Nimvumilie mume huyu au nimuache?

Nimvumilie mume huyu au nimuache?

Pole sana kwa yanayokusibu.
Kwa kusoma hiki ulichoandika ni vigumu sana kulielewa tatizo lako.
Inaelekea kuna kitu hujasema bado.
Kwa mfano, una matatizo makubwa sana kwenye ndoa yako
kiasi ambacho katika hali ya kawaida
ungejiodokea tu kama walivyosema wachangiaji waliotangulia.
Pia kawaida mwanaume hahami chumba
au kunyima tendo la ndoa bila sababu kubwa ya msingi.
Mwanamke kuhamwa chumba na mumewe au kukataliwa
katika tendo ni tusi kubwa sana (IMO). Mara nyingi wanawake ndio huhama au hata kukataa.
Wewe bado mdogo kiumri na hujazaa
hapo kwa mumeo wala hujaonyesha kuchangia katika upatikanaji wa mali za ndoa ( nyumba na rasilimali nyingine).

Kinachokufunga kamba ni nini? Wanawake wengine hawaondoki kwa sababu:
1. Pamoja na matatizo ya ndoa bado waume wana chembechembe za upendo/mapenzi kwao
2. Ndoa ina watoto na mwanamke anatamani watoto walelewe kwenye familia iliyo kamili
3. Mwanamke keshawekeza sana kwenye ndoa hiyo kwa maana ya miaka aliyokaa, na nguvu zake nyingine
4. Utegemezi kwa mume
Sasa wewe kwenye hizo hapo na nyingine labda utuambie ni kipi kimekunfunga hapo ndipo tukupe mawazo namna ya ku survive.

WOS, uliyoyasema ni sawa................... ila mi ningependa aendelee kuvumilia na avumilie zaidi................ imeandikwa kuwa atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka................. majaribu hayana SI unit ............... hayo kwake ni majaribu na akishayashinda ndio atavikwa taji............... sasa akikimbia ndoa yake hilo taji atavikwa kwa ushujaa gani? ............ukisoma michango ya wengi humu wanamshauri achape mwendo!!............... jamani, mbona siku hizi tunawakatisha tamaa na kuwaona washamba wale wote wanaojitahidi kuvumilia??..............

nilivyomuelewa huyu dada ni kuwa yeye amefocus katika kuijenga ndoa yake na sio maraha na mabinjuano ya hapa duniani (japo nayo muhimu)................ so nadhani tumtie moyo na mwenye maujanja ya ziada ampatie ili naye awe na ndoa iliyo mawazoni mwake kama wengine............. eeh, ni haki yake kuwa na ndoa anayoiwaza jamani, tusisahau na hilo..................

hakuna kilichonifunga,nilikuwa najitahd kuvumilia labda ipo cku atabadilika
.na kujaribu kutafuta njia nyngne za kusolve tatzo kabla ya kuamua kutoka na uki
chukulia n mume wa ndoa
so huwez kukurupuka ktkmaamuz.
lakn m sihitaj chcht alichochuma na wala tulichochuma koz mbal na uanafunz
n mjasiriamal

nimependa sana jibu lako dada............... endelea kuvumilia, tena uvumilie zaidi na ujipe moyo mkuu............. unalofanya si la kijinga, huo ndio ukubwa.................. unapigana na kuvumilia kulinda kitu muhimu sana kwako na tena ni kile unachoamini kuwa ni bora!!.................. kaza mwendo na usikatishwe tamaa na mawazo ya watu wasiojali tena kuwa uvumilivu ni nguzo ya kila mahusiano...................

huwezi kujua ni lini mwenzio atajutia matendo anayokufanyia............... unaweza kuondoka leo, kumbe naye amebakiza wiki moja tu kubadilika................... wahenga walisema kuwa ngoma ikilia sana ujue i-karibu kupasuka........... wanaokuambia uondoke ni sawa na kusema ngoma ikilia sana jiondokee zako!!.................. asikudanganye mtu, manyanyaso yakizidi, ujue maisha mazuri unayoyasubiri yamekaribia..................

big up mkuu.................. vumilia mpaka kieleweke...................
 
