanashindwa wakaibana serikali na kumtaka Gavana Daudi Balali akamatwe, walitaka kumfunga gavana hawa mabwana.

“Walichokuwa wanataka Valambhia alipwe deni feki ili wapinzani wagawane hizo fedha… nilipoanza nayo mwaka huo huo nilijiwekea malengo, kwanza gavana asikamatwe katika hilo nilishinda.

“Jingine ni kwamba, serikali ianze mwanzo ili kujua chimbuko la kesi hii… napo nilishinda kwani mahakama ilianza kusikiliza kesi hii. Kesi hii ni ya siku nyingi sana, lakini hatuwezi kumwachia mhalifu, lazima tuendelee kudai,” alisema Mkono huku akionyesha baadhi ya nyaraka zinazohusu kesi hiyo kwa waandishi wa habari.

“Ndiyo… ninalipwa dola 500 kwa saa kila siku ya kazi na fedha hiyo nalipwa kwa saa nane,” alisema Mkono na kuongeza kuwa kesi hiyo inasimamiwa na wanasheria saba. Alifafanua kuwa watatu wapo hapa nchini, wawili wapo Ireland na wengine wawili wapo Jamhuri ya Watu wa Czech, ambako kesi hiyo inasikilizwa.

Kuhusu malipo ya wanasheria wengine wanaosimamia kesi hiyo, Mkono alisema wanaoishi nje ya nchi hulipwa dola 200 (karibu sh 260,000) kwa saa kila siku ya kazi kwa saa nane na kusisitiza kuwa hawezi kuiachia kesi hiyo, kama wanavyotaka wapinzani, hadi imalizike.

Aidha, Mkono alieleza kushangazwa kwake na kutokuwepo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano huo na waandishi wa habari kwani alimualika.

“Nashangaa kwa nini Father (Padri) Willibrod Slaa hajahudhuria mkutano huu, nilimwalika lakini simuoni… najua angekuja tungeshikana mashati hapa hapa, maana lazima tungebishana kuhusu hili,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa aliliambia gazeti hili kuwa, hakuwahi kupokea mwaliko wowote kutoka kwa Mkono kuhudhuria mkutano huo.

“Mkono ni rafiki yangu na anaijua namba yangu ya simu… ukweli ni kwamba wewe ndiyo wa kwanza kuniambia habari hizi, huyu bwana hajaniita kwa namna yoyote.

“Kwanini nikatae wito? Siwezi kwenda sehemu ambayo sijaitwa, nielewe hivyo… nasema Mkono hajaniita, aache kuwadanganya wananchi, sijapokea wito kutoka kwake,” alisisitiza Dk. Slaa kwa njia ya simu.

Lakini katika mkutano wake, Mkono alisisitiza: “Huyu (Dk. Slaa) ni Father wa Kanisa Katoliki, lakini anasema uongo mbele ya Watanzania milioni 35, hii ni kunichafulia jina langu kwa sababu ninawakilisha Watanzania kama 400,000 hivi, wanashangaa Mbunge wao kuitwa fisadi.

“Nafikiria hatua za kuwachukulia walioniita fisadi, sasa nimshitaki nani hapa, Slaa au Chadema au hili gazeti (alilionyesha gazeti la kila wiki la Mwana Halisi lililoandika na kuchapisha jina lake kama mtafuna nchi)… hata nikiwashitaki hawawezi kunilipa,” alisema huku akiwaonyesha waandishi waliokuwepo gazeti hilo.

Aidha, Mkono alisema kuwa alisikitishwa na kitendo cha kumtaja rais wa nchi kuwa mmoja kati ya mafisadi na kuonya kuwa, uhuru wa kuzungumza uliopo nchini, usitumiwe vibaya kwa kusema uongo na kutoa mfano wa yaliyosemwa na Dk. Slaa.

“Wapinzani wameniweka kwenye ‘list of Shame’ (orodha ya mafisadi), rais wa nchi naye yumo… kwa lugha hiyo unawaambia Watanzania wote wasimheshimu rais wao, ndiyo anavyosema Father Willibrod Slaa,” alibainisha.

