Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Waungwana,

Kama mtakumbuka katika sakata la kuhusiana na ufisadi wa BoT, Mkono na Mzindakaya walikuwa mstari wa mbele kumtetea aliyekuwa gavana wa BoT, Balalli na kudai kwamba hakukuwa na tuhuma zozote BoT.

Gazeti moja liliandika kwamba Mkono alilipwa mabilioni na BoT, naye alikanusha na kulishinikiza gazeti hilo limuombe msamaha ama atalifungulia mashtaka kortini. Ukweli ukafichuka kwamba Mkono alilipwa bilioni 8 na BoT ambazo mpaka hii leo haijulikani alifanya kazi ipi na kwa muda gani mpaka akastahili kulipwa pesa nyingi kiasi hicho. Baada ta ukweli kufichuka lile tishio alilolitoa Mzindakaya dhidi ya gazeti lilikufa kimya kimya.

Mzindakaya naye ikaja kubainika kwamba alipewa mkopo wa bilioni na BoT pamoja na kuwa bank hiyo haijishughulishi na kutoa mikopo, bali bank zinazofanya hivyo ni bank za biashara.

Itakuwa si vibaya kama uongozi mpya wa BoT ukiongozwa na gavana ukatufahamisha Watanzania kuhusiana na malipo hayo makubwa. Je, Mkono alilipwa mabilioni hayo kwa kazi ipi? Hiyo tenda ya kuommba kazi hiyo ilitangazwa wapi na lini?

Na huo mkopo wa Mzindakaya aliupata kupitia kipengele kipi cha BoT kilichoruhusu apewe mkopo huo? Na ni Watanzania wangapi ambao wamepata mkopo kama huo alioupata Mzindakaya?

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6460
 
Haya JF naona na mkataba nao umekatishwa... Kama tunavyosema... TIK TIK TIK,

The clock is ticking, JF tunazoza, vitu vinajipa....

Kaaz kweli kweli

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4789
Hilo ni Mwananchi la leo!!!

My take:
1. GHARAMA ZA KUKATISHA MKATABA HUO NI KIASI GANI NA NI KWA VIGEZO GANI
2. KUINGIA HAPO HAO MAJAMAA WALIPATAJE INA MAANA HAKUKUWA NA TENDA - Soma maelezo ya Gavana Ndulu
 
mbona sasa hivi ameshapata wa ATC... ningependa kujua ATC wamemretain kwa fee ya kiasi gani...
 
Mawazo chanya kutoka kwenu yote yana ashiria..we need a new rational constitution, thats all!,maana yake kama sheria mama ina mapungufu then what do you expect?

Joseph Mihangwa amekuwa akiandika makala maridhawa juu ya mchakato wa kuibadili latiba yetu, still for those who are favoured by the 'status quo' have been reluctant kufanya mabadiliko ya maana as if nchi hii ni after wao haitakakuwepo tena[mortal].
 
Watanzania tungependa kujua hizo bilioni 8 na ushee alizolipwa Mkono zilikuwa ni kuhusiana na kesi zipi? Na alikuwa analipwa kiasi gani kwa saa? Je, wateja wake wengine anawacharge kiasi hicho hicho au kwa kuwa aliona kuna kisima cha kuchota kilichojaa akaamua aongeze charge per hour ili apate pesa nzuri? Tunasubiri majibu.

Posted Date::3/3/2008
Mkataba wa Mkono BoT wasitishwa

*Ni wa kiutetea mahakamani

*BoT yatangaza zabuni mpya

*Gavana asema wamekubaliana

* Asema wanatafuta unafuu

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

KATIKA haraka zake za kujisafisha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesitisha mkataba kati yake na Kampuni ya Uwakili ya Mkono.

Kufuatia uamuzi huo, BoT mwishoni mwa wiki ilitangaza zabuni ya kutafuta kampuni ya uwakili ambayo itakuwa ikifanya kazi mbalimbali za benki hiyo kwa kushirikiana na wanasheria wake.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu aliithibitishia gazeti hili jijini Dares Salaam kuhusu uamuzi huo wa kutangaza zabuni ya kutafuta kampuni mpya.

Kampuni ya Uwakili ya Mkono inaongozwa na Nimrod Mkono mbunge wa Musoma Vijijini, ambaye amekuwa akiitetea serikali katika kesi ya Valambhia ambaye aliuzia vifaa vya kijeshi.

