Nina GPA kubwa 4.1 ya Rasilimali watu(HR) ila kazi sipati


Kazi zipo bro, ila ajira ndiyo hamna.
 
Kuna raha yake na karaha yake kuwa na GPA kubwa kama hiyo. Kwenye soko la ajira hasa private hawaangalii GPA sanaa, wao wanataka kuona je skills ulizonazo zitaweza vipi kuleta tija kwenye nafasi unayoomba. Kikubwa ni kuhakikisha unakuwa na skills relevant na career yako ili uendapo mbele kuwania fursa za ajira uwe na confidence. Nakutakia mafanikio kwenye mapambano yako
 
Hongera nyingi kwa ufaulu mzuri....

Kila laheri..... utapata kazi Insha-Allah...
 
Mungu atakusimamia utapata hitaji lako,ila course nyingine ni changamoto kwenye suala la ajira tofauti na course za Afya au Ualimu,unakuta ofisi Moja Ina watumishi zaidi ya 300 lakini HRO mmoja tu anatosha wakati huo vyuo vinamwaga maelfu ya wahitimu Kila mwaka! course kama hizi unatakiwa iwe kama nyongeza katika profession fulani ukiwa tayari umeajiriwa .
 
Tatizo la utitiri wa vyuo matokeo ndiyo haya, zamani form 4 tu una uhakika wa ajira 100%, ni kufedhehesha wasomi, matokeo yake pia wahanga wa Pdiddy watakuwa wengi kulikuwa na haja gani ya kuongeza vyuo wakati ajira ni chache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…