Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch


KKN,

Usijali sana hapa mkuu kwani hata hao unaowaona senior members kuna wakati walikuwa juniors na walikuwa wakileta habari zao na zinawekewa doubts. Kuna wengi tu hata leo hii tukiweka habari hapa bado zinawekewa doubts.

Hii sidhani kama inaweza kudiscourage mtu yeyote mwenye uchungu na nchi. Haijalishi kama watu wanadiscourage au hawakupi thanks, kumbuka kuwa kama kitu unakiamini basi unaweza kukisimiamia mpaka mwisho na baadaye wale wenye hoja hafifu na wenye kukejeli wataondoka na hoja yako itasimama.

Tuendeleza mapammbano na mkuu malindi anaruhusa kabisa ya kuendeleza habari au story yake na so far naona watu wanachangia so dont worry about that. Discouragement ziko kila mahali na ukumbuke kuwa kuna wengine hapa kazi yao ni kuharibu kile kinachoandikwa na wenzao.

Asante
 

Laana ya kuwaibia Watanzania masikini na kula kama mchwa itwakumba kila mmoja na kwa zamu kwa kweli watakiona .Hakuba buyu pesa liliweza kuwa pale juu miaka kadhaa ,sasa la CCM linaelekea kukatika .
 

Hizo 'Thanks' siyo big deal lakini kinachoshangaza zaidi ni watu wanavyo kurupuka na kui label story ya mtu kuwa ni majungu na udaku.

Nadhani ni busara na utaratibu mzuri kwa member kusoma kile kilichoandikwa kwenye thread then kama kuna wanachotaka kufahamu zaidi wamuulize maswali mwenye kuanzisha hiyo thread na hata kama yeye hana majibu kuna uwezekano akatokea member mwingine akatoa majibu.
 

Hiyo ni kweli kabisa na ninakubaliana na wewe katika. Mimi sina tatizo na thanks za watu kwani hazibadili sana ukweli au uongo kwenye post iliyowekwa hapa. Usijali sana ukiona watu wakipewa hizo thanks mia mbili au wengine wakianza kujipanga na kukosoa. Huu ndio mchezo wa JF na bahati mbaya ni kwamba ni vigumu sana kufunga watu na kuwaamulia cha kufanya.

Mimi ningeshauri kama mtu ana story na ana uhakika na kila anachojaribu kusema hapa basi afanye hivyo na hata kama watu wakidoubt story yake basi yeye aendelee kushikilia msimamo wake na kutetea hoja zake kwani mwisho wa siku hoja zenye nguvu hubaki zimesimama.

Asante mkuu!
 

Sijasema kuwa kilichoelezwa ni udaku, nilichosema ni kuwa hiyo ni habari nyeti sana. Nikamtaka amwage vitu zaidi ili nasi ambao hatufahamu vya kutosha kuhusu vitu hivyo tufaidike.

Sikuwa na nia ya kumdiscourage mtu kwa sababu najua kuwa kwa mchango wake, na wa watu wengine, kibaba kitajaa na tutapata habari kamili. Tupo pamoja mkuu
 
Wasiwasi wangu mkubwa kwa sasa ni Serikali kutofanya kazi na Mawaziri na maafisa wengine wa ngazi za juu Serikalini kukaa kupanga jinsi ya kupangua kashfa za ufisadi zinazoweza kuwaandama wakati wowote.

Jamani, lets go back to work. Haya mambo ndiyo aliyofanya Kibaki wa Kenya na Raila wake for the whole of the past term in Kibaki's administration, kila kukicha ni kutafutana uchawi tu badala ya kufanya kazi.

Siku hizi hata magazeti hatusikii wakiandika habari za miradi yoyote ile mikubwa, kila mtu yuko bize kufichua mafisadi.
 
Haya maoni binafsi hayafai tunachjotaka ni uthibitisho wa hizi habari. Weka link hizi habari umezitoa wapi au sema wazi kuwa nililala nikaota habari hii. Longolongo kibao.
 


Aiyaaaah Umesha Pre-empty move muhimu sana aaah nyie watoto kwa ukimbelembele!
 

Miradi mikubwa itatoka wapi wakati pesa yote imeishia na mafisadi?
 

Ole wetu waTZ kama IMMMA na Nkono wataamua kugawana maeneo ya ulaji badala ya kuzozana. Cha moto tunachokiona sasa kinaweza kugeuka kuwa sawa na freezer
 
Kana ka Nsungu,

Mkuu binafsi sioni kosa ktk maelezo ya Mpita njia, nadhani kadadisi zaidi tupate yale aloyaficha kibindoni.
Pumua mkuu wangu pumua acha watu wamwange mavituzzzz!

Inaonyesha wazi mawakili wa TZ wanafaidika kishenzi imefikia hadi kutaka kutoana roho! Eeeeh ama kweli ngawila sii mchezo.
 
Siku hizi hata magazeti hatusikii wakiandika habari za miradi yoyote ile mikubwa, kila mtu yuko bize kufichua mafisadi.
Sio hivyo. Ila wewe pia kama una habari za maendeleo na miradi hiyo mikubwa na jinsi inavyokwamua andika nasi tutachangia. Miradi ya kitaifa kwa sasa si rahisi kuwepo kwani huoni kila kukicha 'wafadhili' wanafunga bomba la pesa.

