Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Mbunge wa Musoma Vijijini Bw. Nimrod Mkono amesema kuwa yuko tayari kumtetea aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu endapo Gavana huyo atafunguliwa mashtaka katika mahakama ya sheria.

Huyu Mzanaki bado haamini kuwa the clock is ticking against him. Ukilewa pesa za wizi huwa unakuwa mpumbavu haswa. Yaani hawa jamaa wan ka-confidence na dharau ya hali ya juu kabisa na kujiona wana right ku-plunder the country and that they can get away with anything in this country for ever.

..Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Gray Mgonja amedai kuwa endapo uchunguzi utafanyika, basi wataonesha kuwa yeye ni safi.

Na kweli ni msafi saana wakati bado analipwa commission pamoja na CD Msuya kuhusina na ujenzi wa Mtera Dam; je kuhusu Japanese Import Support, Alex Stewart, Radar au ni kwenye hilo moja tu ndiyo msafi.

Naye Mwanasheria Mkuu Bw. Mwanyika amesema kuwa anaangalia sheria za nchi ili aweze kuona ni sheria gani zinaweza kutumika katika kufuatilia na hatimaye kuwafikisha wale wanaotuhumiwa ubadhirifu katika Benki Kuu.

Unaona wanavyo anza kujenga hoja za ajabu, eti anaangalia sheria za nchi ili aweze kuona ipi inaweza, the keyword inaweza, meaning inawezekana isiwepo. Je sheria ya uhujumu uchumi mbona bado inatumiwa kuwaswka makarani waodaiwa kuiba maelfu ya shilingi na wala siyo milioni wala bilioni. Kweli kuna cha kuangaliwa uwezekano hapa jamma.

Hapa hafungwi mtu !! Balali katenguliwa uteuzi basi, end of story! Wameanza Kenya na wanaamini kabisa kuwa watanzania hawajifunzi toka kwa majirani zao kuwa kumbe mnaweza kusimama na kupinga ufisadi in the open. Sawa time will tell!
 
ZALENDOHALISI,
nimekusoma mkuu,
Sasa wanajua wazi kwamba tumekua kiakiri,kifikra, kisiasa na hatusahau kilahisi namna hiyo.Tuwashikia hapo hapo mpaka kieleweke na wasidhani watatusahaulisha kwa kujenga Hoja zao hizo za kutaka kupindisha sheria.
 
Askari wa K.A.R anajipanga sawa kwa mashambulizi. Mzee Mkono nasikia wateja wanamkimbia kwa kuhusishwa kwake na ufisadi, naona anachangamkia tenda mapemaaaaa.
 
Askari wa K.A.R anajipanga sawa kwa mashambulizi. Mzee Mkono nasikia wateja wanamkimbia kwa kuhusishwa kwake na ufisadi, naona anachangamkia tenda mapemaaaaa.

Pundit,
Huyu mzee ni fisadi tu kama wenzake na huyo anayetaka mkumtete hana lolote,wezi tu hao.
Na hiyo ya wateja kumkimbia si kweli,WABONGO hatua utamaduni wa namna hiyo,zaidi zaidi watu watataka sifa ya kufanya wanamjua sanaaa.. ili waonekane na mtu maarufu.

La kwa kutaka aonekane msafi ataangaza kwamab wateja wan mkiambia ili watu wamuone msafi.
 
System is broken. That is why Mr. Mkono is strong believed nothing can be done. It is hard to fight against this guy, especial with broken system like the one we had.

I still wait and see what measures will Attorney general takes. To fight with Mkono is not a easy battle.
 
Pundit,
Huyu mzee ni fisadi tu kama wenzake na huyo anayetaka mkumtete hana lolote,wezi tu hao.
Na hiyo ya wateja kumkimbia si kweli,WABONGO hatua utamaduni wa namna hiyo,zaidi zaidi watu watataka sifa ya kufanya wanamjua sanaaa.. ili waonekane na mtu maarufu.
la kwa kutaka aonekane msafi ataangaza kwamab wateja wan mkiambia ili watu wamuone msafi.

Naamini Mr. Mkono ana-deal na wateja wengi wa kimataifa ambao kabla ya kufanya business wanafuatilia rekodi za wanasheria.Hawa ndiyo nawaongelea,
 
System is broken. That is why Mr. Mkono is strong believed nothing can be done. It is hard to fight against this guy, especial with broken system like the one we had.

I still wait and see what measures will Attorney general takes. To fight with Mkono is not a easy battle.

Muungwana alitabiliwa kua akiingia ataivunja na hivyo ndivyo ilivyotokea.
Jamaa alikua na washikaji wengi wa kuwalipa favours na kuna baadhi wan uzalendo halisi hivyo yupo katika kuwalidisha na wao ili wamuuone mwenzao bila ya wale waliokua kwenye system muda mrefu kudhani amewageuka.
Hii ndilo tatizo huyu bwana anakua haeleweki,kwani pia nafsi ina msutaanayajua matatizo ya wannchi kikweli kweli lkn wanao mzunguka sio watu wazuri kwahiyo dhamila yake inakwamishwa.
 
