Nina kiasi cha shilingi milioni 3. Nataka nifungue sehemu ya chips, kuku, mishkaki, Je mtaji unatosha?

Ndio maana akaja kuomba ushauri kwanza.
 
Hiyo pesa inatosha kuanzia kabisa. Kama ulivyoambiwa,kwanza angalia wapi unaweka biashara yako, umewalenga kina nani: vitu vyote hivyo ulivyoorodhesha, kwa mkupuo utaferi. Kumbuka, kuna kukodi eneo la kazi, kuna mzigo kutoisha. Cha kufanya zunguuka maeneo si chini ya kumi. Kama mteja, soma mazingira,ujue wengine wanafanyaje, ulinotisi kitu gani ambacho kimekuvutia na kimekuwa mfano wa kuigwa. Na labda swali: kwa nini unataka hiyo biashara ya hivo! Wakati zipo nyingine zinazoweza kuzunguusha hela?
 
Mkuuu mimi nimefunga location imeniua, nina vyombo najipanga upya
 
Zingatia kinachouzwa NI chips ambayo NI viazi gunia NI Kama laki moja mafuta NI Kama lakimoja deep fryer ya kuanzia Kama laki 2..sahani 10 chumvi na zaga nyingine...ukiipata chumba au sehemu huo NI mtaji mkubwa japo naamini wateja ndio mtaje he unao...unaweza kuanzia kutafuta wateja huku hujui kazi nenda kajitolee kwa mwamba mmoja hata wale wa club night ...UTAPATA kitu Cha ziada ndio uingie
 
Nina kiasi cha shilingi milioni 3. Nataka nifungue sehem ya chips , kuku, mishkaki samaki juice na vinywaji sio vilevi.

Naombeni ushauri kuhusu mtaji huo unatosha? Na vipi Faida na changamoto zake
Inatosha na chenji kubali, Labda pamoja na vifaa,sahani,jiko,karai,Bado inatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…