Akili Kichwani
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,508
- 220
Pole sana kwa yanayokusibu.
Kwa kusoma hiki ulichoandika ni vigumu sana kulielewa tatizo lako.
Inaelekea kuna kitu hujasema bado.
Kwa mfano, una matatizo makubwa sana kwenye ndoa yako
kiasi ambacho katika hali ya kawaida
ungejiodokea tu kama walivyosema wachangiaji waliotangulia.
Pia kawaida mwanaume hahami chumba
au kunyima tendo la ndoa bila sababu kubwa ya msingi.
Mwanamke kuhamwa chumba na mumewe au kukataliwa
katika tendo ni tusi kubwa sana (IMO). Mara nyingi wanawake ndio huhama au hata kukataa.
Wewe bado mdogo kiumri na hujazaa
hapo kwa mumeo wala hujaonyesha kuchangia katika upatikanaji wa mali za ndoa ( nyumba na rasilimali nyingine).
Kinachokufunga kamba ni nini? Wanawake wengine hawaondoki kwa sababu:
1. Pamoja na matatizo ya ndoa bado waume wana chembechembe za upendo/mapenzi kwao
2. Ndoa ina watoto na mwanamke anatamani watoto walelewe kwenye familia iliyo kamili
3. Mwanamke keshawekeza sana kwenye ndoa hiyo kwa maana ya miaka aliyokaa, na nguvu zake nyingine
4. Utegemezi kwa mume
Sasa wewe kwenye hizo hapo na nyingine labda utuambie ni kipi kimekunfunga hapo ndipo tukupe mawazo namna ya ku survive.
WOS, uliyoyasema ni sawa................... ila mi ningependa aendelee kuvumilia na avumilie zaidi................ imeandikwa kuwa atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka................. majaribu hayana SI unit ............... hayo kwake ni majaribu na akishayashinda ndio atavikwa taji............... sasa akikimbia ndoa yake hilo taji atavikwa kwa ushujaa gani? ............ukisoma michango ya wengi humu wanamshauri achape mwendo!!............... jamani, mbona siku hizi tunawakatisha tamaa na kuwaona washamba wale wote wanaojitahidi kuvumilia??..............
nilivyomuelewa huyu dada ni kuwa yeye amefocus katika kuijenga ndoa yake na sio maraha na mabinjuano ya hapa duniani (japo nayo muhimu)................ so nadhani tumtie moyo na mwenye maujanja ya ziada ampatie ili naye awe na ndoa iliyo mawazoni mwake kama wengine............. eeh, ni haki yake kuwa na ndoa anayoiwaza jamani, tusisahau na hilo..................
hakuna kilichonifunga,nilikuwa najitahd kuvumilia labda ipo cku atabadilika
.na kujaribu kutafuta njia nyngne za kusolve tatzo kabla ya kuamua kutoka na uki
chukulia n mume wa ndoa so huwez kukurupuka ktkmaamuz.
lakn m sihitaj chcht alichochuma na wala tulichochuma koz mbal na uanafunz
n mjasiriamal
nimependa sana jibu lako dada............... endelea kuvumilia, tena uvumilie zaidi na ujipe moyo mkuu............. unalofanya si la kijinga, huo ndio ukubwa.................. unapigana na kuvumilia kulinda kitu muhimu sana kwako na tena ni kile unachoamini kuwa ni bora!!.................. kaza mwendo na usikatishwe tamaa na mawazo ya watu wasiojali tena kuwa uvumilivu ni nguzo ya kila mahusiano...................
huwezi kujua ni lini mwenzio atajutia matendo anayokufanyia............... unaweza kuondoka leo, kumbe naye amebakiza wiki moja tu kubadilika................... wahenga walisema kuwa ngoma ikilia sana ujue i-karibu kupasuka........... wanaokuambia uondoke ni sawa na kusema ngoma ikilia sana jiondokee zako!!.................. asikudanganye mtu, manyanyaso yakizidi, ujue maisha mazuri unayoyasubiri yamekaribia..................
big up mkuu.................. vumilia mpaka kieleweke...................