Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nilikuwa najiuliza binti yake Milembe amenunua condominium pale South Beach, FL na ame i-renovate kiasi kile kwa kazi gani anayoifanya yule demu? Now I know, papa Nimrod does't come cheap. Kalagabaho!
 
Lakini Benki Kuu kumlipa kiasi hicho siwezi kushangaa.. hasa wakili ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa Gavana? QUOTE]

Good Mwanakijiji,

Hapo ndo ulipo msingi mkubwa wa malipo hayo ya kufuru!

Halipwi pesa yote hiyo kwa ajili ya uwakili bali kwa vile ni mtetezi wa gavana!!
 
Hivi kwanini wachawi wa nchi nzima wasiungane na kuwaroga MAFISADI kama hiri RI MKONO...anakera kweli
 
Hivi kwanini wachawi wa nchi nzima wasiungane na kuwaroga MAFISADI kama hiri RI MKONO...anakera kweli

Kwi kwi kwi....................... kuna Polonium 210 unaweza kuipata kutoka Russia.
 
Utata wa Mkono kukunjiwa MKONO mkubwa ni refu sana, mimi minafikiri kwamba yeyote anayetaka kulijua hilo hana wajibu wa kujiuliza maswali kadhaa, Je Mkono katokea mkoa gani-"Musoma" je alisoma na nani? wapi? je ana undugu au alikuwa family friend na marehemu baba wa Taifa? je aliwahi kuwa mfanyakazi wa serikali? wizara gani? aliiajiriwa kama nani na kwa muda gani? Je aliacha kazi au alifukuzwa au alijiuzulu?

Je, wakati BOT inaungua moto yeye alikuwa wapi na akifanya kazi gani?je indirectly hakuwa na uhusiano wa karibu na BOT? je kesi ngapi amewahi kuzisimamia huko nyuma kabla ya BOT V/S Vallambhia? Jamani Mkono ni kapu la mjanja mjinga hatii mkono
😕
 
Kubwa zaz\idi na la kujiuliza ni kuwa huyu Mkono amesema kuwa kila wakili analipwa dola 500 kwa saa , na hapo ukisoma vizuri utaona kuwa hapa sipo kila kampuni bali ni kila wakili as an individual, je-kuna usawa hapo kweli, na je huwa wanalipa kodi kama individuals ama kama kampuni na kiasi gani huwa wanalipa.

Kumbe watu wanamwona mtu tajiri kumbe mwizi mkubwa huyu, anasema kuwa yeye sio mkurugenzi wa makampuni yaliyotajwa ila hakumbuki kuwa hata kampuni la mkono n advocates nalo limetajwa naye ndoio mkurugenzi wake ,

hii inaonyesha jinsi ambavyo wameshikwa pabaya na Dr,. Slaa. anasema eti hawezi kwenda mahakamani kwani slaa hana uwezo wa kumlipa , kumbe kuchafuliwa jina kama alivyotutaka tuamini huwa inaangalia ni nani aliyelichafua hilo jina.

Tuamke wakat huu kwani hawa jamaa sasa wanakosa pa kuanzia .
 
nimeshtuka sana pale baada ya kuambiwa kuwa mkono ni maarufu sana kiasi kwamba anaweza kulipwa hela yote hiyo kama advocate wakati maadvocate wengine wakidhalauliwa kuwa they are very cheap. nijuavyo mimi ni kuwa taasisi za serikali huwa zina wanasheria wake wakuzitetea pale ambapo taasisi inakuwa na kesi ya kujibu au kushtaki

pili kama kesi ni ya jinai, ni DPP ndiye ankuwa responsible na huyu ankuwa paid per month, kwa sababu ni employee. hata hivyo kuna akina state attorneys na Attorney generals, wao wako kwa niaba ya serikali na wote wanalipwa permanently.

ila kesi ikionekana imekaa vibaya ndipo unapoita wakili kusaidiana na hawa watu ila sio kwa kiasi cha kutisha kama hivi hapa.

sasa uoga wangu ni kwamba yawezekana ni mpango wa muda mrefu wa kutaka kutuibia ela yetu. na inavyoonekana hawa wote ni kitu kimoja......ila tafadhali atakayeona cv ya huyu bwana ninaomba maana nimeitafuta kwenye mtandao bila mafanikio ili tuone ni sehemu gani ya ziada alipata mafunzo yake ya uwakili, ambapo anatokea kuwa expensive.
 
