Nina mashaka kuwa wasaidizi wa Rais Magufuli wanamdanganya

Nina mashaka kuwa wasaidizi wa Rais Magufuli wanamdanganya

Nadharia za wakomunist inferiority complex,
Aache kukua kwenye cocacola,maziwa ya kopo, computer, condoms,madawa ya ARV vyakula nk aje akuuwe kwenye chanjo.Hawa waliosoma syllabus za zamani zilizopandikizwa chuki dhidi ya weupe tabu kweli kweli.
Hivi hajui kwamba kuna Watz walio oa/olewa na Mzungu?? Watajisikiaje Kiongozi Mkuu wa Nchi anapotamka maneno yale?? Je ktk watoto waliozaliwa kwenye ndoa zile ikitokea mmoja wao akawa na matatizo ya kibiolojia si atakimbilia kumlaumu Mzazi/Mzungu kwa ku reffer maneno ya Rais wake??

Tuache kupandikiza/kuchochea chuki zisizokuwa na sababu. Haya siyo maneno mazuri kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Nchi. Hata kama yeye haamini sayansi aliyosoma bali miti shamba zaidi basi Busara ni muhimu.
 
Mabeberu wenyewe kazi yao ni kupambana na Tanzania tu.
Bila shaka! Biden akiamka, wazo lake la kwanza: Nishambuliaje Tanzania leo hii??
Trump kabla ya kulala, anapiga simu apate habari za mwisho wa Tanzania.
Bill Gates akifungua intaneti: wapi njia bora ya kuangusha Tanzania?

Uchumi wa mabeberu unaporomoka, maana hawana muda tena kuipanga au kuedesha shughuli zao za kawaida, maana"kazi yao ni kupambana na Tanzania tu" !!!! Oyee.
 
Sasa kwa akili yako wewe mzungu anakupenda sana?

Mmmhh, ni aibu kwa rais kuwa na mawazo ya kijima kisha kuhutubia taifa. Hata kama ana mashaka, ni vyema hayo angeya address pembeni kwenye vikao vya ndani. Anasema hana imani na chanjo za wazungu ambazo unaweza kupima dawa zao kwenye maabara, lakini alikwenda kunywa kikombe cha babu, dawa isiyo na udhibitisho wowote wa kimaabara! Halafu unaambiwa eti huyo mtu ni mkemia!

Huwa ninacheka sana nikisikia eti wazungu wanatuonea wivu, hao wazungu walianza kutuonea wivu wakati wa awamu hii? Waache kuonea wivu nchi kama Iran, India nk, waje wahangaike na sisi tulioko kwenye elimu ya kunawa mikono ukitoka chooni?
 
Nadharia za wakomunist inferiority complex,
Aache kukua kwenye cocacola,maziwa ya kopo, computer, condoms,madawa ya ARV vyakula nk aje akuuwe kwenye chanjo.Hawa waliosoma syllabus za zamani zilizopandikizwa chuki dhidi ya weupe tabu kweli kweli.

Inaonekana ameathiriwa na story za post colonial toka kwa wakubwa zake kuhusiana na wakoloni wa kizungu, kwa bahati mbaya anataka kutulisha wananchi wote matatizo yake ya kisaikolojia. Namuunga mkono kwenye kutoweka lockdown, lakini vitu alivyozungumza na mifano aliyotolea kuhusiana na huo ugonjwa, ni kama analazimisha kutuvika aibu watanzania wote.
 
Hivi hajui kwamba kuna Watz walio oa/olewa na Mzungu?? Watajisikiaje Kiongozi Mkuu wa Nchi anapotamka maneno yale?? Je ktk watoto waliozaliwa kwenye ndoa zile ikitokea mmoja wao akawa na matatizo ya kibiolojia si atakimbilia kumlaumu Mzazi/Mzungu kwa ku reffer maneno ya Rais wake??

Tuache kupandikiza/kuchochea chuki zisizokuwa na sababu. Haya siyo maneno mazuri kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Nchi. Hata kama yeye haamini sayansi aliyosoma bali miti shamba zaidi basi Busara ni muhimu.

Yaani anaongea kama mtu wa mtaani, tena mwenye uelewa duni kabisa wa mambo ya kawaida. Asingekuwa na elimu ya sayansi ningeweza kumsamehe kwa hilo, lakini mtu mwenye elimu ya sayansi, kisha anaongea maneno hayo ni bonge la aibu.
 
Kuna mambo ukiyasema hayakusaidii kitu na usipoyasema pia hayakupunguzii kitu ni vyema Vitu vingine tukawa tunanyamaza kuliko kujiweka katika matatizo yasiyokuwa ya lazma
Una maanisha asitoe maoni yake, ?unampa boundary asiongee anachojisikia kuongea?