Alisema zipo sheria za nchi zinazosema kuwa, ni kosa kumtukana rais akiwa madarakani, lakini anashangaa ni kwa nini wapinzani hawajakamatwa hadi sasa.

“Rais wetu yupo Marekani, kaenda kuombaomba huko tupate japo fedha za MCC kwa maendeleo ya nchi yetu… wenzetu wanamwekea red carpet (zulia jekundu), hapa tunamtukana, hii si vizuri, ni makosa sana kufanya hivi.

“Sipo hapa kumsemea rais… mimi si msemaji wake, lakini kwa vile amewekwa kwenye list of shame na kwamba yeye ni mkuu wa nchi imebidi nilizungumzie.

“Huyu father anasema Mkono ni mkurugenzi wa makampuni (aliyataja baadhi yake na kuonyesha orodha ya wakurugenzi wa kampuni hizo kutoka BRELA). Kampuni zote alizozitaja huyu father hazipo, ni kampuni za uongo, wakurugenzi wake ni Wahindi,” alisema na kuongeza kuwa mchango wake katika nchi ni mkubwa na kwamba bila yeye hajui Tanzania ingekuwa wapi sasa.

Alisema alitoa ushawishi mkubwa kwa kushirikiana na wenzake kuhakikisha yanajengwa mahoteli makubwa.

“Kazi ya wakili ni kutetea wahalifu, hivi na mimi ninapotetea wahalifu nakuwa mhalifu? Nilimtetea Chavda asiondoke nchini nikafanikiwa na mimi ni mhalifu?” Alihoji Mkono na kumtaka Dk. Slaa aache kuudanganya umma, badala yake aendelee na kesi inayomkabili ya uchaguzi katika jimbo lake.
 
Lakini Benki Kuu kumlipa kiasi hicho siwezi kushangaa.. kama tunajenga minara miwili kwa gharama mara nne ya majengo kama hayo NY... kweli hawataweza kumlipa wakili wao kiasi hicho, hasa wakili ambayo amekuwa mtetezi mkubwa wa Gavana?

Hivi mnafikiri kama Gavana akishtakiwa mahakamani mnafikiri ni wakili gani atakuwa tayari kumtetea?
 
Hivi huyu Mkono yeye ni nani kujiona bab kubwa mpaka kuchaji mihela yote hiyo...ujiko wake unatokana na nini...ni kesi gani aliyoshinda kwa kuonyesha umahiri wake ktk fani hiyo mpaka watu wawe wanambabaikia hivyo? Kuna mtu ambaye amewahi kushuhudia jinsi anavyo-argue kesi zake?
 
Hivi huyu Mkono yeye ni nani kujiona bab kubwa mpaka kuchaji mihela yote hiyo...ujiko wake unatokana na nini...ni kesi gani aliyoshinda kwa kuonyesha umahiri wake ktk fani hiyo mpaka watu wawe wanambabaikia hivyo? Kuna mtu ambaye amewahi kushuhudia jinsi anavyo-argue kesi zake?

Yuko bungeni kama mwakilishi na mtetezi wa waliomchagua na Watanzania wote kwa ujumla, lakini ameweka mbele maslahi ya tumbo lake na kucharge gharama kubwa kiasi hicho bila haya wala kuona vibaya! hata uzalendo hana! sijui hata huko bungeni anafanya nini kama walivyo wabunge wote wa CCM ambao maslahi yao wameweka mbele.

Haya mapesa chungu nzima aliyolipwa yangeweza kusomesha vijana wengi tu wa Kitanzania pale UDSM, yangeweza kununua madawa mbali mbali katika hospitali zetu, yangeweza kutumika katika kuwaongezea wafanyakazi wanaolipwa mishahara isiyoendana na gharama halisi za maisha, lakini mtu mmoja anakusanya mapesa yote hayo peke yake!
 
I am also curious to know how he (Mkono) argues his case in the court. Is he really good or he just blows his own stinking trumpet?
 
Hakuna nchi ulimwenguni ambayo ni tajiri au masikini kama sisi ambayo inakubali kuwakilishwa mahakamani na mawakili wa kujitegemea kama Nimrod mkono, ndio sababu serikali kama sikosei ina attorney General ambaye ndiye anatakiwa kuiwakilisha serikali katika kesi mbali mbali na kuwaweka mawakili kutoka ofisi yake.

