Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Nchi ngumu sana hii, wakati mwingine uwa najiulizaga Watanzania tunataka kitu gani haswa! Ni aina gani ya kiongozi tunayemtaka ambaye atafaa? Nyerere hakufaa, Mwinyi hakufaa,Mkapa hakufaa, Kikwete hakufaa, Magufuli hakufaa,Huyu wa sasa hafai sasa itabidi turekebishe katiba ili ikiwezekana tukakodi kutoka mataifa mengine. Na mara zote hawa watoaji kasoro ubadilika kutokana inategemea ni nani aliyepo madarakani wakati huo hawa watu mara nyingi wanakuwa na sababu zao sirini lakini hadharani utafuta sababu nyingine yoyote kuonesha udhaifu wa huyo wanayempinga ili kutafuta uungwaji.
Dah, yaani acha tu mkuu! Wakati mwingine unatafakariii mwishowe unaamua kunyamaza tu ili maisha yaendelee.

Ili uongoze bila presha nchi hii inabidi usiwe mtu wa kujali.....yaani we fanya yako tu. Mwendazake alifanikiwe sana katika hilo. Ye alikuwa anakanyaga tu; kelele za kutojua kiingereza, sijui hana exposure n.k aliwaachia wenyewe wazungumzaji na alipoamua kuwalipa basi alilipa kwa 'vitendo' tu wakati wa uchaguzi. Nafarijika kuona na mama nae kama anafuata njia hiyo hiyo ya kutokujali.......

‐ mwanzo ilianza kikwete ndo anaongoza nchi, naona limekufa sasa na mama anaendelea tu na yake!
‐ likaja eti 'haijui nchi', mama akaendelea na yake na limekufa!
‐ mara nchi imerudi kwa mafisadi, kwamba kwenda kwake Kenya n.k ni kwenda kusaini mikataba ya kinyonyaji (eti hajui lolote). Mama kimya anaendelea na yake
‐ Royal tour hamna kitu, kwanza mliona wapi raisi anatangaza utaliii! Mama kimya na ndo kwanza anazidi kutembelea vivutio! Safi kabisa.
‐ na leo hili, kwamba kuna kikundi kinaongoza nchi 'bila raisi kujua'! Hahahahaaaaa!!!

Wakati tunayaongea, hayo mama analipa vitendo;
1. Tozo (‐ or +)
2. Sgr
3. Umeme wa rufiji
4. Vituo vya afya n.k.
 
Tumerudi kwenye urais taasisi. Sio kipindi kile kila siku Rais anajibu hoja za watu hadi wa mtaani kama vile kina Mnyika, Jacob,Piere Liquid, Mzee Mpili pili, Gwajima n.k. Miradi inaendelea reli imeshatolewa fedha toka Mwanza -Dodoma, Umeme,ujenzi wa vituo vya afya,madarasa,Barabara mpya,treni,mikopo ya wanafunzi,madaraja ya watumishi,ajira mpya n.k na pesa zimeshaelekezwa kwenye shughuli husika.

CHADEMA mnalazimisha mjibiwe kila hoja na matakwa yenu ya kisiasa. Hiyo sio style ya Mama
Kuna siku hao CHADEMA hatakuoa maana hata usiku unawaota...
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Na bado, mpaka maji muyaite MMA!
Uzuri ni kwamba huyo unayemtaria mabaya pengine anakula zake kiyoyozi kwenye gari yake wewe hapo Unapambana na bomba kwenye dala dala, yaani roho ya kimasikini ni shiidaa..
 
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE
Mkuu ulichosema kina ukweli ndani yake, hata yeye anajua haongozi.
Kwa kifupi tumepigwa tena, nchi hii ina bahati mbaya Sana.
Hadi sasa raisi hajatoa vision yoyote,
 
Hilo genge gani?hawazeeki?hawafi?hawaishi?mbona mzee aliyetangulia hamkusema amepotezwa na genge ?😂😂
Usipanue uwanja hadi kusiko.

Genge la Chatto halikuwapo enzi za Mkapa hivyo hoja ya kuwa hawazeeki haina kichwa wala miguu 😂😂!

Hiiiiii bagosha!
 
Safi kabisa!

Nashauri ziongezwe! Maana tunapumua baada ya kunyanyaswa kwa miaka 5.

Baada ya kutopandishwa mishahara na madaraja sasa tumeoandishiwa. Nashauri kodi iongezwe mara dufu
Namimi nashauri kodi ziongezwe maaana tuliteseka sana ile miaka mi 5[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE

Nenda haraka Mwamba Miamba kachungulie kwenye ile TV ambayo inasema uongo 100% 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 . Tunaanza kuchakata tangawizi ili tupige chafya vizuri
 
Kuna watu fulani wakifa wote na vizazi vyao ndio nchi mpaka chama ccm kitakuwa salama.

Ila to late maana watoto zao wameshakuwa na wajukuu.

Umeshawahi kusikia miaka ya nyuma japo ni siri sana “mtoto wa jamhuri”

Hawa kwa sasa wanawatoto ila babu zao bado wapo na kwani wanachelewa kufa

Mwenyezi Mungu tunayemuabudu ni kijana na hazeeki. Tusifanye makosa ya kuona mambo kama vile yote tutamaliza leo
 
Mkuu, tusilaumu watu.

Mama yetu sio mfuatiliaji, ni mtu anayepokea ushauri bila kuutafakari.

Ni mtu wa safari, mikutano na matamasha.

Hajui nchi iende wapi, mipango ya kuifanya Tanzania iwe ya viwanda (Malengo ya Magu) haipewi kipaumbele tena, demokrasia (iliyoonekana kuwa leadership style yake) anaiongea mdomoni tu.

Kwa ufupi mama hakujiandaa kuwa Rais, hata baada ya kuwa bado hawazi na kutenda kama Rais. Katika hali kama hiyo ni wazi kuwa kuna watu bila kutaka ndo wanaongoza nchi.

Kwa ufupi nchi inaongozwa na washauri.
Magu alianzisha viwanda vingapi? au unaleta porojo tu.
 
Mkuu nchi iko mikononi mwa kikundi kinachoitwa Axis of Evil na Kiongozi wao ni gaidi Mwigulu Nchemba kwenye kundi hilo yuko Majaliwa, Ndugai, Mpango, Msigwa, Diwani wa TISS, Ndugulile. Hawa watu ni watu hatari sana na sijui nchi itakuwa mikononi mwa hawa kwa kipindi gani.
Unamwacha wapi SIRO?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Leo mama kasimikwa kuwa chifu wa machifu, haya ni matusi ya rejareja.

Ikumbukwe hata Mangungo alikuwa chifu tena mwanaume ila aliingizwa mkenge na Karl Peter's, leo hii huyu bibie anakenua meno hajui hata kukataa, keshaingizwa mkenge dadeki [emoji15]
This is not right..sio kwa manguo haya
JamiiForums-1721357223.jpg
JamiiForums-693990005.jpg
 
Back
Top Bottom