Kumsomesha mchumba najua kumewaliza na kuwatesa wengi, bahati mbaya au nzuri nami nimeangukia katika mtego huo.
Kutokana na hali ya kiuchumi najua sitaoa kwa miaka miwili mitatu ijayo.
Nimeona nimlee mtoto ambae kwa kweli ni mzuri na anazidi kupendeza.
Yeye hajui chochote, nimeongea na mlezi wake kakubali. Ila najua kuna mawili, ukiacha kifo kututenganisha, ni aje abadilike awe na tabia mbaya au anikatae.
Najipanga kisaikolojia kwa yote huku nikimuomba Mungu kwangu na kwa huyu mtoto asibadilike na aje anipende.
Dua zenu pia ushauri nini naweza fanya kudhibiti tabia na mengineyo kwa wenye uzoefu na wajuzi.