hakuna kilichonifunga,nilikuwa najitahd kuvumilia labda ipo cku atabadilika
.na kujaribu kutafuta njia nyngne za kusolve tatzo kabla ya kuamua kutoka na uki
chukulia n mume wa ndoa so huwez kukurupuka ktkmaamuz.
lakn m sihitaj chcht alichochuma na wala tulichochuma koz mbal na uanafunz
n mjasiriamal
Kwanza hapo red, kama wazazi wake walishindwa kumbadilisha, utawezaje wewe?
Kuendelea kusubiri kwako unaweza kujishtukia miaka imepanda na umepoteza nusu ya uhai wako kujaribu kutengeneza lisilokuwa.
Je, umewahi kufikiri kuwa hilo linalokushinda wewe (kuondoka) anaweza kulifanya yeye - kukuondosha - wakati wowote?
Ikifikia hadi hiyo, utafanya nini, utaendelea kulia lia ili akuhurumie ubaki?

Umesema ana ujeuri wa vijisenti, wewe ujeuri wako nini? Ulitakiwa na wewe uwe na fahari yako, uelewe hadhi yako na usiwache fursa zako za maisha mikononi mwa asiyekuthamini.

Sikushauri moja kwa moja kuondoka kwani adhabu ya kaburi...lakini kwa mtaji huo usipoamua haraka, utakuwa umefilisika kimaisha. Na maisha ni mafupi sana! Mwenzako ameamua kuishi kivyake, wewe unasubiri uambiwe toka?

 
Yeahh mara nyingi kesi za upande mmoja kama hizi hua tunaambiwa kile kinachoweza kumfanya mshtaki aonekane anaonewa wakati kiukweli yeye ndie mwenye matatizo.

Namshauri awe mkweli na nafsi yake...hana haja ya kutueleza sisi ila ajiangalie kwa jicho lisilo na upendeleo aone amechangia vipi kufika hapo walipofika kabda ya kumpaka mwenzake matope huku yeye angang'aa!


jambo jingie wanakuwa so emotional kiasi cha kutaka watu tuamini nini anasema japo ukijaribu kuingia ndani ya tatizo wanakwepa hahahaha
 
ahhh wewe so ata nyuk au mbu akikuuma aupaswi kumtoa kwenye ngozi kwsababu YEYE PIA NI KIUMBE CHA MUNGU NA ANAHITAJ DAMU KUISHI?

kumbe nyie ndo mnaopingana na ule msemo wa fuata nyuki ule asali eeee!!!.................. ukitaka asali lazima utoe ka-ofa kidogo ka kung'atwa na nyuki ndo kitaeleweka.................... kamuulize hata mkulu anajua mambo ya kuliwa ili ule!!.............

anyway, ngoja nisubiri hapahapa nisubiri kushuhudia zali linaloibuka hivi punde............. aimeen, ngoja mwenyewe aje akusikie kipenzi chake unamfananisha na mbu................... ila tu usije kuniita kuamulia ugomvu hapo atakapokuwa anakupa kibano......................
 
WOS, uliyoyasema ni sawa................... ila mi ningependa aendelee kuvumilia na avumilie zaidi................ 1. imeandikwa kuwa atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka................. majaribu hayana SI unit ............... hayo kwake ni majaribu na akishayashinda ndio atavikwa taji............... 2. sasa akikimbia ndoa yake hilo taji atavikwa kwa ushujaa gani? ............ukisoma michango ya wengi humu wanamshauri achape mwendo!!............... jamani, mbona siku hizi tunawakatisha tamaa na kuwaona washamba wale wote wanaojitahidi kuvumilia??..............

nilivyomuelewa huyu dada ni kuwa yeye amefocus katika 3. kuijenga ndoa yake na sio maraha na mabinjuano ya hapa duniani (japo nayo muhimu)................ so nadhani tumtie moyo na mwenye maujanja ya ziada ampatie ili naye awe na ndoa iliyo mawazoni mwake kama wengine............. eeh, ni haki yake kuwa na ndoa anayoiwaza jamani, tusisahau na hilo..................