Hata hivyo, Mkono pia amekuwa akitajwa na wapinzani kwamba amekuwa akilipwa zaidi ya sh 500,000 na BoT kwa sasa moja katika kesi hiyo.

Akizungumzia uamuzi huo, Profesa Ndulu alisema BoT imetangaza zabuni hiyo kutafuta unafuu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alipoulizwa iwapo unafuu huo anaozungumzia unatokana na kuona gharama za Kampuni ya Mkono kuwa kubwa, alijibu: "Si unajua ukitangaza zabuni unakuwa na unafuu, ushindani unasaidia kuleta unafuu."

Alisema kabla ya uamuzi huo pande mbili zilikutana na kukubaliana.

"Ndiyo tumesimamisha mkataba, lengo ni kujipanga upya na vizuri, na hayo ni makubaliano ya pande zote mbili, si uamuzi wetu kwa kuwa mkataba unazihusisha pande zote mbili (BoT na Kampuni ya Uwakili ya Mkono," alisisitiza.

Alisema mara nyingi inapotangazwa zabuni katika mfumo wa ushindani, huchangia punguza gharama za kazi katika mkataba.

Alifafanua kwamba, mkataba uko wazi kwamba upande mmoja unaweza kusimamisha mkataba wakati wowote baada ya kukaa na kukubaliana.

Kuhusu kampuni hiyo kuendelee kuitetea serikali katika rufaa yake dhidi ya Valambhia, alisema pia wamesimamisha.

Aliongeza kuwa kuna taratibu ambazo zimekwishafanyika katika utetezi wa kesi hiyo akasema si sahihi kuzungumzia kwa undani kwani iko mahakamani.

Chini ya uongozi wa gavana Daud Ballali, BoT ilikuwa na taswira ya ufisadi mbele ya Watanzania huku makampuni na watu mbalimbali wakijitoe mamilioni ya shilingi kwa njia mbalimbali.

Uamuzi huo wa BoT chini ya uongozi wa Profesa Ndulu kuisaifisha benki, kuanzia kwa wakurugenzi wake na hatimaye kusimamisha mkataba huo, unaonekana kama pambazuko jipya kuelekea kuitakasa taasisi hiyo nyeti ya umma ambayo imechafuka kwa tuhuma za ufisadi.

Wakati hayo yakiendelea tayari mchakato kurejesha zaidi ya Sh133 bilioni, zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya benki hiyo unaendelea, hadi mwisho mwa wiki iliyopita zilishakusanywa Sh50 bilioni.

Wiki iliyopita vigogo watano wa vitengo mbalimbali vya benki hiyo walisimamishwa kazi katika hatua ya kuhakikisha kuwa benki hiyo inasafishwa.

Sambamba na hilo pia alipangua safu ya Wakurugenzi wa matawi yote nchini isipokuwa Mwanza.
 
Inasemekana Mkono alikuwa analipwa na BOT wastani wa USD 400,000/- kila mwezi, hiyo ni aidha alikwenda Mahakamani au lah! Habari za ndani ya BoT zinasema aliyekuwa anaidhinisha malipo hayo ni Liumba (labda ndio maana kawekwa benchi). Kesi kuu ya malipo hayo ilikuwa ni ya mfanyabiasha wa kihindi aitwaye Valambiah, ambaye anaidai serikali dola milioni 55 kama malipo ya vifaa vya kijeshi alivyo "supply" kwa serikali mwishoni mwa miaka ya 80.

Valambiah alishinda kesi katika Mahakama Kuu katika miaka ya hivi karibuni, BoT wakasema hawawezi kulipa pesa zote hizo kwani watafilisika. Ndipo serikali ikakata rufaa kwenye Mahakama ya rufaa. Rufaa hiyo ndio ukawa mwanya wa baadhi ya watu kujichotea pesa za wavuja jasho.

Huo ni mrija wa kula pesa ya serikali inayotokana na jasho la walipa kodi.
 
wakati wote tunajua kwa Ditopile alishuka kwenye gari lake akaenda kwenye basi na kumuua dereva wa basi, FULL STOP!

In almost every civil and criminal case, the person who fired the gun claims that the weapon "just went off" (i.e. an accidental discharge). Most observers (lawyers, media, police, etc) dismiss these claims with a shrug and a smile; perhaps justifiably saying "well, he would say that, wouldn't he".

