Dah, yaani acha tu mkuu! Wakati mwingine unatafakariii mwishowe unaamua kunyamaza tu ili maisha yaendelee.
Ili uongoze bila presha nchi hii inabidi usiwe mtu wa kujali.....yaani we fanya yako tu. Mwendazake alifanikiwe sana katika hilo. Ye alikuwa anakanyaga tu; kelele za kutojua kiingereza, sijui hana exposure n.k aliwaachia wenyewe wazungumzaji na alipoamua kuwalipa basi alilipa kwa 'vitendo' tu wakati wa uchaguzi. Nafarijika kuona na mama nae kama anafuata njia hiyo hiyo ya kutokujali.......
‐ mwanzo ilianza kikwete ndo anaongoza nchi, naona limekufa sasa na mama anaendelea tu na yake!
‐ likaja eti 'haijui nchi', mama akaendelea na yake na limekufa!
‐ mara nchi imerudi kwa mafisadi, kwamba kwenda kwake Kenya n.k ni kwenda kusaini mikataba ya kinyonyaji (eti hajui lolote). Mama kimya anaendelea na yake
‐ Royal tour hamna kitu, kwanza mliona wapi raisi anatangaza utaliii! Mama kimya na ndo kwanza anazidi kutembelea vivutio! Safi kabisa.
‐ na leo hili, kwamba kuna kikundi kinaongoza nchi 'bila raisi kujua'! Hahahahaaaaa!!!
Wakati tunayaongea, hayo mama analipa vitendo;
1. Tozo (‐ or +)
2. Sgr
3. Umeme wa rufiji
4. Vituo vya afya n.k.