Nina GPA kubwa 4.1 ya Rasilimali watu(HR) ila kazi sipati

HRO, bila mentorship huwezi pewa. Just a graduate upewe taasisi ,sio rahisi. Tafuta sehemu ujitolee kidogo ujenge network na kuaminika. Kwa h/shauri jifunze pia siasa za huko. Wanaweza kukuazimia ukileta u GPA wako tu. Nakuombea kwa Mungu milango ifunguke
 
Hello MWANA-HR
1. Hutakiwi kudharau mshahara unaoanza nao kazini, hata wanaoajiriwa serikalini hawaanzi na mshahara wa juu, kama kuna wengine wanapokea mishahara ya juu kwenye kampuni hiyo hiyo maana yake hata wewe utafikia huko. Wapo wenzako huku mtaani wanajitolea kufanya kazi za bure (nauli na chakula juu yao wenyewe) lakini lengo lao kuu ni kutafuta connection.

2. GPA ya 4.1 hiyo ni ya chuo. Huku mtaani tunachanganya GPA na connection, nakushauri ukiwa unatafuta ajira jifanye kama mtu mwenye GPA 2.7 - namaanisha usipuuze kazi yoyote halali wala mshahara wowote kwasababu eti una GPA 4.1

3. Hakikisha kwa kutumia simu yako unajiunga kwenye magroup ambayo yanatangaza ajira mbalimbali. Lakini pia usiache kuzunguka ofisi mbalimbali kutafuta kazi (usikae ndani tu), ikiwezekana anza kufanya kazi ya kujitolea kwenye kampuni iliyopo karibu na unakoishi, kufanya kazi ya kujitolea ni moja wapo ya connection. Mtembea bure si sawa na mkaa bure, ukiwa ofisini hata kama ni kujitolea watu watakuona, watakutathmini, watakuhitaji kwenye makampuni yao kuliko kukaa ndani.
 
Nna gpa ya 4.8 hr na kazi sikupata hadi niliwekaga vyeti vyangu humu kipindi hcho so mentality hyo achana nayo
 
Hr ni kozi moja rahisi sana siku hizi hapa Tanzania,,na imetoa wahitimu wengi sanaaaaaa na wapo mtaani,,,na Serikalini ajira hakuna za Hr sababu hata mwalimu akitaka kujiendeleza anaenda kusomea Hr na kubadilishwa kazi,,Ushauri wangu ondoa dhana ya kuajiriwa anza kufikiria kitu kingine,,kama ajira itakuja ije tu kwa bahati mbaya
 
GPA nzuri ni jambo la kwanza, jambo la pili ni GPA ya kwenye makaratasi au ipo kichwani?

Ukiachana na hilo ajira siku hizi imekuwa ya connection zaidi, ukiwa na network kubwa hata GPA ya 2.8 unapata ajira nzuri tu.

So far hakikisha una vitu vingi kichwani (Kuwa T-shaped person), unakuwa ni expert kwenye kitu kimoja lakini kichwani unakuwa na skills za kutosha.
 
Bado bado aisee
2022 juzi tu
 
Umenikumbusha mbali sana afisa rasimali watu kuna jamaa alikosa kazi kwenye shirika kubwa sana kisa aliulizwa umeshawahi kufukuza mtu kazi akasema hapana akaambiwa hufai kuwa hr wa hii kampuni ila kila la kheri mkuu.
 
Njoo na wazo la kujiajiri mwenyewe , ukisema GPA kwamba ni kubwa unakosea wapo wenye PhD na Masters mtaani weng tu kwa hiyo kma kujiajirii umeshindwa tafufa kaz ya kujishkiza inaweza kua nje ya career yako fanya kwa moyoo connection ztakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…