Nina $ 23,000 ila sijui biashara gani inanifaa

Nina $ 23,000 ila sijui biashara gani inanifaa

Mkuu inategemea uko location gani.
Ila Kama upo dar au dodoma biashara rahisi na isiyooza ni ya vifaa vya ujenzi.

Ingekuwa Mimi ndio ww na Nina mtaji Kama huo nisingeumiza kichwa.

Ningechukua milioni 20 nikaanzisha hardware nje ya mji maeneo Kama kiluvya,goba,madale,vikindu n.k.

Halaf ile m 30 ingekaa tu kwenye akaunti wakati huo naisoma biashara inakwendaje?

Yaani wala usijiingize kwenye mabiashara makubwa yanayohusisha vibali vya maliasili au vibali vya kusafirisha nje ya nchi,utajikuta hela imepukutika wakati hata hyo biashara haijaanza kufanyika.

Milioni 50 Ni hela nzuri ukituliza kichwa lakini pia ni hela ndogo ukibugi utajikuta inakupita Kama upepo.
Kila biashara inamitihani yake. Usifikiri hardware hawafirisiki mkuuu. Au usifikiri wote waiofanya biashara za kusafirisha maliasili walifilisika. Kila mmoja katika field yake na kwa bahati mbaya au nzuri kila aina ya biashara au shuguli inamatajiri wa kutupwa na pia inamasikini wa kutupwa.
Tazama kilimo, madini, wauza mandazi etc utangundua kuna matajiri na masikini
 
Mkuu inategemea uko location gani.
Ila Kama upo dar au dodoma biashara rahisi na isiyooza ni ya vifaa vya ujenzi.

Ingekuwa Mimi ndio ww na Nina mtaji Kama huo nisingeumiza kichwa.

Ningechukua milioni 20 nikaanzisha hardware nje ya mji maeneo Kama kiluvya,goba,madale,vikindu n.k.

Halaf ile m 30 ingekaa tu kwenye akaunti wakati huo naisoma biashara inakwendaje?

Yaani wala usijiingize kwenye mabiashara makubwa yanayohusisha vibali vya maliasili au vibali vya kusafirisha nje ya nchi,utajikuta hela imepukutika wakati hata hyo biashara haijaanza kufanyika.

Milioni 50 Ni hela nzuri ukituliza kichwa lakini pia ni hela ndogo ukibugi utajikuta inakupita Kama upepo.
Ni sawa ulichoongea ndio maana nimekupa like. Lakini milioni 20 kwa hardware ni ndogo sana mkuu
 
Wazanzibari nao wanatolea macho hizo fursa hapo "kwao" sasa wewe "Chogo" ndo ukajidai unajua kukamata fursa kwao. Hawachelew kukutoa dv
Kujaribu ndio kila kitu mimi niko huku mbona hakuna swala kama hilo huwa nakodi magari sometimes kazi yangu inajumuisha sana watu so vipindi kadhaa inabidi nipate magari ya ziada hapo nakodi kwa watu , so naona sana uwanja wa wanaokodisha magari kikubwa kua na mtu wa kumpa abc, tena hata usimamii unazikabidhi kwenye kampuni mnakubaliana kiasi zinakua kwenye kampuni husika wewe unakaa kando unakula hela yako tu taratibu. Kikiwa kipindi cha high season ambayo kwa Zanzibar ni kuanzia mwezi wa saba mpaka mwezi wa nne kama hujawahi booking na kama hujulikani basi hata magari hupati yote yanakua occupied
 
Wanajamii nimekuwa na wakati mgumu wa kuamua kufanya biashara gani itakayonifaa nitakapoamua kuacha kuangaika kwenye kazi za watu,

Nahisi pesa nilionayo($23,000=milioni 50 hivi za shilingi) inafaa kuwekeza ila nakuwa na wakati mgumu wa biashara hipi inafaa kulingana na pesa nilionayo au njia zipi nipitie ili niwe na mafanikio katika biashara yangu

Kwa mwenye kuwa na uelewa au uzoefu na maswala ya biashara na ushauri wa mambo haya anaweza kunishauri nipite njia zipi au nini nifanye kuwa bora katika biashara yangu ya aina yeyote ninayotaka kufanya

NINAWAKARIBISHA WAKUU.
Mi nikopeshe $3000 kwa mwaka nakupa 20% mkataba wa miaka miwili. Meaning after 2yrs narudisha $4200
 
Kama ni pesa huitegemei kwa chakula basi ingia Zanzibar, tafuta kampuni ya utalii ongea nao ziko nyingi haswa zenye magari ya kukodisha mkubaliane bei huwa sio chini ya laki tano kwa mwezi kama utampabdereva moja moja au inaweza fika dollar 30 kwa siku kama kampuni wataichukua maana wao wanakodisha kwa dollar 50 mpaka 60 kwa siku. Ukishapata kampuni sasa nunua alphard 3 kila moja Zanzibar haizidi milioni 12 mpaka na usajili hapo pia unaweza changanya magari ukawa na ya aina tofauti ila alphard isikose ndio habari ya mjini kwa sasa kwa kampuni ikiwa sambamba na prado tx (model flani ya kati hivi sio old ila prado ghari wewe chukua gari zisizidi m12), unaweza chukua Alphard na suzuki vitara au na toyota hizi size ya suzuki vitara. Kwa kila mwezi hutokosa 1.5m sasa sio ya kula hiyo unakusanya unaongeza magari hapo inamaana kila miezi 6 unaongeza gari moja zikifika kumi basi zinatosha, usihofu kuhusu kuharibika barabara za zenji nzuri utafanya kazi ya service tu ambayo kwa mwezi ni kumwaga oil pekee ndio kinafanyika huku. Wakati ukiwa umezikodisha kwa mtu fungua website anza kutafuta wageni mtandaoni na kukodisha magari kwa wahitaji wazawa na wageni, basi utafurahi mwenyewe.

