Uchaguzi 2020 Nina mashaka na idadi ya wapiga kura 2020

Hao watu ni sahihi 2015 watu wengi sana walichukua hivyo vitambulisho kwa ajili ya kusaijilia line
 
Si mlikuwa nnahamasishana humu msiende kuhakiki taarifa zenu?
Nani tena alikuwa anamasisha watu wasiende kuhakiki? Maana Chadema walikuwa wanawapa taarifa wananchi kwamba wakahakiki taarifa zao,sasa sijui wewe unatoa taarifa za wapi hizo?
 
Hao watu ni sahihi 2015 watu wengi sana walichukua hivyo vitambulisho kwa ajili ya kusaijilia line
Hapana mkuu 2015 hawakufika hao ,walikuwa around 21m...sasa hao 8m wametoka wapi?
 
To be very frank with you, ulitaka NEC iseme idadi ya wapiga kura ni wangapi ILI UKUBALIANO NAO!?Sema tu ili tujue idadi yako.
 
Kwa hiyo mwaka huu wameingzeka milion 7.

Sioni sababu ya kusema ni fake

Hivi unajua maana ya watu milioni saba? Sasa tuache hilo ongezeko lao. Kama tuko 59m+, ina maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote, inawezekana vipi wenye umri mkubwa wakawa sawa sawa na walio chini? Hii haihitaji elimu ya degree kujua kuwa hii idadi ya wapiga kura ni ya kupika. Wangalau idadi ya wapiga kura ya 2015, ambayo ilikuwa 22m+, wakati huo idadi yetu ikiwa 54-55m+.m, ukitoa hapo utaona inabaki kama 30m walio chini ya 18+yrs. Lakini sasa makundi yote ya 18+ na 18- yanalingana!
 
Semistocles Kaijage amaeamua kwa makusudi kucheza na akili za watanzania, ila ajiandae kwa yatakayomkuta.
 
Wala haihitaji Akili kubwa sana kujua kuwa Kukishinda chama kilichokaa Madarakani kwa zaidi ya Miaka 40 hasa Barani Afrika ni Mtihani mzito mno.
Malawi walijaribu lakini baada ya muda mchache MCP imerudi madarakani na nilikua nacheka Sana nikisikia baadhi ya wanasiasa (mostly wa upinzani) Kwa kuwapongeza wamalawi na vyombo vya ulinzi na mahakama vya Malawi Kwa kukomaa mpaka chama kilichotawala tangia enzi za Banda kurudi madarakani...Kwa lugha nyingine system ya Malawi iliyoundwa na Malawi Congress Party Chini ya Hasting Kamuzu Banda ( CCM ya Malawi) ndiyo imecheza part kubwa kuirudisha MCP kwenye Dola.
 
Cha ajabu zaidi half of the population ni watoto ina maana hii nchi watu wazima wote wamejiandikisha ???

Sitaki kulisadiki hili hata kidogo.
 
Nimechota kwa Mchambuzi Mmoja huko Facebook

"HAPA KUNA HOJA NZITO
1.0 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza idadi ya wapiga kura waliojiandikisha (2020) kuwa ni 29,188,347 (NEC, August 19, 2020).

2.0 Makadirio ya Idadi ya watu Tanzania hadi sasa (2020) ni milioni 59.7. Idadi hii imegawanyika kama ifuatavyo:-
a). Fungu la watu (wananchi) wenye umri chini ya miaka 15 ni zaidi ya 44.8%
b). Fungu la watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 ni 52%
c). Fungu la watu wenye umri zaidi ya miaka 64 ni 3%

3.0 Uchambuzi
i). Wapiga kura (kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi) ni miaka 18+
ii). Idadi ya wapiga kura (2020) waliotangazwa na NEC ni takriban 48.9% ya watanzania wote.
iii). Hebu tukadirie: idadi ya watu wasioruhusiwa kupiga kura kwa mujibu wa sheria (umri chini ya miaka 18 kutoka fungu #2.0(b) hapo juu) kuwa ni 1.1% ya wapiga kura wote.
iv). Kwa hiyo, idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa 2020 ni 50% ya Watanzania wote au 100% ya wapiga kura wote!

Uchambuzi huu unabainisha (imply);
1. Kwamba wakati wa kujiandikisha Watanzania WOTE walikuwepo hapa nchini na walijiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu 2020;
2. Kwamba kila Mtamzamia mwenye umri wa kupiga kura kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi atakuwa na yamkini ya asilimia hamsini (50%) ya kwenda kupiga kura; na
3. Kwamba hakuna Mtanzania hata mmoja mwenye umri wa kupiga kura ambaye hakujiandikisha kupiga kura.

Binafsi, niseme kuwa tangu uchaguzi mkuu wa kwanza katika Tanzania huru, uchaguzi mkuu 2020 ndio utakuwa maajabu ya kwanza kuwa asilimia mia moja (100%) ya Watanzania wenye umri wa kupiga kura walijiandikisha kupiga kura!."
 

Hata mimi nilikuwa nawaza katika mstari huo huo,
HAIWEZEKANI WATANZANIA WOTE WENYE UMRI WA KUPIGA KURA WAKAWA WAMEJIANDISHA..!
NI NGUMU SANA KUTOKANA NA HULKA ZA KIBINADAMU
 
Haya ndiyo yale wengine tuliyaona 2014 kwamba Lisu na genge lake hawakujua priority ilikuwa nini kwenye lile bunge la Katiba.

Wao Priority yao ilikuwa Kura ya "UWAZI" Kura ya "SIRI" Priority yao ilikuwa Serikali "TATU"

CCM ni mafundi, waliwatega mtego wakategeka, Leo wanakumbuka kwamba bila Tume huru CCM haichomoki.

Mtavuna mlichokipanda 2014
 
Cha ajabu zaidi half of the population ni watoto ina maana hii nchi watu wazima wote wamejiandikisha ???

Sitaki kulisadiki hili hata kidogo.

Ndio maana hawa jamaa wanasema kila mara kuwa Magufuli atashinda kwa 85%+, kwakuwa wanajua wana idadi yao ya kubumba pembeni. Hakuna uchaguzi mwaka huu, bali kuna zoezi la kutaka kumfurahisha Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…