Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Mama anafanyishwa kazi alizotakiwa kupewa Diamond na Mobeto. Loyo tuwa eti!!!!!!
 
Nyerere alitukosea sana.

Kwa kipindi hiki ni ngumu kuipata, watu lazima walinde maslahi yao.

Wafaidika wakubwa wa katiba hii ndo hao tunaotegemea watuletee katiba mpya hali inayopelekea mchakato wake kuwa ngumu
Kabisa huyu mwalimu alitukosea sanaa, halafu akawa mara kwa mara anatoa angalizo kwamba hii katiba akiingia mtu mtata atatuvuruga sana maana inatoa mamlaka makubwa sanaa but kwa maajabu hakufanya lolote kwenye urais wake wote na hata alipostaafu.
 
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE
Leo mama kasimikwa kuwa chifu wa machifu, haya ni matusi ya rejareja.

Ikumbukwe hata Mangungo alikuwa chifu tena mwanaume ila aliingizwa mkenge na Karl Peter's, leo hii huyu bibie anakenua meno hajui hata kukataa, keshaingizwa mkenge dadeki 😳
 
Nchi ngumu sana hii, wakati mwingine uwa najiulizaga Watanzania tunataka kitu gani haswa! Ni aina gani ya kiongozi tunayemtaka ambaye atafaa? Nyerere hakufaa, Mwinyi hakufaa,Mkapa hakufaa, Kikwete hakufaa, Magufuli hakufaa,Huyu wa sasa hafai sasa itabidi turekebishe katiba ili ikiwezekana tukakodi kutoka mataifa mengine. Na mara zote hawa watoaji kasoro ubadilika kutokana inategemea ni nani aliyepo madarakani wakati huo hawa watu mara nyingi kama sio mara zote wanakuwa na sababu zao sirini lakini hadharani utafuta sababu nyingine yoyote kuonesha udhaifu wa huyo wanayempinga ili kutafuta uungwaji mkono.
 
kumbukumbu zangu zinaniambia kikwete aliambiwa nchi imemshinda mwaka 2009/2010, ajabu mpaka 2015 nchi ikiwa salama na 2016 akakabidhi uenyekiti wa chama kikiwa salama.

Wasiwaxi ukizidi unaweza kujikuta unanimity kivuri chako mwenyewe
 
Unamaanisha huyo mama haja consolidate power? ndiyo matatizo ya urais wa kudandia maana alishindwa kabisa kuunda serikali yake........amebaki kwenda na serikali ya magu.
 
Safi kabisa!

Nashauri ziongezwe! Maana tunapumua baada ya kunyanyaswa kwa miaka 5.

Baada ya kutopandishwa mishahara na madaraja sasa tumeoandishiwa. Nashauri kodi iongezwe mara dufu

Nakazia mama anaupiga yaan dimba kalimiliki timu inacheza. Uhuru sasa upo, ajira za kumwaga, hakuna maneno ya kashfa, uchumi unapanda na tunajitangaza, Mwendazake alituchelewesha sana.
 
Mpangaji ni Mungu. In fact Kila jambo na Kila tukio katika maisha yako vimepanjwa kabla hujazaliwa.
Vilivyopangwa na vikatimia kwa asilimia zote Ni pale mwanadamu huyu anaposimama kwenye kusudi la Mungu, Kwani mpango na kusudi la Mungu kwa mwanadamu yeyote anaezaliwa Ni kuona mwanadamu huyu akiishi maisha matakatifu yenye kumpendeza na kumwabudu yeye, jiulize Ni wanadamu wangapi wapo kwenye huu moango?
Na kwa bahati mbaya Sana Mungu Ni bingwa wa demokrasia , Kwani hakupenda kumlazimisha kila ,mwanadamu aufuate mpango wake,(japokuwa uwezo wa kufanya hivo anao na amekuwa akifanya hivo kwa baadhi ya watu ili kuhakikisha jina lake linazidi kukumbukwa duniani), Bali amempa kila mwanadamu Uhuru wa kuamua njia ya kufuata(kumb 30:19)

Kumbukumbu la Torati 30 : 19
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; "

Hii ina maana kwamba kwa wanadamu wengi, Mungu huweka mpango kupitia maamuzi ambayo mwanadamu huyu ameyafanya, kwamba ayafanikishe au la:
Hi ni kwa sababu wanadamu wengi Ni vigeugeu, Leo atafanya maamuzi ya kumpendeza Mungu kesho ya kumkasirisha Nk.
Angalau wale wachache walio consistent (upande wa kumkasirisha Mungu always au kumfurahisha) Mungu aweza kuwa na mipango ya Muda mrefu kwa hawa..
 
Eti anatangaza utalii! Utalii unatangazwa vile wadau? Yani wizara imeshindwa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom