Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Mbao ya chuma

Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
12
Reaction score
57
Wakuu wa JF hope mko poa sana na maisha yanaenda fresh pande zenu.

Ninaandika uzi huu kwa uchungu sana kuhusu rafiki yangu wa kufa na kuzikana (he Is like a brother to me), huyu jamaa alijitumbukiza kwenye FOREX yapata mwaka sasa na hakuna kitu amefaidika nacho zaidi ya kupoteza pesa. Jamaa ni student nimekua nikimshauri sana aachane na hiyo miradi ya wazungu huko Ulaya kwani hakuna anachopata zaidi ya kuunguza account every now and then.

Jamaa ana hali mbaya sana kwa sasa ameuza kila kitu hana hata nguo ya kuvaa/kiatu lakini pesa yote ya boom + anayotumiwa kwa matumizi mengine anatumbukiza FOREX. Jana nimeongea nae aachane na hii mishe naona kama ameanza kunichukia flani, daily yupo YOUTUBE anafatilia videos about FOREX, ana groups za Telegram & Whatsapp zaidi ya 50 za mambo hayo ya FOREX na nyingi analipia. Kila nikimpa ushauri ananiona kama mimi ni kikwazo cha maisha yake, he keeps on saying anzia January nakua tajiri namwambia kirahisi hivo anasema we tulia hizi hela ni za bure lazima nizipate.

Then he keeps on saying HELA za FOREX zipo tuu na ni zabure kabisa eti mimi ndio mshamba sizitaki hizo ela za bure. FOREX complications ni nyingi sana, daily ananitajia watu wa uko SOUTH AFRICA waliofanikiwa, namjibu waliofanikiwa ni mmoja kwa milioni Ila haelewi. Bado sijajua aliemdanganya aingie kwenye hiyo mishe ni nani.
Ukimwambia FOREX ni mchezo kama UPATU anamind sana eti nisidharau biashara za watu.

Wakuu nimpe ushauri gani huyu best yangu maana anaangamia mbele ya macho yangu and sitaki kuona hilo linatokea.

Best regards,
Mbao Ya Chuma.
 
Amesha pata uraibu wa forex,maana Kama umemshauri hataki mwache apigwe atakuja ashtuke tu na maana wasemi hunena kuwa kupanga ni kuchagua.
 
Kwangu forex ndio inaniweka mjini..nimepaga Nyumba kwa sababu ya forex na ninaishi kwa sababu ya forex..huyo kuna kosa analofanya..na ni la kawaida nalo ni kwamba hana business plan ya daily au malengo..na hasa anawaza utajili wa haraka kupitia forex kitu ambacho sio ukweli...
Lakini huenda anategemea signals za kwenye magroup hayo anayolipia kitu ambacho ni kosa kubwa sana kwenye forex
Zaidi atafute mwalimu wa karibu Ili amfundishe hakika atafanikiwa
 
Usimkatishe tamaa.
Mimi nimeacha kazi nilikuwa meneja mauzo Vodacom kanda ya kaskazini nikaaacha kazi.
Nimejenga sasa nina usafiri nimeoa....
Ninaishi maisha yangu ninayotaka.
Huyo anakosea mahali anichek nimtumie vitabu 9 tu akimaliza kusoma atafaidi.
Tatizo letu hatutaki kusoma...tunapenda kutumia maarifa ya waliosoma huko kwenye magrup.
 
Mbao ya chuma

Hii biashara haina Disclaimer kwamba unaweza kufanikiwa ama kupoteza pesa zako?

Mwambie asome disclaimer na aielewe vizuri
 
Kwangu forex ndio inaniweka mjini..nimepaga Nyumba kwa sababu ya forex na ninaishi kwa sababu ya forex..huyo kuna kosa analofanya..na ni la kawaida nalo ni kwamba hana business plan ya daily au malengo..na hasa anawaza utajili wa haraka kupitia forex kitu ambacho sio ukweli...
Lakini huenda anategemea signals za kwenye magroup hayo anayolipia kitu ambacho ni kosa kubwa sana kwenye forex
Zaidi atafute mwalimu wa karibu Ili amfundishe hakika atafanikiwa
Dah hivi mwalimu kwa hapa dar nitapata wapi maana naona uvivu kusoma
 
Usimkatishe tamaa.
Mimi nimeacha kazi nilikuwa meneja mauzo Vodacom kanda ya kaskazini nikaaacha kazi.
Nimejenga sasa nina usafiri nimeoa....
Ninaishi maisha yangu ninayotaka.
Huyo anakosea mahali anichek nimtumie vitabu 9 tu akimaliza kusoma atafaidi.
Tatizo letu hatutaki kusoma...tunapenda kutumia maarifa ya waliosoma huko kwenye magrup.
Nitumie hivyo vitabu PM mkuu
 
Back
Top Bottom