Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Pamoja na mapungufu yake, JPM alikuwa ana uwezo wa kumiliki maamuzi yake katika kila jambo. Hili lilimfanya ajiamini na kusimamia mawazo/maamuzi yake hata kama yalipingwa na ulimwengu mzima.
Sasa kwa mama yetu ni kama vile haamini bado kuwa yeye ndie raisi, ni kama vile hajui nguvu aliyokuwa nayo na mbaya zaidi ni wazi kaweka bayana kwa washauri wake kuwa hana dira. Hili linawapa nguvu wasaidizi wake kufanya maamuzi bila kumshirikisha ipaswavyo ama kupindisha uhalisia hasa wa athari ya maamuzi hayo. Hii inamgharimu mama pale athari inapokuwa hasi, inabidi kutoa kauli kutuliza jazba ambapo in reality linafikirisha juu ya alikuwa wapi mambo yakiamuliwa.
Japo kuna baadhi ya watu watapinga kwa vile wamampenda mama, ila ni wazi mama hajui anakokwenda, hana dira na hana kauli katika maamuzi yake.
Mama amekuwa mithili ya mtoto ambae kanunuliwa vitu vya kuchezea na kupangiwa leo utachezea hiki na kesho kile. Ni kwamba anamiliki vitu hivyo lakini hana mamlaka navyo mpaka mzazi aongee.