Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Leo mama kasimikwa kuwa chifu wa machifu, haya ni matusi ya rejareja.

Ikumbukwe hata Mangungo alikuwa chifu tena mwanaume ila aliingizwa mkenge na Karl Peter's, leo hii huyu bibie anakenua meno hajui hata kukataa, keshaingizwa mkenge dadeki [emoji15]
Huyu Mangungo alikuwa chifu wa kabila gani

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE
Nchi inaongozwa na top management ya TISS wakishirikiana na viongozi wa majeshi baada ya kuona mama hana uwezo.
Katiba imewabana kuwa mama awe Rais ivyo hakuna namna
 
Yaani Tozo juu ya Tozo na mama anaona sawa tuu wananchi wake wakiumia hivyo daah kweli siamini kama mzazi kutufanyia hivyo maana najua Mwiguru hawezi kutoa ushauri mzuri kwetu zaidi ya kutuumiza tu..
 
Nchi inaongozwa na top management ya TISS wakishirikiana na viongozi wa majeshi baada ya kuona mama hana uwezo.
Katiba imewabana kuwa mama awe Rais ivyo hakuna namna
Haiwezi kuwa compromised?
 
Usilete fitina !

Huwezi ku-concludes jambo kupitia mchango wa mtu mmoja au wachache!

So far kila mtu anayo haki ya Uhuru wa kutoa maoni yake bila kujali jinsia yake!
Sijahitimisha kwa kuzingatia mchango wa mtu mmoja. Nina data nyingi na nakutana na wengi haswa wanawake wengi
 
Without any doubt Mkuu and that’s very scary. Hopefully Mabeyo will do something before it’s too late.

Mabeyo nae ananjaa kama Mbwa Mwitu. Hana chochote cha kufanya.

Tatizo mama aliingia madarakani kwa fantasy na pressure huku akijaribu kuaminisha watu kwamba mtawala aliyemtangulia alikuwa akifanya vibaya.

Watoto wa mjini wakawa wanamuingiza kwenye 18; na ameshaingia, hachomoki,!now amekuwa muimba taarabu tu na kupangiwa safari za nje akale shushu si ana penda raha sana.

Hivi nyie mnaopoteza Muda kusikiliza speach zake mna moyo sana. Mimi nikimuona nazima kabisa TV. Hakuna anachoongea chochote cha maana.Yeye ni pambo tu kwenye kiti.

Na hii ndio sababu kwa nchi za Africa , feminism kwenye kiti cha Urais haitakiwi. Kwa ulaya ni sawa maana they have closed System na mifumo inajiendesha.
 
Mkuu umenena kweli tupu, nilikuwa nawaza Sana Nani ndo rais kwasasa sielewi, Samia Hana Kazi yoyote ambayo inaonekana kufanywa na rais wa nchi.

Haongozi chochote, hatoi maelekezo, yupo njiani Kila siku, Mpango ndo sijui kapangwa wapi, WK nae anajitutumua bila maboss wake kusikika.

Kabaki anasikika gwajima tu.

Sijui mabeyo anatusikia?
Yupo anaandaa royal tour
 
Everything is in the dirty hands now. Samia if won't be warned as early as possible, she may end up into a hole of shit! President need not to trust anyone except herself. She has to question everything on her table. She started well, when they saw they are losing they pulled her back. They are ahead of her. Mshana what you have said is a glance of ice in a big sea. Let's keep waiting, before sun set, the child will be in town.

When did she start well ? , we don’t see that. she is Horrible in our history . The country is losing ,I am doubting her mental strength and decision making skills. Ni Mavitu vitu tu
 
Tozo kwenye benk zilianza muda ila hawakutaka kuweka wazi, kama una mtu benk muulize.

Kitu ambacho natamani kiondolewe kwenye katiba ni ile rais akifa, maaidizi wake achukue nchi aiseee hii ni kitu ya kipumbavu.

Ila aliecheza hii movie kuanzia kuondoka jpm aliicheza haswa, mwenyewe yupo amekaa anaset mitambo inaenda kama atakavyo dah.

Hakuna movie wala sinema. Hapa ni ule mkono “invisible” unaofanya kazi kuweka sawa mitazamo finyu ya binadamu umefanya yake.

Suala la “caretaker/interim govt” Rais akifariki lilipendekezwa wakati wa mjadala wa katiba awamu ya 4, lakini wazee wa chama wenye maono makuu ya kuishi na kutawala milele waligoma kabisa kukubaliana na point hiyo. Nina hakika walijuta sana mwezi Machi mkono usioonekana uliposhuka ghafla na kupangua ndoto zao.