Testing should be performed to determine if a given firearm is too easy to discharge, thereby rendering it unsafe. Police laboratories (kama zipo) have no inherent interest in justice, but do have a strong interest in assisting prosecutors to secure convictions.

Prosecutors are employed and funded by Government. Police labs are funded by Government, staffed by government employees (often police). The police are funded and employed by Government and blaza Dito is....... From a defence perspective, there is clearly a conflict of interest here.
 
Inasemekana Mkono alikuwa analipwa na BOT wastani wa USD 400,000/- kila mwezi, hiyo ni aidha alikwenda Mahakamani au lah! Habari za ndani ya BoT zinasema aliyekuwa anaidhinisha malipo hayo ni Liumba (labda ndio maana kawekwa benchi). Kesi kuu ya malipo hayo ilikuwa ni ya mfanyabiasha wa kihindi aitwaye Valambiah, ambaye anaidai serikali dola milioni 55 kama malipo ya vifaa vya kijeshi alivyo "supply" kwa serikali mwishoni mwa miaka ya 80.

Valambiah alishinda kesi katika Mahakama Kuu katika miaka ya hivi karibuni, BoT wakasema hawawezi kulipa pesa zote hizo kwani watafilisika. Ndipo serikali ikakata rufaa kwenye Mahakama ya rufaa. Rufaa hiyo ndio ukawa mwanya wa baadhi ya watu kujichotea pesa za wavuja jasho.

Huo ni mrija wa kula pesa ya serikali inayotokana na jasho la walipa kodi.

Duu?? ama kweli
Ukistaajabu ya Musa....

Sasa kama Mkono alikuwa analamba dola laki 4 kwa mwezi manake kwa hesabu za haraka haraka ni miaka 11 inatosha kupata hela yote anyo dai huyo Valambiah, swali la kujiuliza kesi imedumu muda gani? je walikuwa na uhakika wa
1) Kushinda kesi?
2)kesi kuisha kabla ya miaka 11? kiasi kwamba kuendesha hiyo kesi garama yake ingekuwa ndogo kulingana na kiasi kinachodaiwa?

Ama basi tu ni ile kwamba fedha za walipa kodi wa Tanzania hazina mwenyewe ni kwa ajili ya wajanja wachache kujichotea watakavyo??

Je mtu aliye ingia mkataba wa nmana hii bila kuangalia no 1 na na 2 hapo juu hausiki kwa njia moja ama nyingine kuhujumu uchumi? sheria zetu zinasemaje juu ya hili??

I guess segerea/Keko could be the right place kwa fisadi hawa!
 
Mkono,mkono,rudisha fedha zetu. Gazeti moja liliwahi kuripoti kuhusu kulipwa kwa kampuni hii visivyohalali na BOT.

Mkono akaja juu sana na akaitisha mkutano pale habari/maelezo na akalitaka gazeti hilo kumwaomba radhi kabla ajalifungulia mashtaka. Baadaye akaona itakuwa balaa akatulia.

Huko kwao Musoma,mkono ni kama kamungu kadogo, kumbe naye ni fisadi. Imakwisha rudisha ngapi?
 
..huenda zabuni akashinda Dr.Mwakyembe kama njia ya kumnyamazisha.
 
..huenda Dr.Mwakyembe atashinda hii zabuni ya kuitetea BOT.

..ninavyoelewa mimi gharama za wakili zinaongezeka kulingana na kiwango cha madai ktk kesi/shauri.

..sasa gavana anatafuta unafuu kutoka wapi? waandishi wa habari hawaulizi maswali ya msingi.

NB:

Dr.Ndullu alikuwa board member wa BOT miaka ya 1990. kuna fedha zilipotea miaka ile. Watanzania tulipaswa kuhoji kama yuko credible enough kuchunguza hizi fedha zilizopotea wakati wa Balali.
 
Hili suala Ndullu kuwa miongoni mwa wezi wa BoT limeulizwa sana hapa JF na inaonekana waaandishi wa habari nyumbani wanachukua muda kidogo kuanza kumpa kibano huyu Ndullu ili aseme kuwa alihusika vipi katika wizi huu, na kama hakuhusika alifanyani kuuzuia
 
Masaki,
Vallambia alishalipwa fedha zake millioni 55. Lakini hapo katikati mfanyibiashara mjanja Nolan akakimbia nazo Ulaya. Yeye alitapeliwa na mwenzake na akarudi kudai tena serikali. Ndiyo maana benki ilikataa kumlipa hata baada ya kushinda mahakamani.
 
