Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Hii Tanzania naona wanakula wenye meno na huku usalama wa taifa wakihangaika kujua nani anapost hapa JF! Huyu mkono ndiyo anatishia usalama wa taifa na ndiye angefaa achunguzwe na wala sio wana JF! grrrrrrrrrrrrrr
 
Hiyo credibility ya Mkono na kampuni yake tuliisha e-question hapa, huyu alitakiwa kuchunguzwa na Bunge na kufukuzwa muda mrefu sana. Wabunge MAFISADI kama huyu hawatatutatulia matatizo tuliyonayo.

Natumaini anayehusika atachukua hatua madhubuti bila kuchelewa kuona kwamba taifa halipotezi pesa ya walipa kodi kwa ujanja ujanja. Na vile vile aache kukomalia vimwana kama Zuma kwani taifa liko taabani.
 
WanaJF wenzangu, utani kidogo kama Issa Michuzi alivyotuwekea kule kwake (copmliments to him and KP)

Naendelea kucheka manake KP ame "sum up" haya tunayoyaongea kwenye picha mbili tu...............

michkp.jpg

Kaaz kweli kweli!!!
 
Masaki,
Vallambia alishalipwa fedha zake millioni 55. Lakini hapo katikati mfanyibiashara mjanja Nolan akakimbia nazo Ulaya. Yeye alitapeliwa na mwenzake na akarudi kudai tena serikali. Ndiyo maana benki ilikataa kumlipa hata baada ya kushinda mahakamani.

Huyu Nolan mbona kachoka sana! huwa anaonekana sana Moevenpic.NA Vallambia si alifariki jamani,au nachanganya na mtu mwingine?
 
Wana JF kuna IMMMA Advocates mnaonaje wakiichukua tenda? tik tak tik tak…
 
ninachohisi kwenye swala la mkono kulikuwa na ufisadi, kwani alikuwa ameshalipwa around 18bn ambazo ni kama 13% ya deni inalodaiwa serikali, kwa kawaida advocate fees ni 10% of the deni, na kama deni linalodaiwa ni kubwa mna negottiate hata 5%, sasa huyu amelipwa 13% why?
 
WanaJF wenzangu, utani kidogo kama Issa Michuzi alivyotuwekea kule kwake (copmliments to him and KP)

Naendelea kucheka manake KP ame "sum up" haya tunayoyaongea kwenye picha mbili tu...............

Kaaz kweli kweli!!!

rlys7k.jpg

Morani75, hii summary ni kiboko... hamna kilichoachwa nje!!
 
Kuna habari ambzo hazipingiki kwamba kuna vita kali kati ya makampuni wawili ya sheria tajwa. Inasemekana kampuni ya Mheshimiwa Mkono ina vita kali na IMMMA kwa sababu imefanya fitna mpaka ikaondolewa kwenye tender ya BOT. Pia inasemekana kwamba kwa mvuto mkubwa iliyo nayo kwa sasa (IMMMA) ina mpango wa kupewa nafasi iliyokuwa ikishikwa na Mokono.

Hali hiyo umepelekea Mkono kuapa kuwa atakufa na mtu! Yaani yuko tayari tenda hiyo aperwe mwingine lakini lakini sio fisadi Masha. Hali ni tete zaidi kwani Mvuto wa Masha kwa serikali kwa sas ni kubwa zaidi ya Mkono kwa serikali ya awamu hii ikizingatiwa na nafasi aliyo nayo. Vita hii imepelekea kuibuliwa kwa madhambi ambayo ambayo haiyumkini tukashuhudia mengi zaidi siku za karibuni hasa ukizingatia kwamba wanajuana vizuri.

Mkono na IMMMA Wote wana uzoefu wa kutosha na zile account zinazomwaga fedha kwenye benk kubwa ya nchi.

Tusubiri tuone vita ya panzi, sie yetu macho!!!
 
Malindi, unapaswa kuelewa kuwa waungwana hapa hawataki blah blah. Hii habari ni nyeti kweli kweli lakini haina nyama za kutosha kuwafanya watu waamini moja kwa moja.

Ni kweli vita vya panzi ni furaha kwa kunguru na kama ni kweli yanatokea hayo tutafaidi mambo.

Lakini inaelekea unajua mengi zaidi ya haya uliyoeleza. Ubu mwaga mavituuuuuz zaidi.
 
Mwaka huu tutajua mengi sana hata yale yaliyo nyuma ya pazia!
 
Mpita njia, wewe mwenyewe unafahamu kuwa Bi Karume ni mmoja wa wana IMMMA kwa sasa. Waliazimia kuchota fedha za kidume mzoefu, hatua ya kwanza ni kumchomoa kwenye mrija.

Wamefanikiwa lakini wao kutia mdomo imekuwa shida kwani aliyechomolewa hakubali. Kwa kifupi ni hivyo, ya zaidi tusubirie.
 