nimependa sana jibu lako dada............... endelea kuvumilia, tena uvumilie zaidi na ujipe moyo mkuu............. unalofanya si la kijinga, huo ndio ukubwa.................. unapigana na kuvumilia kulinda kitu muhimu sana kwako na tena ni kile unachoamini kuwa ni bora!!.................. kaza mwendo na usikatishwe tamaa na mawazo ya watu wasiojali tena kuwa uvumilivu ni nguzo ya kila mahusiano...................

huwezi kujua ni lini mwenzio atajutia matendo anayokufanyia...............4. unaweza kuondoka leo, kumbe naye amebakiza wiki moja tu kubadilika................... wahenga walisema kuwa 5. ngoma ikilia sana ujue i-karibu kupasuka........... wanaokuambia uondoke ni sawa na kusema ngoma ikilia sana jiondokee zako!!.................. asikudanganye mtu, manyanyaso yakizidi, ujue maisha mazuri unayoyasubiri yamekaribia..................

big up mkuu.................. vumilia mpaka kieleweke...................
Sidhani kama mtu wa kawaida na busara zake angetoa maoni ya moja kwa moja huyu dada aondoke bila sababu za msingi. lakini pia hatujapata version ya mlalamikiwa, inawezekana jkuwa na yeye anahusika kwa japo sehemu ndogo ya tatizo. Lakini ikiwa kama alivyoeleza ni kweli yote, hapo kwenye red pananipa mashaka:
1. Unakusudia uokozi gani? Wa mbinguni? Hapo siwezi kusema lolote kwa sababu "Where there is faith, reasoning is not needed", lakini ikiwa ni kwa uokozi wa duniani, ndio unakuta waliovumilia kusubiri mbivu, wanaambukia kula mbovu.

2. Kuna haja gani ya kuitwa shujaa wa uvumilivu. mwili umejaa majeraha, moyo umejaa makovu? Uridhike kwa kuitwa shujaa wakati muda wote wa mapambano hakuna aliyekuthamini. Kukimbia ni mbinu moja ya vita ikiwa unataka uandike historia yako mwenyewe na sio kuandikiwa ukishaondoka duniani.

3. Watu wanaoana kwa kutaka hizo raha, ikiwemo mibanjuano, tena hapa duniani. Ukizikosa hizo katika ndoa, utabanjuliwa na mafunza kaburini.

4. Kama ukabaki milele je na mwenzako asibadilike?

5. NGOMA: Hili ndilo linalonitisha zaidi. Kuna hatari akiendelea kuvumilia akaletewa hiyo ngoma na ikapasukia mwilini. Tujilinde na tujikinge na NGOMA.

ANGALIZO LA MWISHO: Ndoa ni makubaliano, ikifuatiwa na maelewano. Ikiwa hakuna maelewano, hakuna ndoa. Vyeti vya ndoa vitakuwepo, lakini maisha ya ndoa yatakuwa yamekosekana. HATA HIVYO; mwamuzi wa mwisho ni muhusika.
 
Kwa hali hiyo ningeshaondoka kabla hata sijaomba ushauri...........your too young to suffer mamie leave the place immediately enjoy ur life...life is too short
 
Pole sana dada,kwenye maisha ya ndoa kuna raha na tabu na kila binadamu ana uwezo wake wa kustahmili,kwa ufupi nikupe hongera kwa kuweza kuvumilia machungu yote hayo mimi binafsi siwezi hata kidogo,kwa upande wangu nadhani sasa imeshafika mahala pake
Kwanza jiulize wewe na yeye mlikua mke na mume na ukiwa kama mke unamahitaji yako licha ya mavazi na kula bali kukupa haki yako ya ndoa, mkiwa mnalala kila mtu chumba chake na mpaka wewe ndio uende ukamwambia nataka chali leo huoni kama huyo bwana keshakua mumunya kaharibikia ukubwani,
jipange upya kimaisha na wala usisikitike kua umemkosa wako wengi wasiokua na dhiki kama zake.
 
Kama mumeo ana kasoro zoote ulizoorodhesha na wewe ni perfecto; chapa lapa dada haraka.

Ila nahisi na wewe una yako ila umetuficha. Kwa nini nahisi hivyo:

Haiwezekani mwanaume aliyehama chumba akaendelea kuwa na wivu na mkewe maana umesema ana wivu na hakuamini.