Wao wanaziita serikali zetu ni kama 'bottomless pit'. Kwa hiyo ufisadi umetuonyesha kuwa pesa tunazo ila zinaelekezwa kusiko. Hiyo miradi ni ipi Kiwira coal, Richmond?
 
CCM wapigana mkwara ubunge 2010


*Asiyefanya kama Nimrod Mkono kutemwa

Na George John, Musoma

WAJUMBE wa Mkutano wa siku mbili wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kinatarajia kufanyika leo kijijini Butiama, mkoni Mara, wamesema wabunge watakaogombea ubunge 2010 watapimwa kwa walichokifanya majimboni mwao.

Walisema hayo juzi walipokuwa wakikagua miradi iliyoanzishwa na Mbunge wa Musoma vijijini, Bw. Nimrod Mkono, na kuonesha kuridhishwa na miradi hiyo jimboni mwake.

Wajumbe hao kila mmoja kwa kauli yake, walielezea kuridhishwa na kazi kubwa zinazofanywa na Bw. Mkono ambaye pia ni mjumbe wa NEC, baada ya kutembelea sehemu ya miradi ya shule iliyojengwa kwa nguvu zake jimboni humo.

Walisema baadhi ya viongozi hasa wabunge, wamekuwa ving’ang’anizi wa kuomba kuteuliwa kugombea kila baada ya kipindi chake kwisha bila kujali kama wametekeleza Ilani ya CCM kama ilivyooneshwa kwa vitendo na Bw. Mkono.

Kutokana na hatua ya Mbunge Mkono, walisema hakuna sababu ya kumtuhumu kwa ufisadi, kutokana na kutumia sehemu kubwa ya mapato yake kuwapelekea wananchi maendeleo ya haraka kupitia elimu.

Huku wakionesha kushangazwa na ujenzi wa shule hizo za kisasa walizotembelea juzi, wajumbe hao walisikika wakisema kuwa mfano wa Mbunge Mkono ni wa kuigwa na viongozi wengine hata kama ni wezi wa mali za umma.

Wajumbe hao walisema hatua ya Bw. Mkono kujitolea kujenga shule kama hizo ni moyo wa kuiga, kwani hata kama alizipata bila halali lakini amezileta kwa wananchi badala ya kujali tumbo lake, kwani hata angekula au kuzipeleka nje asingeulizwa.

Naye mjumbe kutoka mkoa wa Kigoma, alimfananisha Mbunge huyo na nabii aliyeshushwa na Mungu kuwatumikia wananchi na kutaka kila kiongozi kuiga mfano huo, badala ya maneno ya majukwaani na wakati mwingine kuchafuana majina bila sababu.

Shule za Sekondari zilitombelewa na wajumbe hao wa NEC ni pamoja na Chifu Ihunyo, Oswald Mang’ombe, Chifu Wanzagi, Buturu na Kiabakari.

Wajumbe hao pia walitembelea eneo ambalo mbunge huyo anatarajia kujenga Chuo Kikuu cha Sayansi, ambacho kitakuwa na jina la kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
 
Is this man our moden day Robin Hoods or just another fisadi?

At least he is doing something good for the poor.
 
Huyu mheshimiwa yupo katika ile orodha ya mafisadi, kwa hiyo na yeye ni mchafu kabisa kama mafisadi wenzake.

Sina cha kujazia zaidi!
 
Jamaa anakwiba na kuwaanzishia miradi watanzania wenzake.
Kwa hili anastahili pongezi hata kama yuko kwenye list ya mafisadi.
 
Mh. Nkono yupo sharp sana katika kutafuta, hali kadhalika kuona ni jinsi gani anawewezesha hao wanaomweka katika system.

Wakati JK alipokuwa anatangaza ajila milioni, wataalamu wa ajila walitegemea kuwa moja ya sehemu ambazo zitaweza kutoa ajila hizo ni kwenye zao la Mkonge. Hadi sasa Tz inatumia asilimia ndogo sana ya zao hilo.

Kwa wale watumiao vinywaji vikali watakua wanajua tekila ni nini. Tekila hutengenezwa kutokana na mkonge. Nkono aliposikia hivyo aliamua kununua mikonge yote kwenye maboma ya huko Mara ili aweze kusafilisha malighafi hiyo ambayo inazidi kupanda soko.
 


Sasa tuelewe kwua Mkono ni fisadi? Mjasiriamali? au mfanyabiashara wenye akili?
 
Sasa tuelewe kwua Mkono ni fisadi? Mjasiriamali? au mfanyabiashara wenye akili?

Mkono ni Fisadi tu! ameshindwa kujisafisha kwenye ile "list of shame". Na hata Gavana Mpya Prof Ndullu ameshtukia hilo amesitisha mkataba wa firm yake (Mkono Advocate) na BoT. Huyu ulindwa wale wenje njaa, naye uwajua sana ni nani mwenye njaa ndani ya serikali na hata taifa!!
 
Mkono sasa ajitetea





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…