I still wait and see what measures will Attorney general takes. To fight with Mkono is not a easy battle.
He is still reviewing!
just give him more time!
 
hakuna lolote litakaloendelea lets pray wana JF tusiache kumwomba mungu mambo mengi tu yanakuja hasa mwezi february mwanzoni,,,kila mtanznia ataamini kweli mungu yupo....
""MUNGU IBARIKI TANZANIA""
 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Gray Mgonja amedai kuwa endapo uchunguzi utafanyika, basi wataonesha kuwa yeye ni safi.

He! He! He! Ukistaajabu ya Balali, utayaona ya Mgonja!
 
Jamani mimi nahitaji msaada tena mkubwa nieleweshwe. Kuna siku sikusimuliwa nilimwona mwenyewe kwenye tv fisadi mkubwa mgonja akijitapa kwamba yeye ndio MLIPAJI MKUU WA SERIKALI (PAYMASTER GENERAL).Sasa pale ambapo pesa ya kodi ya walalahoi kwa mabilioni inapopotea kupitia malipo ya kifisadi na mlipaji mkuu akasema yeye ni clean hahusiki ni uclean upi anaouzungumzia au ndio ule wa Mr.clean yule wa kiwira na ANBEM?

Hv kwanini tusiandamane maandamano ya amani kushinikiza mramba na huyu mr.clean mwingine feki watoke ofisini? Kuendelea kuwalipa mshahara na kuendelea kutumia mashangingi yetu sio matusi haya jamani kwa maskini wa Tanzania?
 
Huyu Mzee Mkono naona keshaanza kupagawa. Yeye si ni mmoja wa malawyer wa BOT na serikali ya Tanzania(Refer case ya Valambhia, Citi Water). Na I pressume lawyer wa his caliber lazima atakuwa na retainer's arrangement na mashirika kama BOT. Sasa atakapokuwa anamtetea Balali si patakuwa na conflict of interest.

Nafahamu alishafanya hivyo previously kwa Dito, lakini kwa Balali na hizi tuhuma, yeye Mkono ni interested party bearing in mind, he is a shareholder of Bank M ambaye Bwana Jeetu Patel(The most beneficiary of EPA fund) is his co- director/shareholders na hata hiyo leseni ilipatikana wakati wa Balali's era.

I guess sasa is the time to return favours.
 
Mkono is right,

Kazi ya Law Firm yoyote ni exactly hiyo... sio kazi ya Law firm kuangalia mtu atakuwa guilt or not.

so there is no wrong doing for him to help Balali tuache unazi!
 
Jamani mimi naomba nisaidiwe kuna kitu sielewi hapa kuhusian na huyu fisadi mgonja. Kuna siku nilimwona kwa macho yangu kwenye tv akijitapa kwamba yeye ndio MLIPAJI MKUU WA SERIKALI (PAYMASTER GENERAL) Sasa leo kunatokea upotevu wa mabilioni ya walalahoi wa TZ kwa njia ya malipo ya kifisadi anasema yeye yuko clean ni uclean upi huo au ndio ule wa yule mr.clean wa kiwira na ANBEM.

I think tunahitaji kuandama kwa amani kuwashinikiza mramba, meghji na mgonja waachie hizo ofisi kwa kuanzia hatuhitaji hata uchunguzi maana tunayo audit report maana kuendelea kuwalipa mshahara na kutumia mashangingi yetu ni matusi kwa wazt maskini.

Kuna waziri juzi huko asia kajiuzuru kwa kuwa na njumba ndogo sasa wabongo umepoteza mabilioni ya walipa kodi unasimama mbele na kusema u are clean jamanio huu si uchuro?
 
Mkono is right,

Kazi ya Law Firm yoyote ni exactly hiyo... sio kazi ya Law firm kuangalia mtu atakuwa guilt or not.

so there is no wrong doing for him to help Balali tuache unazi!

Kasheshe,

Lakini unasahau kwamba Nkono ni mwanasiasa, kwahiyo ungetegemea asikubali kuwatetea mafisadi. Lakini kwa Tanzania ambako mafisadi wako juu ya sheria, sishangai kusikia alichosema.

Ila angelikuwa huku majuu, na kama ni mbunge na akasema atamtetea fisadi, hiyo kampuni yake ingelikuwa kwenye matatizo makubwa sana.
 
Ni kweli kabisa Mkono hata kama ni Mwanasheria na anahaki ya kumtetea mtu yeyote katika hili alipaswa kufikiri kidogo kabla ya kukurupuka na kuropoka.

Kama mwanasiasa na aliyeingia Bungeni kwa ridhaa ya wananchi Masikini wa Musoma ambao wanapoteza maisha kila siku kutokana na kuibiwa rasilimali zao na haohao mafisadi, atakuwa hajawatendea haki wapiga kura wake na hataeleweka kabisa.

Hata hivyo hapa anatuonyesha jinsi gani alivyo na KIBURI mbele ya Watanzania wenzake waliojaa dhiki na shida.
 
Back
Top Bottom