Specialisation: Hon. Nimrod Mkono is the founder and Managing Partner of Mkono & Co, which he has headed since 1977.
The name Nimrod Mkono has come to be the mark of competence and efficiency in relation to legal work in Tanzania. His specialisations include company law, corporate finance, privatisation and corporate taxation. Hon. Mkono has handled numerous consortium arrangements and has been responsible for advising on a number of high profile acquisitions including the unbundling of and eventual privatisation of the National Bank of Commerce and the privatisation of Tanzania Telecommunications Company Limited, as well as acting for both the government and major corporations in international commercial litigation and arbitration.

Career:

Managing Partner, Mkono & Co since 1977
Member of Parliament, United Republic of Tanzania
Trustee, The Mwalimu Nyerere Foundation since 1996
Advocate, High Court of Zanzibar since 1993
Company secretary and legal advisor to Tanzania Development Finance Company Limited (TDFL), 1978 – 1981
Advocate, High Court of Tanzania since 1977
Resident Magistrate, Civil and Criminal Jurisdiction.

Qualifications:

Fellow, Institute of Chartered Secretaries & Administrators, F.C.I.S., UK, 1986
Associate, Institute of Chartered Secretaries & Administrators, A.C.I.S., UK, 1976
MA (Bus. Law), Council for National Academic Awards, City of London Polytechnic , UK, 1976
Chartered Secretaryship Final Examination (C.I.S.), South West London College, UK, 1975
LL.B, University of East Africa, University College of Dar es Salaam, Tanzania, 1970.
Languages:
English, Swahili.


Mkono Soma hapa
 
...hivi kazi ya Attorney general wetu na jeshi chungu nzima la mawakili wa serikali tunaowalipa mamilioni kila mwezi nafikiri ndio wenye jukumu hapa la kutetea Serikali ila sijui nini kinaendelea,wanasheria tusaidieni hapa kama kuna sheria ya kutumia mawakili binafsi kwenye kesi za serikali kama hizi,na malipo ya dola kwa local firm ni illegal na hairuhusiwi kisheria.

kwa haraka haraka tuu hapa wananchi tuna legit case against hawa wezi wanavyokula pesa zetu lakini tuliowakabidhi watusimamie kina takururu aka PCCB na kamati zetu za bunge ni hooooi kabisa imejaa vilaza na wala rushwa, itabidi katiba mpya iruhusu private lawsuits kwa mafisadi wa mali zetu
 
Kama Mono analipwa $1,000 kwa saa (na kila mteja?) basi maadam BoT wamemlipa $8 mil. (and counting), ina maana ameshawafanyia kazi ya masaa 8,000. Kama mtu unafanya kazi masaa 8 kwa siku, basi ina maana ameshawafanyia kazi kwa miaka 2.73, kwa masaa 8 kila siku, bila kupumzika!

Mkono ni mwansheria. Bila shaka alijua kuna sheria inaweka kikomo cha malipo ya cha 3% ya madai, kama madai yanazidi shilingi milioni 10. Ameshirikiana na BoT kuvunja hiyo sheria. Tueleweje Legislator ambaye ni wa fani ya sheria anapovunja, kwa makusudi, sheria za nchi?

Mkono anaogopa kwenda Mahakamani kwani amevunja sheria kuhusu kikomo cha malipo kwa mwanasheria.

So, you don't "come cheap"? But you have cheapened yourself badly in the eyes of Tanzanians. They now count you among ordinary thieves!

Namuunga mkono Kinepinepi kwamba wanachoweza kufanya wananchi kwa kipindi hiki ambacho CCM bado iko madarakani ni kuwazoemea viongozi wezi kila wanapojitokeza kutaka kusema hadharani.
 
Attorney general anaweza kuamru kutumika kwa wakiri fulani wa kujitegemea, pia hata DPP anaweza kufanya hivyo, na pale tunaita, to hold belief of the attorney general, lakini sio kwa kiasi hicho cha kutumia mawakili tu. kawaida kinachofanyika ni kusaidiana na kushauriana.