Mkono,mkono,rudisha fedha zetu. Gazeti moja liliwahi kuripoti kuhusu kulipwa kwa kampuni hii visivyohalali na BOT.Mkono akaja juu sana na akaitisha mkutano pale habari/maelezo na akalitaka gazeti hilo kumwaomba radhi kabla ajalifungulia mashtaka. Baadaye akaona itakuwa balaa akatulia. Huko kwao Musoma,mkono ni kama kamungu kadogo,kumbe naye ni fisadi. Imakwisha rudisha ngapi?

Huyu naye ni fisadi. Tumkabe koo mpaka arudishe pesa zetu ambazo hakustahili kulipwa.
 
Mkono,mkono,rudisha fedha zetu. Gazeti moja liliwahi kuripoti kuhusu kulipwa kwa kampuni hii visivyohalali na BOT.Mkono akaja juu sana na akaitisha mkutano pale habari/maelezo na akalitaka gazeti hilo kumwaomba radhi kabla ajalifungulia mashtaka. Baadaye akaona itakuwa balaa akatulia. Huko kwao Musoma,mkono ni kama kamungu kadogo,kumbe naye ni fisadi. Imakwisha rudisha ngapi?
Mkono ni Mbunge wa Musoma vijijini lakini yeye anadai mkoa mzima hakuna Mbunge wa maana ni yeye tu .So anajiita Mbunge wa Mkoa .Lakini u mungu zaidi ni maeneo yake ya Musoma vijinini huko majita , zanaki, Makutano ya juu,Butiana, maeneo ya Magorombe, Busegwe nk
 
Inasemekana Mkono alikuwa analipwa na BOT wastani wa USD 400,000/- kila mwezi, hiyo ni aidha alikwenda Mahakamani au lah! Habari za ndani ya BoT zinasema aliyekuwa anaidhinisha malipo hayo ni Liumba (labda ndio maana kawekwa benchi). Kesi kuu ya malipo hayo ilikuwa ni ya mfanyabiasha wa kihindi aitwaye Valambiah, ambaye anaidai serikali dola milioni 55 kama malipo ya vifaa vya kijeshi alivyo "supply" kwa serikali mwishoni mwa miaka ya 80.

Valambiah alishinda kesi katika Mahakama Kuu katika miaka ya hivi karibuni, BoT wakasema hawawezi kulipa pesa zote hizo kwani watafilisika. Ndipo serikali ikakata rufaa kwenye Mahakama ya rufaa. Rufaa hiyo ndio ukawa mwanya wa baadhi ya watu kujichotea pesa za wavuja jasho.

Huo ni mrija wa kula pesa ya serikali inayotokana na jasho la walipa kodi.

Je Wateja wake wengine anawacharge pia hata kama haendi mahakamani au kwa kuwa aliona kuna kisima akaamua kuwa na uroho wa kujitajirisha haraka kupitia migongo ya walipa kodi? Hayo malipo ya dola zote hizo kwa mwezi yalifikiwaje?
 
Masaki,
Vallambia alishalipwa fedha zake millioni 55. Lakini hapo katikati mfanyibiashara mjanja Nolan akakimbia nazo Ulaya. Yeye alitapeliwa na mwenzake na akarudi kudai tena serikali. Ndiyo maana benki ilikataa kumlipa hata baada ya kushinda mahakamani.

Hey! kumbe zilishalipwa? ama kweli BOT limekuwa kapu la mjinga...
 
Masaki,
Vallambia alishalipwa fedha zake millioni 55. Lakini hapo katikati mfanyibiashara mjanja Nolan akakimbia nazo Ulaya. Yeye alitapeliwa na mwenzake na akarudi kudai tena serikali. Ndiyo maana benki ilikataa kumlipa hata baada ya kushinda mahakamani.

