Kuna ule utafiti kwamba kwenye kila watanzania 7 kuna wawili wenye matatizo ya akili.. sasa katika hao wawili wote ni mashabiki wa Yanga. Kiufupi katika hao milioni 10 wanaoweza kulipia ada ni kama laki 3 tu.
Binadamu bila Elimu na kujengewa hamasa basi ni kiumbe wa ajabu kuliko mnyama na viumbe wote.
Unajua hata maendeleo yasiporatibiwa vizuri kisomi na kitaalamu yanagaeuka kuwa janga na tatizo kubwa Kwa Dunia na ustawi endelevu. Mfano watu wakiachwa wajenge nyumba watajenga mpaka katikati ya reli na Barabara.
Watu wakiachwa wachimbe madini bila kufuata utaalam wa mazingira wataharibu vyanzo vya maji bila kujali kuwa maji ni muhimu kuliko Madini mengine yote.
Kila kitu chema na kizuri Duniani kimemengwa au kuasisiwa na watu wenye nia njema.
Matizo ya akili yanatibika , kama tuna watu wanaosafiri kutoka Kigoma kuja kukaa nje ya uwanja wa Taifa na kuangalia mechi ya Simba na Yanga kwenye TV basi hawashindwi kulipa Ada Sh. Mia Tano Kila mwaka Kwa tigo pesa kulipia ada zao za uanachama. Ambapo Kwa mwaka ni TSh. 6000/- .
Tatizo kubwa kila mahali penye pesa ni kukosa uaminifu. Wahuni na wezi wanatumia rushwa ,uchawi na hata kuua na kila aina ya hila ili aongoze vilabu na kila sehemu na Idara yenye mapato Kwa Lengo la kwenda kupata pesa za anasa na mambo binafsi bila kujali ustawi wa jamii au taasisi husika.
Badala yake watu hao hao waliokosa uadilifu wananunuliwa na mtu aliyejengwa kimaadili na SHERIA Kali kwenye nchi nyingine na kuja kuwekeza kwenye vilabu vyetu.
Mfano Mwarabu kutoka Libya au Mashariki ya Kati au MCHINA wamejengwa Kwa kutumia SHERIA Kali za kimaadili , dini na serikali zao. Kuuawa kwa kula rushwa au kuiba Mali ya umma ni adhabu ya kawaida Kwa nchi wanakotoka. Lakini Tanzania mtu akiiba Mali ya umma anapongezwa na jamii na serikali inatumia mamilioni ya pesa kuunda tume na kumshauri kuwa ajitafakari Mwenyewe.
Watu wanapaswa kuhamasishwa Kwa hamasa kubwa na watu waadilifu juu ya kuthamini nguvu zao na michango yao.
Hivi nani mpaka Sasa anajua kuwa Club ya wananchi ilikusanya sh. Ngapi wakati wa kuchangia timu ya wananchi. Baada ya michango ndio akajitokeza mdhamini.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Yaani wakati timu Haina pesa hakuna mdhamini baada ya kupata pesa akajitokeza mdhamini!!!!
Pesa inapigwa watu wanatengeneza igizo. Mdhamini anakuja .Kwa Nini anawekeza timu yenye wanachama na mashabiki wengi kuliko idadi ya watu wa nchi ya Rwanda. Akili kichwani.
Kwa Nini asiwekeze bil. 30 Mbeya City.? Bila shaka wanachama wanamchango mkubwa sana bila kujali matatizo yao ya akili yanayotokana na kukosa uhuru wa kuwaadhibu na kuwawajiibisha wahuni wanaocheza na hisia na furaha yao.