kitaboy
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 341
- 1,219
Ilikuwa hivo wakt wa JPM, mawaziri walisikika kila kona ila kwa sasa naona kasi imepungua sanaYote kwa yote. Mimi kama raia wa kawaida ningependa rais wetu awe anatokea kwa nadra. Labda kila baada ya miezi mitatu.
Na akitokea nchi inasimama kusikia yaliyofanyika, yanayofanyika na matarajio.
Akitokea anakuja na suluhu za mambo makubwa yenye matokeo makubwa.
Mtindo wa mkuu wa nchi kuonekana kila siku yupo wapi, anafanya nini ni kama kumchosha tu na sisi raia kumzoea kama wa kawaida na kupoteza hamu ya kumsikiliza.
Mawaziri ndio askari wa miavuli, hao ndio wa kuhangaika na kutoa mrejesho na anae kwamisha anasaidiwa inavyo stahili.
Ni maoni tu yanaweza kupuuzwa.
Sent using Jamii Forums mobile app