Deni la Valambiah linakua kila siku,
hii tulushaijadili hapa The Inside Story

Tanzania Ordered to Pay Military Supplier $72 million
By FAUSTINE RWAMBALI
THE EASTAFRICAN

THE HIGH Court of Tanzania has ordered the Bank of Tanzania (BoT) to pay $72,234,821 to a Dar es Salaam businessman, Mr Devram Valambhia, for the supply of 830 military vehicles and equipment in the 1980s.

The contract to deliver the military equipment was between the government and an Irish registered firm, Transport Equipment Ltd, whose chief executive officer was Mr Reginald John Nolan, and the Tanzania businessman, Mr Valambhia.

The High Court ordered the government to pay the outstanding debt of $57,366,110 in 1991, but the then Minister of Finance, the late Ali Kighoma Malima, disregarded the order.

The court observed that Mr Nolan had come into the contract as chief executive officer of Transport Equipment Ltd and that any payment was supposed to be paid to TEL rather than to Mr Nolan in person, as Minister Malima had instructed. Mr Valambhia was TEL's local partner who held 45 per cent shares in the contract deal, while TEL held 55 per cent shares.

The order arises from a February 12, 1991 ruling in which Mr Valambhia was awarded $57,366,110 plus interest on the contract sum.

The ruling stated: "Pursuant to a contract between the Government of Tanzania and Mr Valambhia, dated April 25,1985, and that the government acting through the Ministry of Defence and National Service, and through the Bank of Tanzania, shall pay the proceeds as at June 10, 1989 together with interest, arrears, management fees direct to the defendant (Valambhia)."

However, BoT has since appealed against the ruling, with its counsel, Mr Bosco Kimela, questioning the legality of the order "as it was not served as per laid down legal requirements and that government property was not the subject of attachment because the BoT is the government's banker."

Its counsel said: "The applicants (BoT) are the government's bankers by law. They are required to administer the government's payment agreement ... but they can only do so upon instruction by the government and upon the existence of budgetary directions that enable the applicant to effectuate payments." The appeal comes up for ruling on September 21.

According to facts of the suit, TEL entered into an agreement with the government of Tanzania to supply military equipment on April 25, 1985. The equipment included 830 military vehicles between 1986 and 1987 and no down payment was made in respect of the contract price, which was Tsh42.2 billion ($46,915,170).

Mr Valambhia worked together with Mr Nolan, and BoT then paid some $3,250,000.

Mr Valambhia was entitled to a 45 per cent share of the payment, but later, Mr Nolan tried to impeach the agreement document.

A counter affidavit filed by Maira and Company Advocates for Mr Valambhia, says that the February 12, 1989 decree, which is the subject of the proceedings, has never been set aside by any revision or appeal by any higher court in Tanzania

"The obligation of the BoT to administer and make payments such as the one between TEL and the government of Tanzania is statutory and arises from Sec.54 of the BoT Act No. 1 of 1995 which is in force and the contention that BoT does not operate any government account for purposes of payments due to judgment debtor is without any basis or merit," the affidavit says.

"The government of Tanzania as we have stated ... has been very antagonistic to the decree holder and has formed an unholy alliance with the chief executive of the judgment debtor, Mr Nolan," Maira claims.

Maira cites the example of a $2 million payment to Tannol Holdings Ltd, a company not party to the agreement, when the matter was sub judice. Tannol Holdings Ltd belongs to Mr Nolan.

The affidavit further prays that the "conduct of the government of Tanzania, in particular the office of the Attorney General's Chambers and the Treasury, during this litigation and after attracts no sympathy from this honourable court."

And in the rejoinder affidavit to the reply to the counter-affidavit filed on August 9, Maira states: "A document entitled 'Instrument' executed by the former Minister for Finance, the late Kighoma Malima, on July 29, 1993, the government agreed to pay money directly to Reginald John Nolan instead of TEL as a company."

The 'instrument' states: "I, Kighoma Ali Malima, Minister for Finance of the Government of Tanzania, in exercise of powers conferred upon me under Section 20 of the Government's Loans, Guarantees and Grants Act No 30 of 1974, do hereby appoint Mr Frank Kejo, Principal Secretary to the Ministry of Defence and National Service of Tanzania to execute on my behalf, Addendum No.1 to the contract of April 24, 1985 between Transport Equipment Ltd of Dublin, Ireland, and Tanzania, which seeks to provide for full and final settlement of the outstanding claims of M/S Transport Equipment Ltd against the government of the United Republic of Tanzania."
 
Back
Top Bottom