Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Kama katibu mkuu kiongozi ndugu katanga ni team msoga na katibu mkuu ccm ni team msoga!!Baasi wanampangia mama kwa maelekezo kutoka msoga!!!MAMA afifie ili ifikapo 2025 asiwe na nguvu ya kuendelea!!!Hata Shaka naona kimya sana siku hizi!!ngoja tuone!!!
 
Siku zote adui wako ni mtu wa karibu yako. .ule mkono invisible nao kuna siku utaonja mauti ni swala la muda. Mungu wetu sote.nawaza siku ile alikuwa akijisemea moyoni amka sasa tuone kama una uwezo tena dah😒
Ni hivi, ule mkono usioonekana sio mtu au watu fulani. Ni nguvu za asili zinazotenda kazi kwa kuzingatia hali halisi (reality).

Bila shaka umeshasikia ule usemi wa "mchimba kisima huingia na wa kwao". Binadamu sisi kwa kutoona mbali, huwa tuna tabia ya kupitisha maamuzi (ikiwa ni pamoja na sheria) kwa lengo la kuwakomoa "maadui" zetu. Lakini "Mungu si Athumani". Hutokea ndugu au rafiki yako sana ndiye akawa mdhurika wa kwanza kwa uamuzi mbaya/sheria mbovu uliyopitisha. Ndivyo ilivyotokea kwa wapinga katiba mpya. Na leo wanarudia mchezo uleule.

Huo mkono unajulikana sana kwenye uchumi wa soko (market forces). Ukiwekeza kwenye biashara isiyo na mvuto, jiandae kuanguka kwa kukosa wanunuzi.

Halafu usiamini sana mambo ya gizani. Hakuna faulo iliyochezwa. Ni muda ulifika matatizo ya kiafya yanayojulikana vizuri siku nyingi yakasababisha kifo. Aliyeingia madarakani alibahatika sana, akaingia Ikulu kwa sheria waliyopitisha na kuilea wenye madaraka ya nchi hii tangu tupate uhuru 1961. Kisima kilikuwa kimekwishachimbwa. Ndio hivyo tena. Itabidi avumiliwe tu hadi atakapojisikia kukabidhi kwa mwingine.
 
Wewe bado mdogo kwenye siasa, hivi unajua watu kutumia fursa? Kupata nafasi ikatumika vizuri as if ni ukweli? Hivi jambo hilo unadhani linapangwa ndani ya mwaka mmoja? Ogopa mtu anapojua udhaifu wako atakupiga nao na hakuna atakaeamini siri ya ndani.
 
Hakuna rais atakayekuja kuwa maarufu na kupendwa hadi amzidi hayati Magufuli, Samia yuko poa ila hamfikii Magufuli lakini mama hana tatizo, msimlinganishe na viwango vya wengine
 
Tuko na taharuki, kuna muda ukiangalia ni kama mama ameenda sokoni kununua mahitaji ya home ila ukiangali angalia house boi haonekani ila watoto watulivu.
 
Wewe bado mdogo kwenye siasa, hivi unajua watu kutumia fursa? Kupata nafasi ikatumika vizuri as if ni ukweli? Hivi jambo hilo unadhani linapangwa ndani ya mwaka mmoja? Ogopa mtu anapojua udhaifu wako atakupiga nao na hakuna atakaeamini siri ya ndani.
Umeongea neno kwa akili nyingi. Kuna neno zito limehificha hapa lakini linasikika kwa sauti kubwa sana. Vitu havitokei kwa bahati (nzuri au mbaya), vinapangwa!

Hata Covid-19 imetumika kama fursa kwa baadhi ya matukio!

I’m off!
 
Huyu mama umakamu ulimkaa sana anajisahau kama ni rais wa nchi
Alikuwa likizo fulani hivi, kijakazi akifanya kazi zote mpaka kulala na majalada kitandani. Sasa kijakazi kafa, likizo imekatishwa, hata aliyokuwa akifanya kijakazi yeye hajui yanafanywa aje.
 