Isiji kuwa ameama chumba kwa kuwa amekuona si muaminifu kwenye ndoa.

Je mmeshawahi kuwa na ugomvi kuhusu uaminifu wako? Sikuhukumu maana najua inaweza kuwa ni hisia tu ya mumeo. Nachotaka kusema ni "wewe umechangia nini katika hali kuwa mbaya kiasi hiki? Maana wanaume wengi wanaooa dogo dogo wanachezeshwa shere sana.

Na kama ameama chumba sioni kwa nini mkigombana ukirudi kwenu anakufata. Huyo mwanaume anakupenda ila anakuogopa akidhani (au kweli) kuwa hujatulia.

Kurudi saa nane tisa za usiku inaweza kuwa ni frustration; unless ungetuambia ana nyumba ndogo; ambayo kama ingekuwepo ungeshakuwa replaced maana hana shida na wewe (au at least anazuia hisia zake kwako)
 
Dada Mnyonge acha kuvumilia ujinga,huyo jamaa keshakuchoka au hana mapenzio na wewe,una 26 fanya uamuzi wa maana sasa kuliko kuchelewa ukajuuta baadae,ondoka tafuta kazi jipange na maisha yako na umuombe mungu akusaidie
 
Maneno mafupi na ya busara toka kwa ODM.

Hapo hamna ndoa mama.

Chapa mwendo!!
 
Pole sana kwa matatizo uliyonayo,hapa unaweza kupata ushauri wa kumuacha huyo mwanaume ila bado hatujui ya ndani zaidi yaliyofanya mpaka mkafikia hivi,kwangu mimi naona kuna mambo ambayo yalisababisha mpaka mmefikia hapa na ambayo huwezi kutuwekea hapa kwa undani.
Kwa kuwa umekwishaona kuwa kuna matatizo basi tumia vizuri kitchen party uliyoipata,au ndio siku hizi umeifanya fasheni yaani unashereheka tu bila kujua ni nini mwanaume anataka katika ndoa?
Angalia unavyoona inafaa kulingana na maisha ambayo uliyapanga na haijalishi una degree au phd maisha ni namna unavyoyaendesha si elimu uliyoipata ndiyo itakayoamua mustakabali wa maisha yako zaidi ya kukusaidia tu katika kuyaendesha.

kiongozi umemjjibu vzr sana,awo wanaomshauri aachane na mmewe kwa sbb ana degree,degree nini bana!
 
Ndoa ndoana. Si kanisani ulisema mpaka kifo kitakapowatenga? ni humo humo tu hakuna kutoka, kama ulifanya kosa kwenye uchaguzi huna wa kumlaumu. Komaa tu ndiyo ndoa hiyo.
 
Ndoa ndoana. Si kanisani ulisema mpaka kifo kitakapowatenga? ni humo humo tu hakuna kutoka, kama ulifanya kosa kwenye uchaguzi huna wa kumlaumu. Komaa tu ndiyo ndoa hiyo.

lazima utakuwa umefanana na MWENYE MAPEMBE.
 
tena uko na degree hebu sepa kafanye kazi loh! ww elimu inatakiwa ikukomboe mtoto wakike na sio ikulemaze tena plzzzzzzzzz sasa hapo kuna tofauti gani na mtoto wa la saba jamani kama ww huwezi kufanya maamuzi mwenye degree na wa lasaba atafanya nn sasa
hebu onesha tofauti ya kufikiri
samahani ka ntakua nimekuboa mpz
 
Nafl sory sana to u dada mnyonge, kwanza natamani jina ubadilishe coz kua mnyonge nahc kumechangia kidogo katika hili...nimejaribu pia kufikir juu ya kuona kwenu,alikuoa ukiwa na miaka 22 kwa mujibu wa maelezo yako,nahusisha umri wako na kauli yako ya kishule kwamba umemaliza chuo UD na unampango wa kutafuta kaz.!

Umri sio tatizo lakini mambo ambayo mtu unayafanya katka umri fulani huenda ikawa ndio tatizo,najaribu kujiuliza kwamba "alikuoa ulipomalza tu form six au,? Ulikubali kuolewa kwa kuforegone shule au uliamua kubeba vyote kwa pamoja?