Ila hapa inaonekana kesi yote iko mikononi mwa advocates wa kujitegemea. je... akicorrupt na the other side si serikali itapoteza. maana ela ya advocate ipo pale pale hata client akishinda au kushindwa
 
Kutoka Tanzania Daima

Maira sasa ataka kumshitaki Mkono



na Irene Mark



WAKILI maarufu nchini, Moses Maira, amesema leo anatarajia kufungua kesi ya madai dhidi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), akimdai sh bilioni 10 kwa kumkashifu.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti juzi na jana, Maira alieleza kusikitishwa na madai aliyoyatoa Mkono mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi yake, wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomhusisha na ufujaji wa fedha za umma kupitia kampuni yake ya uwakili ya Mkono Company & Advocates.

Mkono katika mkutano aliouitisha na waandishi wa habari aliwalaumu Maira na Mabere Marando, akiwataja kuwa ni mawakili waliokuwa wakimwonea wivu kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kesi ya Benki Kuu kwa upande mmoja na mfanyabiashara Devram Valambhia na Kampuni ya usafirishaji ya Equipment.

Maira alilieleza gazeti hili kwamba, alikuwa amefedheheshwa na maneno hayo ya Mkono aliyoyaelezea kuwa yasiyo na maana kutokana na ukweli kwamba, yeye na mwenzake Marando, hawajapata kushindwa hata mara moja katika kesi hiyo.

Aidha, Maira, mmoja wa mawakili waliojijengea majina hapa nchini, alimtaka Mkono kubeba mzigo wa tuhuma zake na kuacha kujaribu kuwabebesha yeye na Marando shutuma zisizo na chembe ya ukweli.

“Kesho nitafungua kesi Mahakama Kuu kuiomba mahakama imuamuru Mkono anilipe sh bilioni 10 kama fidia kutokana na kunikashifu bila sababu. Siwezi kumwonea wivu, heshima na hadhi yangu ipo juu… naamini inamzidi Mkono.

“Kozi moja niliyoisoma mimi kwa miezi 18, yeye ameisoma kwa miaka mitano, halafu mtu huyo huyo aseme eti mimi ninamuonea wivu, nimuonee wivu kwa kitu gani?” alihoji Maira.

Wakili huyo alisema, yeye na Marando walikuwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kuitisha mkutano wa waandishi wa habari leo kuzungumzia suala hilo baada ya jitihada zao za kutaka waufanye jana kushindikana.

Hivi karibuni, Mkono alikiri kwamba amekuwa akipokea dola 500 za Marekani (karibu sh 650,000) kwa saa, kutokana na kazi yake ya uwakili katika kesi hiyo na kumtaja Wakili Maira na Marando, kuwa watu wanaomtumia Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na kumhusisha kwenye kashfa za ubadhirifu.

Mkono alisema Maira na Marando walishindwa kuendelea na kesi hiyo, hali inayosababisha chuki na wivu kwake, kutokana na malipo anayopata katika kesi hiyo, ambayo hata hivyo hakusema mwendelezo wake.

Marando alikanusha tuhuma zilizotolewa na Mkono siku ile ile na kama alivyodai Maira naye alisema walikuwa hawajapata kushindwa katika shauri hilo ambalo Mkono amekuwa ni wakili wa BoT na Mwanasheria Mkuu.

Marando alisema wakati wanaisimamia kesi hiyo (yeye na Maira) waliishinda serikali baada ya Gavana wa BoT kukutwa na hatia na kupewa hukumu ya kifungo au kulipa faini, na aliokoka kwenda jela baada ya kulipa faini ya sh 400,000 mbele ya Jaji Massati.

“Sioni sababu ya Mkono kulipwa mamilioni ya fedha kila mwezi kutoka serikalini wakati kesi ilishamalizika,” alisema Marando akiielezea kesi hiyo iliyodumu kwa takriban miaka 20 sasa.

Majibizano hayo yanaendelea wakati taifa likiwa katika hali tete, tangu Slaa akisaidiwa na wakili mwingine maarufu jijini Dar es Salaam, Tundu Lissu, watoe orodha ya viongozi 11 ambao waliwataja kuwa wanaohusika katika ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za serikali.
 
