Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninashangaa saana na utetezi alioutoa Mheshimiwa Mkono ...Tanzania ni nchi changa Mheshimiwa Mkono kama unataka kulipwa Dolar 600 kwa saa fungua ofisi yako Uingereza au America kama utapata hata kesi moja kusimamia wewe umesajilia Tanzania unalipwa kama mtanzania anavyolipwa, labda ufanye ujanja kama uliofanya.Huo ni wizi.
Kama ni nchi changa mbona tuna hela ya kulipa mtu $500 kwa saa? Tatizo sio Mkono, ni yule aliye mlipa. Binadamu wa kawaida akipewa tenda anaweza kusema hapana ndugu umenizidishia?
Huyu ni fisadi tuu na DR.SLAA alisema zamani tangia september 15 2007 ,sasa mbona hakujitokeza kujibu anakuja kujibu leo eti kuna watu wanatumia CAG ofisi kumdhoofisha kisiasa.
Huyu ni fisadi tuu tena la kimataifa ,na hapo bado atakuja kutueleza na wabia wenzake wa benki M wametoa wapi mitaji kama si kugawana hizo hizo za BOT.
kama CCM inataka kupona isiendelee kupokea pesa za hawa mafisadi hadi watakapokuwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya dola.
Hakuna jiwe ambalo litasalia juu ya jiwe kuhusiana na mafisadi wetui na haswa wale 11 wa awamu ya kwanza.
m,apambano yanaendelea mpka kieleweke......
...ilishatolewa hoja huko nyuma kwamba kwa utaratibu wa fedha za Serikali, mdai anapeleka hati ya madai (Invoive) kwanza. Hivyo Mkono anahusika kwa kudai kiwango kikubwa na Maafisa wa BOT wanakosa la kulipa kiwango hicho cha juu.
Pia ni vema kujenga tabia ya kusema hapana ndugu umenizidishia!...
Nziku;
Nimesoma hoja zote za huko nyuma. Hapa kulikuwa na tenda halafu mkataba. Tusitake kusema kwamba Serikali ilipokea huduma kwa mtu bila kujua gharama kabla ya kutumiwa invoice. Kiasi cha $500 Serikali ilikuwa inakijua kabla Mkono hajaanza kazi. Sasa niambie Mkono kosa lake nini?
Na katika ile taarifa ya wakaguzi ni kwamba pesa zilizolipwa zilikuwa nyingi kuliko zilizolipwa mwaka. Hawajasema ni nyingi kuliko makubaliano au kuliko mawakili wengine wanavyo chaji. Isitoshe kulikuwa na tenda. Na hata jana wakaguzi wameongea tena, wakasema hawajadai kwamba Mkono ni corrupt. Wametoa uchambuzi wa hesabu tu. Na Mkono hawezi kusema ndugu mmenizidishia kwa sababu yeye ndie alipeleka tenda.
Taarifa ipi hiyo unayoiongelea hapa mkuu?
Mwambie aende zake akalale huyo. Aturudishie pesa zetu kwanza halafu ndiyo akainvest!!