Umesema unampenda sana mumeo evenif kwa mambo anayokutendea kwa sasa mimi cdhani kama yeye anakupenda hasa ukizingatia maana ya upendo.!! Unaweza ukajipa moyo kwamba ni jaribu tu litapita,but umesimama kwenye msingi wa kufanya jaribu hilo lipiteg?

Lakini pia,kuna kitu ambacho hua kinachangia sana ndoa nyingi kupepesuka."KUSUDI" sababu ya kuoana ilikua ninini.nasema sababu kwa sababu katika sababu tutajua kusudi..na kusudi likitimia hapo huwa mwisho wa jambo.!!!

Kuoana ni kufanana.hasa katika mtazamo juu ya ndoa,Je,mlioana au kila mtu alikua na picha yake?.

Sitaki nikuchoshe kwa maswali mengi,lakini wewe una nafasi kubwa ya kutengeneza ndoa yako na kuirudisha hai na ikubariki..agano ulilifanya kanisani na ukamwomba Mungu akusaidie,basi mwombe Mungu tena mkumbushe nae atakusaidia,isaya 43:2.!

Pole sana, lakini nikwambie jambo moja la mwisho kwamba "utapona katika hili kwa kiwango kile kile cha utakavokua mkweli katika hili."
 
Aisee huyu dada nae jasiri...anakufa na tai shingoni. ID yake imemponza dada huyu ambaye mim naamini sio mnyonge kama anavyojiita. mtu na degree aseee bado unakufa na tai shingoni? ha ha ha ha
hivi wanaume pia huwa wanahama chumba? huyo mwanaume nae ni suruali tuu...hakuna kitu kama hicho kwa mwanaume mwenye ufahamu na msimamo..kama maisha ya mahusiano ameona hayana mwelekeo aweke mambo hadharani kila mtu ashike ustaarabu wake.

He yaani mpaka kahama chumba?? Bado umekaa tu unasubiri nini???
Anarudi saa 8 or 9 usiku are you serious?? Ni mlevi?? Je! anakuwa anatoka wapi??
Mahusiano ya nje?? Unajua??

We chukua hatua si mpaka kwa hisani ya watu wa marekani ndo uelewe
Chapa mwendo Ndoa ndoa ndo nini??? Waliachana kina Winie Mandela ije kuwa wewe??
Yanini ujipe matezo duniani wakati bado unajipenda?? Tena una degree halafu unailalia
Tu kitandani?? Halafu we mwanamke wa wapi wewe bado umelala mpaka leo
Eti unanyanyaswa umekaa tu?? Hivi husikii hata wanaharakati wanavyosema??
Wanawake wanaweza??? Hebu funguka macho wewe acha kulegea ahhh
Cha uzembe kama huo bana............
 
Aisee huyu dada nae jasiri...anakufa na tai shingoni. ID yake imemponza dada huyu ambaye mim naamini sio mnyonge kama anavyojiita. mtu na degree aseee bado unakufa na tai shingoni? ha ha ha ha
hivi wanaume pia huwa wanahama chumba? huyo mwanaume nae ni suruali tuu...hakuna kitu kama hicho kwa mwanaume mwenye ufahamu na msimamo..kama maisha ya mahusiano ameona hayana mwelekeo aweke mambo hadharani kila mtu ashike ustaarabu wake.

hebu jaribu kutake as ni mtu mwenye ufahamu na msimamo sasa ndo amefanya hvyo,what does t comunicate kwa mtendwa.? Ts rly a problem...
 
Aisee huyu dada nae jasiri...anakufa na tai shingoni. ID yake imemponza dada huyu ambaye mim naamini sio mnyonge kama anavyojiita. mtu na degree aseee bado unakufa na tai shingoni? ha ha ha ha
hivi wanaume pia huwa wanahama chumba? huyo mwanaume nae ni suruali tuu...hakuna kitu kama hicho kwa mwanaume mwenye ufahamu na msimamo..kama maisha ya mahusiano ameona hayana mwelekeo aweke mambo hadharani kila mtu ashike ustaarabu wake.


Hapo kwenye red nakubaliana na wewe mkuu huyo si mwanaume ama mwingine ananuna mwezi mzika kha??!!!
 
Back
Top Bottom