*Yeye, wenzake wasema wameshinda, wanaisubiri Bodi
Na Mwandishi Wetu

WAHARIRI wa magazeti ya kila siku ya This Day Bw. Ernest Mwitumba na Kulikoni, Bw. Nyaronyo Kicheere, wamekataa kuomba msamaha kwa Mbunge wa Musoma Vijijini, Bw. Nimrod Mkono, kwa madai ya kuandika habari za kumchafulia jina, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Wahariri hao walitoa tamko hilo jana muda mfupi baada ya kupewa ushauri wa kuomba msamaha na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Mark Bomani, mbele ya Kamati hiyo, ujumbe uliofuatana na Bw. Mkono ukiongozwa na Wakili Eric Ng'maryo na wawakilishi wa Mabaraza ya Habari kutoka nchi za Uganda, Kenya, Malawi na Zambia.

Awali akitoa malalamiko yake dhidi ya magazeti hayo baada ya kula kiapo cha kusema ukweli, Bw. Mkono alidai kuwa magazeti hayo yanalalamikiwa na wawalalamikaji wawili ambao ni kampuni ya Mkono and Company na Bw. Mkono.

Kwa mujibu wa malalamiko ya Bw. Mkono, gazeti ya This Day lilichapisha habari kwenye ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza, chenye maana sawa na 'Benki Kuu ya Tanzania (BoT)' imetumia sh. bilioni 8 zenye utata kulipa gharama ya uendeshaji wa kesi'

Bw. Mkono alidai kuwa habari hiyo iliendelea kuonesha kuwa BoT iliilipa kampuni ya uwakili wastani wa sh. milioni 450 na 650 kwa mwezi, gharama ambazo zinadhaniwa kuwa za juu kuliko ilivyo kawaida.

Akinyambulisha maana ya baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye habari hiyo, Bw. Mkono alidai kuwa yalikuwa na lengo la kuelezea jinsi thamani ya fedha hizo ilivyo na utata na zinazoashiria uongo na kwamba ilikuwa na lengo la kuonesha kuwa kampuni hiyo haikustahili malipo hayo.

Kuhusu Gazeti la Kulikoni, Bw. Mkono alilalamikia kichwa cha habari kilichoandikwa 'Kampuni ya Mbunge yachota mabilioni Benki Kuu' ambacho kwa mujibu wa malalamiko hayo, neno 'yachota' lilimaanisha kuiba au kupata au kuchukua fedha hizo kinyume na sheria au bila kufuata taratibu.

Aidha, Bw. Mkono alilalamikia matumizi ya neno Mbunge kwenye habari hiyo aliyosema kuwa yalilenga kumchafulia jina, kwa kuwa neno hilo halina uhusiano na kampuni ya Mkono and Co.

Kutokana na tuhuma hizo, Wakili Ng'maryo iliyekuwa akitoa utetezi kwa niaba ya mteja wake kwa kupitia vifungu vya maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, alidai kuwa tuhuma hizo zinaashiria kuanguka kwa taaluma ya uandishi wa habari nchini, na kwamba ni jambo la aibu na lililokosa ubinadamu.

Aliiomba kamati hiyo ambayo aliita isiyokuwa na meno, itoe ushauri kwa magazeti hayo yaandike habari ya kuomba radhi na kuwasafisha Bw. Mkono na Mkono and Co, na baadaye Kamati hiyo iyaweke magazeti hayo kwenye uangalizi maalumu kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja, ili kuona kama kweli yanajiendesha ka uhuru au yana ajenda ya siri mbali ya kuihabarisha jamii.

Akijibu tuhuma hizo, Bw. Mwitumba alidai kuwa kilichoandikwa ni ukweli na si upotoshaji na kwamba waliridhika na ushahidi wa habari hiyo, pamoja na kuona uwepo wa maslahi ya Taifa na ndiyo maana wakaiandika.

Bw. Mwitumba aliyelazimika kusoma sehemu ya ushahidi uliotumika kuandika habari hiyo, alidai kuwa walitarajia mlalamikaji awe BoT, kwa kuwa ndiye aliyeandikwa kutoa fedha hizo na kumtaka Bw. Mkono kueleza fedha hizo alipewa kwa ajili ya kitu gani ili waandike habari inayoonesha maendeleo ya kilichokuwa kimeandikwa awali.