Siku zote kiongozi mpya anapoingia madarakani kuna baadhi ya watu lazima awaudhi..usijal sana
 
Mataifa yaliyoendelea kisiasa na hata kiuchumi kuna vipindi vigumu yalipitia
..naona hiki kipindi tunachopitia ni lazima na ilipaswa tukipitie ili tuvuke upande wapili..tatizo ni lini na wapi na kwanamna gani tutavuka hali hii.....
 
Mataifa yaliyoendelea kisiasa na hata kiuchumi kuna vipindi vigumu yalipitia
..naona hiki kipindi tunachopitia ni lazima na ilipaswa tukipitie ili tuvuke upande wapili..tatizo ni lini na wapi na kwanamna gani tutavuka hali hii.....
Tuombe sana Mungu tukivuke salama
 
Oh Tanzania! Are you really the one that you used to be, all that long?

Where are those strong pillars that used to hold you firmly and make you unshakable?
 
Umeongea neno kwa akili nyingi. Kuna neno zito limehificha hapa lakini linasikika kwa sauti kubwa sana. Vitu havitokei kwa bahati (nzuri au mbaya), vinapangwa!

Hata Covid-19 imetumika kama fursa kwa baadhi ya matukio!

I’m off!
Covid yenyewe ilitengenezwa uko majuu ili mambo fulani yakae sawa.unajua ukiona mtu (inch) a anataka kukuzidi ubavu mletee maradhi aendelee kukutegemea au anakuletea maradhi yakutowe kwenye mstari wakati ukiangaika kuyatibu yaye anatimiza matakwa yake.hata kama hayo maradhi yatamuumiza ila lengo lazima litimie.hilo ndo lengo la covid

Tofauti na hilo fursa kama bahati ikapatikana yule bwana mwenye timu yake tiifu imekamilika uwanjani akaingia 18 lakini ili watu wenye akili fupi waamini kuwa ni matakwa ya mungu lazima timu hii haifai lazima timu mzima iguswe.

Hii timu bingwa tunafanyaje ili ifutike kwenye uso wa dunia, refa inabidi afate maelekezo kumbuka anatakiwa mwenye timu yake saa tunaanza na wachezaji,

Maelekezo yanaanza, kwa kutumia fursa ile ile wewe refa hakikisha walinda mlango hata kosa dogo atoke kwa red card.

Wakaanzia mbalimbali ili watu wasielewe mpira unachezwaje uwanjani, wataondo wale wa kati hope ndo zinaitwa wing , ikaondoka 5, kaguswa no 2, mwenye timu akapata mshutuko aamini kama amempoteza mlinzi makini, nahisi alijua ni mpango wa mungu, kabla hajakaa sawa akanyofolewa goalkeeper mwenye timu hakuamini, akajipa matumaini, timu ndo inadhoofishwa hivyo, wakamgusa no 3 ahaaa huyu nadhani aliaga kwao maana alibahaa kweli kweli, akapigwa yellow card anaumwa kabisa akaamua kwenda hospital na vifaa vyake Israel inamuita. Watu sasa mchezaji no 3 bana yupo hoi wengine wanasema hayupo hoi mara kajitokeza anaongea kwa taabu kweriiiiy kweriiiiy. Mungu si juma wala khamis akapona sasa. Akarudi uwanjani.

Kama bahati mwenye timu akaingia 18 dah bora angesafirigi, tho asingeweza safiri, kama utani mwenye timu kaondolewa. Wachezaji na mashabeki waliumua hadi leo, Kumbuka timu inaendelea, baada ya muda wakaona no 4 nae mtiifu sana ya mwenye timu yake atakuja kuleta shida mwenye usaili mpya akapigwa redcard.

Hawa waliobaki kwenye timu ni forward ambao hawana back nyuma timu haina walinzi magoli yanaingia tu.ila nao watatoka tu mdogo mdogo.
Kweli mpira hauhitaji hasira.tunaiangalia hii time na mmiliki mpya akisajili vijana wapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…