Tundu Lissu amerudi nchini na tunategemea joto la ushindani wa kisiasa litapanda kwa faida ya umma. Nina mambo matatu ya kujadili kuhusu TL,
- Muda umebadilika na inabidi atulie aangalie muelekeo wa mambo ya ndani na ni hoja ipi inaweza kupeleka Chama chake mbele. Kwa Tanzania bado rushwa ni kubwa na kutokuwajibika kwa viongozi. Shida ni kuwa utaweza kupata ushahidi madhubuti wa kutetea hoja hiyo? Atakapotebelea mikoa athibitishe atakachotanguliziwa na wenyeji wake ili asije akaingizwa chaka.
- TL kwa sasa ni kiongozi wa Chama cha siasa. Ni wajibu wake binafsi na taasisi anayoiongoza kuweza kuangalia dressing code yake. Inaelekea ana shida ya uzito uliopitiliza, designer wake amsaidie nguo gani zitamfaa katika muonekano wake wa sasa.
- Siasa chafu hazijahama na zitamuandama popote alipo. Ni kwa kiasi gani atapambana nazo? Anaweza ku diffuse hili la mfarakano na mkewe kabla yalijavaliwa njuga na wapinzani wake wa kisiasa?