Kuhusu matumizi ya neno 'kuchota', Bw. Kicheere alidai kuwa licha ya kulenga kutengeneza kichwa cha habari kinachovutia, neno hilo halina maana sawa na wizi.

Alifafanua kuwa neno 'kuchota' limetumika baada ya kuona kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na kwamba hakiwezi kuchukiliwa ila kuchotwa.

Kuhusu matumizi ya neno Mbunge, Bw. Kicheere, alidai kuwa Bw. Mkono ni mbunge na kwamba yeye amefundishwa kuwa jambo la mtu mkubwa kama Rais au Waziri ni habari.

Hata hivyo, Kamati ilitaka kurudiwa kwa kipengee cha ushahidi uliosomwa na Bw. Mwitumba unaodaiwa kupatikana kutoka taarifa ya Utawala wa BoT, ikijibu hoja ya Mkaguzi wa Mahesabu kuhusu matumizi ya fedha hizo na kuhoji sababu za kutokuwapo kwenye habari hizo.

Kipengee hicho kilichorudiwa kusomwa, ambacho hakikuwekwa kwenye habari hiyo, kilieleza kuwa malipo hayo yalifanyika kwa kampuni hiyo kutokana na unyeti wa shauri lililopo mahakamani na uzoefu wa kampuni iliyopewa kazi ya kuwakilisha BoT.

Vile vile, kamati ilihoji sababu za kutokuwapo kwa mawasiliano kati ya magazeti hayo na Bw. Mkono au mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Mkono and Co., kabla ya kutoa ushauri uliokataliwa na wahariri hao.

Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Hamza Kasongo, alimtuhumu Wakili Ng'maryo na Bw. Mkono kwa kutumia maneno yanayolingana na wanayoyakataa, kama kuanguka kwa taaluma ya uandishi wa habari Tanzania, alikosema ni kuhusisha wanataaluma na vyombo visivyohusika.

Bw. Kasongo aliema hata maelezo ya kwamba kamati hiyo iliyokuwa inasikiliza shauri hilo haina meno, yaliyotumiwa mara kadhaa na Bw. Mkono na Wakili Ng'maryo, ni kinyume na mwenendo wa jamii iliyostaarabika.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Bw. Mkono alisema anaamini ameshinda, kwa kuwa alitaka kuonesha kuwa kanuni hazikufuatwa na kamati ililiona na kuwataka wahariri hao kuomba radhi.

Naye Kapteni mstaafu Audax Kameja, ambaye ni mmoja wa wenye hisa kwenye kampuni ya Mkono and Co., alisema uamuzi wa wahariri hao ni wa waajiriwa na kwamba wao watasubiri uamuzi wa Bodi inayoendesha kampuni inayochapisha magazeti hayo.
 
Hivi majuzi nilisoma kwenye vyombo vya habari vikisema, Mkono anapaswa kuombwa msamaha na gazeti hilolililoandika yeye kuhusishwa na matumizi mabaya ya Benki kuu.

NI kwamba alipeleka malalamiko yake kwenye Baraza la Habari Tanzania(MCT), ambalo liliona gazeti hilo kukiuka maadili kuandika tuhuma hizo Zilizotolewa na Dr. Slaa kule mwembe yanga.

Cha kufurahisha ni kujua ni akina nani waliosikiliza madai hayo na kutoa hukumu, ni kwamba maamuzi hayo yalisomwa na Bomani.

Kilichojitokeza ni kuwa gazeti hilo lilipinga hukumu hiyo(sijui litafanywaje kwa kugomea maamuzi)

Kilichonishangaza kwa saga lote hilo ni kuwa, Mkono kama wakili kazi zake nyingi anazifanyia mahakamani. Kwa kuogopa kulipeleka hili mahakamani na badala yake kwenda kwenye baraza tu; Je se kweli kuwa ameikimbia ofisi yake?
 
Hivi majuzi nilisoma kwenye vyombo vya habari vikisema, Mkono anapaswa kuombwa msamaha na gazeti hilolililoandika yeye kuhusishwa na matumizi mabaya ya Benki kuu.

