ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,852
Kila biashara inamitihani yake. Usifikiri hardware hawafirisiki mkuuu. Au usifikiri wote waiofanya biashara za kusafirisha maliasili walifilisika. Kila mmoja katika field yake na kwa bahati mbaya au nzuri kila aina ya biashara au shuguli inamatajiri wa kutupwa na pia inamasikini wa kutupwa.Mkuu inategemea uko location gani.
Ila Kama upo dar au dodoma biashara rahisi na isiyooza ni ya vifaa vya ujenzi.
Ingekuwa Mimi ndio ww na Nina mtaji Kama huo nisingeumiza kichwa.
Ningechukua milioni 20 nikaanzisha hardware nje ya mji maeneo Kama kiluvya,goba,madale,vikindu n.k.
Halaf ile m 30 ingekaa tu kwenye akaunti wakati huo naisoma biashara inakwendaje?
Yaani wala usijiingize kwenye mabiashara makubwa yanayohusisha vibali vya maliasili au vibali vya kusafirisha nje ya nchi,utajikuta hela imepukutika wakati hata hyo biashara haijaanza kufanyika.
Milioni 50 Ni hela nzuri ukituliza kichwa lakini pia ni hela ndogo ukibugi utajikuta inakupita Kama upepo.
Tazama kilimo, madini, wauza mandazi etc utangundua kuna matajiri na masikini