Mpita njia, wewe mwenyewe unafahamu kuwa Bi Karume ni mmoja wa wana IMMMA kwa sasa. Waliazimia kuchota fedha za kidume mzoefu, hatua ya kwanza ni kumchomoa kwenye mrija... Wamefanikiwa lakini wao kutia mdomo imekuwa shida kwani aliyechomolewa hakubali. Kwa kifupi ni hivyo, ya zaidi tusubirie.

Usitunyuime uhondo mwanaume.... umeshaanza, hakuna haja ya kusubiri.. taja, taja, taja, taja
 
"vita vya panzi ni furaha kwa kunguru" i like this quote..

Ulaji kwa wale wanasheria wadogo waliobaniwa kwa miaka mingi!! LOL..Sasa tusubiri tuone nani atapewa hii tenda..ningependa kwa kweli kuona smaller firms kujitokeza..swali je wanaexperience na expertise to handle such?? But then again in the Tanzanian system who needs expertise and experience...tutajifunza kazi tukishapewa..(Naona nimejijibu)
 
Oh! Analipwa kama kawaida. Ila kwenye taarifa ya leo kutoka kwenye kampuni hiyo kuhusu makala za Mwanahalisi wanasema amechukua likizo ya 'kisiasa'! ila yeye ni bado mmoja wa wamiliki na wenye hisa.
 
Oh! Analipwa kama kawaida. Ila kwenye taarifa ya leo kutoka kwenye kampuni hiyo kuhusu makala za Mwanahalisi wanasema amechukua likizo ya 'kisiasa'! ila yeye ni bado mmoja wa wamiliki na wenye hisa.

kwa hiyo bado anavuna matunda ya Tangold na Deep Green siyo? Hivi alikuwa hapa IMMMA wakati madili hayo yanaingiwa?
 
kwa hiyo bado anavuna matunda ya Tangold na Deep Green siyo? Hivi alikuwa hapa IMMMA wakati madili hayo yanaingiwa?

Mkuu MKJ,

umewahi kuamini katika bahati nasibu/mbaya/coincidence maishani?Huyu bwana aliyepost thread hii naamini ana mengi sana ambayo anasita kuyamwaga.Lakini hata hivyo hoja yake inaleta mwangaza fulani na mwenye macho anaweza kuona nini kilicho mbele

1. Kikwete kaingia madarakani tunaanza kusikia deals chafu za Mkono na BoT.

2. Ridhiwani KIKWETE anakwenda IMMMA licha ya g.p.a yake ya bata kinyume na utaratibu wa IMMMA kuajiri hata kuadmit interns (sina taarifa kama walbadili utaratibu huu).

3.Mujulizi anakuwa Jaji katika mahakama kuu.

4.Fatma KARUME anaingia IMMMA.

5.Balali anatimuliwa,Ndulu anaingia na kusitisha mkataba wa Mkono-BoT. Ikumbukwe kuwa IMMMA wanaguswa na skandali ya

6. Mkono ghafla naye anapiga u-turn na kuanza kurusha makombora BoT kuhusu Tangold/Meremeta baada ya mkataba kusitishwa

Dose this make any sense to you?Je unaweza kuunganisha na anachokisema huyu bwana kuhusu hii vita ya Mkono-IMMMA?

Only time will tell.
 
Ndio maana wanapotutaka tukubali tu ati kwa vile tumewachagua wanakuwa wamekosea; kuna mchezo unapangwa na tusipoangalia tunaweza kujikuta tunafungwa magoli mengine ya kuotea na tukabakia kushangalia..
 
Malindi, unapaswa kuelewa kuwa waungwana hapa hawataki blah blah. Hii habari ni nyeti kweli kweli lakini haina nyama za kutosha kuwafanya watu waamini moja kwa moja.
Ni kweli vita vya panzi ni furaha kwa kunguru na kama ni kweli yanatokea hayo tutafaidi mambo.
Lakini inaelekea unajua mengi zaidi ya haya uliyoeleza. Ubu mwaga mavituuuuuz zaidi.

Jambo hili limekuwa likinichefua kila siku hapa JF, mara nyingi members, haswa senior members kushuka chini, walikileta habari hapa kuna mtu ataitilia walakini, watakuwa doubted and questioned- hii ina discourage watu kumwaga vitu hapa, hata kama member kasikia issue fulani kwa juu juu tu anachopaswa kufanya ni kuianzisha tu akiileta hapa na kutatokea mtu mwenye data zaidi na hivyo vidogo vidogo tunavyojua as individuals vinaishia kutoa habari kamili.

Tukumbuke kwamba wengi wetu hapa uandishi wa habari sio profession yetu na wala hili sio gazeti so its unfair to expect 'habari kamili' kila mara. Hebu fikiria hii habari kama ingeletwa na Senior Expert flani hapa jinsi ambavyo watu wangemmwagia 'thanks'.
 
Back
Top Bottom