NI kwamba alipeleka malalamiko yake kwenye Baraza la Habari Tanzania(MCT), ambalo liliona gazeti hilo kukiuka maadili kuandika tuhuma hizo Zilizotolewa na Dr. Slaa kule mwembe yanga.

Cha kufurahisha ni kujua ni akina nani waliosikiliza madai hayo na kutoa hukumu, ni kwamba maamuzi hayo yalisomwa na Bomani.

Kilichojitokeza ni kuwa gazeti hilo lilipinga hukumu hiyo(sijui litafanywaje kwa kugomea maamuzi)

Kilichonishangaza kwa saga lote hilo ni kuwa, Mkono kama wakili kazi zake nyingi anazifanyia mahakamani. Kwa kuogopa kulipeleka hili mahakamani na badala yake kwenda kwenye baraza tu; Je se kweli kuwa ameikimbia ofisi yake?
Yaani hapo kakimbia ofisi kabisa, tena ni sawa na golikipa ambaye penati inapigwa yeye anakimbia goli na kwenda kupiga yeye mwenyewe, hapo kuna woga wa mtu mzima au kaona nini kinaweza kumpata hivyo anaenda kuomba msaada kwa wengine ili kunyamazisha media, hiyo no haiwezekani bila hilo gazeti sisi walala hoi tungejuaje Mkono ni fisadi? Sisi lengo letu ni kuona nchi yetu inakuwa safi bila ya mafisadi.
 
huenda ameona kuwa kwa nini atumie nyundo wakati anaweza kumuua kwa ujiti?
 
Cha kufurahisha kama sio kuchekesha ni sababu ya msingi iliyotolewa na Bomani kuwa ThisDay waliandika ile habari bila kwanza kupata maoni ya Mkono.

Swali, hivi na huu utamaduni wetu wa kutotoa ushirikiano kwa waandishi hata tunapotafutwa mbona haukupewa kipaumbele?

Kama Mkono alikuwa na maoni tofauti na yaliyoandikwa kwenye gazeti kwanini asiwaombe ThisDay wayachapishe ukurasa wa mbele kwa uzito ule ule, badala ya ThisDay kukanusha taarifa ambayo Mkono hajaipinga?
 
Mbunge wa Musoma Vijijini Bw. Nimrod Mkono amesema kuwa yuko tayari kumtetea aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu endapo Gavana huyo atafunguliwa mashtaka katika mahakama ya sheria.

mkonobc.jpg

Bw. Mkono amesema hayo akidai kuwa kama mwanasheria ni jukumu lake kumtetea mtu yeyote anayehitaji msaada wake wa kisheria. Kwa mujibu wa ile iitwayo "orodha ya ufisadi" iliyotolewa na Wapinzani. Bw. Mkono ni mmoja wa watu ambao wamedaiwa kutumia Benki Kuu kujipatia fedha zaidi.

Bw. Mkono ambaye amedai kuwa alimtembelea Balali hospitalini haoni tatizo lolote lile kumtetea Balali. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Gray Mgonja amedai kuwa endapo uchunguzi utafanyika, basi wataonesha kuwa yeye ni safi. Bw. Mgonja ni mmoja wa watu wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za ubadhirifu Benki Kuu. Hata hivyo mtu mwingine anayetajwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Basil Mramba.

Bw. Mramba hata hivyo amekataa kusema lolote kuhusu ubadhirifu katika akaunti ya EPA

Naye Mwanasheria Mkuu Bw. Mwanyika amesema kuwa anaangalia sheria za nchi ili aweze kuona ni sheria gani zinaweza kutumika katika kufuatilia na hatimaye kuwafikisha wale wanaotuhumiwa ubadhirifu katika Benki Kuu.

Habari nyingine za uhakika zinasema kuwa Bw. Balali hajamuagiza mtu yeyote kuzungumza kwa niaba yake kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari nyumbani na madaktari wake wameendelea kumshauri kuzingatia afya yake huku masuala yake ya kisheria yakichukua nafasi ya pili.

"Balali amesema hajazungumza na mtu yeyote, na anadai inawezekana ni kweli mdogo wake ambaye hayuko Boston kama ilivyodaiwa ndiye amezungumza na vyombo vya habari, lakini Balali mwenyewe hajamwagiza mtu yeyote kufanya hivyo" kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Gavana huyo.
 
Back
Top Bottom