Hebu soma 'motto' wa JF kwanza.
 
Sayansi unaijua wewe?

Siijui, lakini huwezi kuniambia upinge dawa yenye ushahidi wa kimaabara, lakini ukanywe kikombe cha babu wa loliondo kisicho na ushahidi wowote wa kimaabara. Hapo tofauti ya anayejua sayansi na mimi nisiyejua lolote iko wapi? Alichopatia rais ni kutokuweka wananchi lockdown tu, mengine yote anayosimamia ni aibu tupu kwa mtu mwenye PhD ya sayansi.
 
MKUBWA HAKOSEI lakini mwanasayansi wa Chemistry wa kiwango cha PhD kwa hili la chanjo amekosea!!
Taasisi yetu ya magonjwa ya binadamu NIMR inaweza ikaomba audience na Mwalimu wa Chemistry na kujaribu kumuelewesha.
Leo hii couple ya HIV inazaa HIV free child,leo hii Surua imetokomea pamoja na polio.Science ni pana na tuepuke kuichanganya na siasa.
😄 Mkuu, nakumbuka zamani kulikuwa na sehemu ya somo la economics inaitwa political economy, sasa litaingia somo jipya la political chemistry
 
Tahadhima kwenu kizazi Cha Covido-19!

Leo akihutubia kijijini kwake Chato katika uzinduzi wa shamba la miti (Silayo Forest) Rais Magufuli alitumia jukwaa hilo kutoa msimamo wa Serikali kuhusu vita kuu dhidi ya janga la Corona.

Pamoja na mambo mengine, Magufuli ameonya Watanzania kujihadhari na chanjo mbalimbali zinazoletwa na "vipepeo weupe" yaani wazungu akisema, "nchi hii ni tajiri sana" akimaanisha weupe hao hawana nia njema na Afrika.

Rais Magufuli ametolea mfano,"kuna nchi moja ililetewa chanjo kwa mabinti wa miaka 14 ili kujikinga na kansa ya kizazi lakini ikaja kugundulika chanjo hiyo iliwafanya wasichana hao wasizae kabisa", wawe wagumba.

Sijui Magufuli amesahau, hakuwepo nchini, au amedanganywa na wasaidizi wangu. Kwa mujibu wa kumbu-kumbu zangu ni kwamba chanjo hiyo ilitolewa kwa watoto wa Kitanzania kati ya Mwaka 2013/14 ikihamasishwa na Wizara ya Afya chini ya udhamini wa USAID.

Kama ni kweli maneno ya Mr. President, basi nchi hiyo ni Tanzania na tujiandaye kwa wimbi kubwa la kinadada wasiozaa, wagumba.

Hofu kubwa kwa wasichana wetu waliochanjwa.

Kashazoea kuingizwa chaka.
 
Siijui, lakini huwezi kuniambia upinge dawa yenye ushahidi wa kimaabara, lakini ukanywe kikombe cha babu wa loliondo kisicho na ushahidi wowote wa kimaabara. Hapo tofauti ya anayejua sayansi na mimi nisiyejua lolote iko wapi? Alichopatia rais ni kutokuweka wananchi lockdown tu, mengine yote anayosimamia ni aibu tupu kwa mtu mwenye PhD ya sayansi.
Yaani jamaa anapuyanga Sana , ni heri akakaa kimya kuliko kufanya criticism za hovyo namna Ile tena public .. Anatia aibu Sana hili taifa , hata kama kuna vitu vya kiujanja ujanja wanakufanyia is better ukasolve kimya kimya aisee.... Kwa kutokuweka Lockdown hapo Sawa na hii ni kutokana na uchumi wetu ambao ni tia maji Tia maji.... Lakn kutuaminisha kwamba mzungu anafight na wewe Kwa njia hyo et ha ha haaaa ni ushamba wa kiwango cha tarmac road......!!!

Hata rasilimali tunazoaminishwa kila sku et Tanzania ni tajiri hazipo hata....
 
kwani uwongo ndugu zangu?
ila maelezo yake yana ukweli kabisa 100% wapo watoto wa kike waliofanyiwa huo unyama na ingeendelea kwa shule nyingi sana
 
..labda bwana mkubwa ni mtumiaji mzuri wa mitandao, halafu siyo muangalifu, yaani anasomba chochote anachokikuta huko.
 
Kuna magonjwa mengi baada ya chanjo yametoweka kama sio kupungua kabisa mfano
Surua
Pepopunda
Tetekuwanga n.k
So sio kila la mzungu ni baya inatakiwa na sisi tuliboreshe tunavyotaka sisi
Ata hiyo corona yenyew inaaminika nchi zinazotoa chanjo ya kifua kikuu wamekuwa na cases chache zaidi za vifo vya covid 9
 
Back
Top Bottom