Kwanza uje utazame fika pale Forodhani kuna kijiwe cha madereva tax, wale ndio wanabeba watalii huku watakupa abc zote. Kuna mtu nimesomea nae primary yaani ni mate wangu mpaka umri kazi yake ndio hiyo now anamalizia ujenzi wa nyumba yake ya milioni 200 so nikikueleza iko hela tambua iko tatizo la watu huwa mitaji na wewe mtaji huo unao. Nimekuchagulia zenji sababu barabara nzuri, kuna bahari sio rahisi watu kuvusha gari kwa nia ya kuiba, wengi wanakuja zenji kutalii hivyo wazawa na wageni wanakodisha sana magari sio bara mpaka upate kampuni ndio watakodisha gari kwako.
Ahsante sana
Unamzungumzia Abdillahi Lali (kibabu)??
 
Huu ushauri mzuri mkuu nitaufanyia kazi siku nikikamilisha hlo duka nitarudi kwako
Ushauri wangu ni huu mkuu: Usimwamini mtu YOYOTE kwenye suala la fedha hata awe ndugu yako labda uwe una uhakika naye. Simamia kila kitu peke yako kama inawezekena. Usipofuata ushauri wangu nina uhakika utarudi hapa ukiwa umeshalizwa! Kila la kheri.
 
Nimepitia Uzi huu mwanzo mwisho. Nipo kwenye ujasiriamali since my graduation in 2013 ninaweza nika recommend with my greatest experience all are here are just ideal and will remain Ideas. Any one can try but does not guarantee success. Kwa mawazo mengi yaliyoko hapa yanaeleza kuwa tatizo pekee linalokwamisha success ni mtaji na kwa kuwa unao no any problems litakukwamisha. Mtaji wako ni mkubwa sana na ni mdogo sana itategemea na wazo utakalochagua. But kumbuka biashara au miradi iliyofanikiwa imetegemea sana muongoza njia katika mafanikio hayo. Ndiyo maana wasitafu wengi au watu wanaopata mtaji kwa namna yeyote na wasiwe na uwezo wa kuongoza njia ya miradi yao huwa wanaishia kukwama.

All the best kwa kupata mtaji but mtaji pekee siyo kikwazo cha mafanikio.
 
Asikudanganye mtu na taxi. Biashara ya taxi huwa inamnufaisha dereva tu. Ninao uzoefu huo. Ni uzoefu mbaya. Mwenye mali anakuwa mtu wa kumfanyia service na matengenezo dereva.
N kazi nzur mkuu ila kwa mimi uwa nna amini nyumba kuliko ngari,
 
Kama Mimi ningenunua IST kama 5 hivi natafuta Madereva then nawapa deal

Zinarudisha 170,000-200,000 kwa Wiki moja so Gari zikiwa used from Japan nina Uhakika matengenezo yanakuaga si sanaa kwa kipindi cha Miaka 2

170,000 * 5 = 850,000
200,000*5 = 1,000,000
850,000 *52= 44,200,000
1,000,000*52= 52,000,000

So itachukua Mwaka 1 kuweza kurudisha pesa yako then unaanza kula Faida baada ya mwaka 1

NB kwa Dar es Salaam risk ya gari kupiga mzinga ni ndogo sana kutokana na Magari jiji kuwa na Gari nyingi
Ukitaka kulia kwenye biashara basi vamia biashara ya magari. Hayo mahesabu uliyopiga; kwenye field hayaendi smooth namna hiyo. Ni watu wengi wanalia kuhusu hii biashara kwani madereva wengi si wa kuaminika kabisa.
 
Unatoa gari kwa kila Mtu? Mi natoa Gari kwa mtu mwenye Familia ambaye hata kwa muonekano awe decent
 
Wanajamii nimekuwa na wakati mgumu wa kuamua kufanya biashara gani itakayonifaa nitakapoamua kuacha kuangaika kwenye kazi za watu,

Nahisi pesa nilionayo($23,000=milioni 50 hivi za shilingi) inafaa kuwekeza ila nakuwa na wakati mgumu wa biashara hipi inafaa kulingana na pesa nilionayo au njia zipi nipitie ili niwe na mafanikio katika biashara yangu

Kwa mwenye kuwa na uelewa au uzoefu na maswala ya biashara na ushauri wa mambo haya anaweza kunishauri nipite njia zipi au nini nifanye kuwa bora katika biashara yangu ya aina yeyote ninayotaka kufanya

NINAWAKARIBISHA WAKUU.
Buy Bitcoin
 
Back
Top Bottom