Kama serikali ikiona kuna umuhimu huo huwa inaweka viwango maalum ambavyo vitalipwa kwa mwanasheria yoyote ambaye atapewa jukumu hilo vikizingatia uchumi wa nchi husika. Lakini kama mshitakiwa ni kiongozi wa serikali na anashitakiwa binafsi anayo ruhusa kumwajiri wakili wa kumtetea binafsi kama akipenda kwa gharama yake mwenyewe.

Swala ni je ilikuwaje Balali atetewe na Mkono? alikuwa anamtetea yeye binafsi au BOT? Kama alikuwa anamtetea yeye binafsi nani analipa hizo gharama? Kama zinalipwa na BOT au serikali nani aliidhinisha na kwa sheria ipi? Kama alikuwa anatetea BOT nani aliidhinisha hiyo contract na nani walikubali malipo hayo yafanyike? Je ni viwango gani vilitumika kutathmini kiasi cha kulipwa kwa Mkono au wakili mwingine yoyote ambaye ni private? Je huyu wakili ambaye ni private anapewa access ya nyaraka ambazo ni sensitive kwa wale walioajiriwa na serikali tu?
Mkono ambaye ni mbunge na mwanasheria atakuwa mtu wa kwanza kufahamu kama kanuni na sheria za nchi zilikiukwa katika kufanikisha malipo haya, Je Bunge letu linafahamu ni kiasi gani imelipwa kampuni moja tu na sio kampuni nyingine za mawakili kiasi kikubwa namna hii cha pesa?


Kamati ya bunge ambayo ndiyo inapitisha bajeti ina jukumu la kuunda tume kuchunguza mwenendo mzima wa malipo haya na kumchunguza mbunge Mkono na ikijulikana yeye kwa njia moja au nyingine kukiuka taratibu na kujipatia pesa kwa malipo ya mtu binafsi kutoka serikalini itabidi azirudishe pesa alizolipwa na serikali au BOT na Balali amlipe mwenyewe binafsi kama mteja wake na sio kutumia vibaya pesa za walipa kodi.

Binafsi sifikirii serikali inaweza kuridhia malipo kama haya ya kiwendawazimu.

Well Spoted, why not government Lawyers, wata danganya hawana experience au elimu. So why not sponsaor them?
 
Sasa hiyo shilingi itatengemaa lini wakati hata wabunge wetu wana-charge
gharama zao kwa kutumia pesa ambayo siyo ya Tanzania, na malipo yenyewe mengi ni malipo hewa. Nchi yetu hawa vizwezwe wanaipeleka wapi?

Dua, ndiyo maana nikataka kuuliza. Inasikitisha kwa kweli. Dhahabu, pamba, karafuu, minofu ya sangara, kahawa, tanzanite, almasi n.k. zinahangaikiwa kuuzwa nje ili Taifa letu lijipatie walau pesa za kigeni kwa ajiri ya kununulia vifaa na teknolojia mbalimbali kutoka nje, lakini badala yake pesa hizo zinaishia kwenye majitu kama haya ambayo yapo hapa hapa Tanzania na yanajifanya mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi hali halisi ni majizi makubwa na yanachangia kuporomoka kwa shillingi yetu kila siku.

Nakumbuka katika bunge lililoisha Waziri wa fedha alisema malipo katika mazingira ya Tanzania yafanyike kwa hela za madafu, je usemi wake huu unatekelezekaje wakati karibu hela yote ya kigeni nchi yetu inayopata kwa wiki inaishia kwenye mifuko ya mijitu kama minne tu na ipo hapa hapa Tanzania?!

SteveD.
 
Huyu Nimrod anadai yeye amejenga shule bora katika jimbo lake kushinda hata wawekezaji wa madini katika jimbo lake, kumbe dili zenyewe ndio hizi!. Hivi Mkono huyu ndio yule yule rais wa HESLB? Kaazi kweli kweli!

Akina Kayumba tulie tu. Tuuze mayai lakini tukipata nafasi basi walau tuwazomee watu wa dizaini ya ya huyu bwana.
 
Back
Top Bottom