Sasa sijui itakuwaje manake sasa ndio wamecharuka kabisa. Wanadai suala la katiba mpya si kipaumbele cha wananchi bali wanasiasa wenye uroho wa madaraka! Wala halimo kwenye ilani yao. Eti wananchi wanataka chakula, elimu, maji safi, n.k.
 
Sijui chuo gani wanafundisha kujenga changarawe juu ya lami nzima isiyo na tatizo.

Sijui tathmin ya kumwaga changarawe kwenye lami kwenye tenda inajazweje na mimi nikashiriki. wanataka kutugombanisha vile kati ya wananchi na serikali.

hawajali wenye magari tumelipa vingapi na tunalipia mangapi.

Mtazamo wangu TUNAGOMBANISHWA.

Always tunasema ; Hii jamii ya pwani ikiongoza nchi, ni kweli nchi inaonekana haina VURUGU lakini nchi huwa inaharibiwa na kuoza kabisa ; baada ya hapo reform inahitajika sana.

Alitoka Mkwere , JPM alikuwa na kazi kubwa ya reforms , mpaka ikafikia hatua anatumia nguvu kusawazisha nchi , he was very much successful on that. Alitoka mzee ruksa, nchi ilioza, akaja Ben, the struggle was really

Yaani Hii jamii kazi yao ni kuharibu tu kuacha kila kitu kijiendeshe, nchi inakuwa kama shamba la bibi, nchi inakuwa haina control

Leo hii watanzania wanaona tabu hata kutumia miamala yao, control control

F%^^K off ,
 
Hakuna movie wala sinema. Hapa ni ule mkono “invisible” unaofanya kazi kuweka sawa mitazamo finyu ya binadamu umefanya yake.

Suala la “caretaker/interim govt” Rais akifariki lilipendekezwa wakati wa mjadala wa katiba awamu ya 4, lakini wazee wa chama wenye maono makuu ya kuishi na kutawala milele waligoma kabisa kukubaliana na point hiyo. Nina hakika walijuta sana mwezi Machi mkono usioonekana uliposhuka ghafla na kupangua ndoto zao.

Sasa sijui itakuwaje manake sasa ndio wamecharuka kabisa. Wanadai suala la katiba mpya si kipaumbele cha wananchi bali wanasiasa wenye uroho wa madaraka! Wala halimo kwenye ilani yao. Eti wananchi wanataka chakula, elimu, maji safi, n.k.
Eti wananchi wanataka chakula, elimu, maji safi, n.k.[emoji848][emoji848][emoji848] Katiba inahusika na haya yote
 
Nchi ngumu sana hii, wakati mwingine uwa najiulizaga Watanzania tunataka kitu gani haswa! Ni aina gani ya kiongozi tunayemtaka ambaye atafaa? Nyerere hakufaa, Mwinyi hakufaa,Mkapa hakufaa, Kikwete hakufaa, Magufuli hakufaa,Huyu wa sasa hafai sasa itabidi turekebishe katiba ili ikiwezekana tukakodi kutoka mataifa mengine. Na mara zote hawa watoaji kasoro ubadilika kutokana inategemea ni nani aliyepo madarakani wakati huo hawa watu mara nyingi kama sio mara zote wanakuwa na sababu zao sirini lakini hadharani utafuta sababu nyingine yoyote kuonesha udhaifu wa huyo wanayempinga ili kutafuta uungwaji mkono.

Hakuna Raisi anayefaa wakati wote kwa asilimia 100. Rais ni binadamu kama wengine. Asipowekewa vigezo na nyenzo za kumdhibiti anaweza kufanya mambo ya ovyo sana. Marekani ilishuhudia Rais Trump akijaribu kukiuka katiba ili kubomoa demokrasia na kupigia chapuo ukuu wa watu weupe kwa kivuli cha Make America Great Again (MAGA). Lakini taasisi imara zikamdhibiti.

Ndio maana katiba bora inatakiwa isiyoruhusu Rais kuwa juu ya katiba, sheria na taasisi zote za dola. Katiba inatakiwa iruhusu bunge na wananchi kupima, kujadili na kuchukua hatua za kumwajibisha Rais akivunja katiba, sheria au kuwa na utendaji mbovu sana chini ya vigezo vilivyokubaliwa.
 
Back
Top Bottom