Nina maswali kadhaa kuhusu Uraia Wa Kibu Denis

Nina maswali kadhaa kuhusu Uraia Wa Kibu Denis

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Mchezaji wa Taifa stars anapewaje uraia leo?

Daaaah So sad figisu za soka letu. Mtu ameshavaa jezi ya Stars leo ndiyo anapewa uraia leo?

NaKumbuka hata Yusuph Poulsen alitaka sana kuichezea Stars,alienda mpaka ofisi za tifua tifua lkn akagongeshwa mwamba!!!!

Kwanini ya huyu iwe ni so special? Afu kitu kingine Kibu alipokipigia Stars, alikua anatumia passport ipi au ya nani?

Screenshot_20211003-091920.jpg
 
Kibu Denis ni mTanzania ila wazazi wake Wana asili toka Congo kwa kuwa walikuwa wakimbizi.

Cha kushangaza, alicheza Geita Gold mine fc, mbeya city na taifa stars ila aliposajiliwa tu Simba sc ikawa tatizo.

Ila hakuna shida kwa sababu Mambo yako sawa kwa Sasa.
 
Ntaambiwa ninanongwa, nitaambiwa sina dogo...

Ukweli ukakasi huu umetengenezwa kwa makusudi kutumia influence na ushawishi...

Huo ndio ukweli... mwendo wa kukomoana tu.
 
Kuna mtu aliambiwa anashindwa kutumia ofisi yake ku influence hili nae bila kutafakari katumia ofisi yake tena eti kwa faida ya taifa wakati.

Kuna vijana lukuki wako nje wanatafuta pa kurudia na akirudi hapati nafasi.
 
Na taifa stars pia mbona uitaji? Alafu ndo ujiulize hilo swali lako,,, fitna fitna fitna
Kwani huyo ana uwezo gani mpk afanyiwe fitna na kwa kipi hasa alichonacho?

Halafu TFF mbona kuna wachezaji wazuri huko nje mpk kesho wanahitaji kuchezea timu ya Taifa ila hawafanyi mkakati wa kuwaombea uraia kama walivyofanya kwa huyu mburundi? Licha ya kuwa mmoja wa wazazi anakuwa ni mtanzania
 
Kwani huyo ana uwezo gani mpk afanyiwe fitna na kwa kipi hasa alichonacho?

Halafu TFF mbona kuna wachezaji wazuri huko nje mpk kesho wanahitaji kuchezea timu ya Taifa ila hawafanyi mkakati wa kuwaombea uraia kama walivyofanya kwa huyu mburundi? Licha ya kuwa mmoja wa wazazi anakuwa ni
Sababu ya kwanza,, Uwezo anao na ndio maana kaitwa yeye ambae kwa mujibu wa tff sio mtanzania lkn kaitwa, na hao ambao unaowasema wewe wako nje ambao ni watanzania hawajaitwa.

Sababu ya pili ni yeye kujiunga na simba kwa kuwa huko alikopita nyuma mbona hatukuyasikia haya,, ikiwa mtu kacheza mpaka taifa stars
 
Je,timu tulizocheza nazo huyo mchezaji akiwemo zikienda kulalamika kua tulitumia mchezaji wa kigeni itakuaje? Haiwezi kuleta nongwa katika hili?
Na taifa stars pia mbona uitaji? Alafu ndo ujiulize hilo swali lako,,, fitna fitna fitna
 
Wakuu Mchezaji wa Taifa stars anapewaje uraia leo??

Daaaah So sad figisu za soka letu. Mtu ameshavaa jezi ya Stars leo ndiyo anapewa uraia leo?..
Hii nchi kila kitu ni usanii tu na siasa! Kwa uzembe tu wa kuruhusu raia wa kigeni kufoji taarifa zake na kujifanya ni raia mwenzetu, ilikua ni sababu tosha ya kumfikisha mahakamani! Na baada ya hapo, kumrejesha katika nchi yake husika.
 
Kwanini leo hii ndo apewe uraia?

Huko Geita, Mbeya City alikuwa anacheza kama raia wa wapi?
😁😁😁😁 Tunaposema hii nchi ni ngumu sana, muwe mnatuelewa ndugu zangu! Yaani mambo yanaenda kienyeji enyeji tu!
 
Kwahyo alikuwa anaishi nchini kinyume na sheria?

Na sheria inasemaje endapo mtu akiwa anaishi kinyume na sheria hapa nchini?
Kwa hali hii ni bora tukawaachia tu wale Waethiopia wa watu wajipitie kwenda zao Afrika Kusini!

Kama inafikia wakati Wahamiaji haram wengine tunawakumbatia, huku wengine tunawahukumu! Hii inakua ni double standard isiyo hata na chembe ya aibu.
 
Kwahyo alikuwa anaishi nchini kinyume na sheria?

Na sheria inasemaje endapo mtu akiwa anaishi kinyume na sheria hapa nchini?
Kwahyo alikuwa anaishi nchini kinyume na sheria?

Na sheria inasemaje endapo mtu akiwa anaishi kinyume na sheria hapa nchini?
Alikuwa anaishi kimbele na Sheria
#kazi iendelee
 
Je,timu tulizocheza nazo huyo mchezaji akiwemo zikienda kulalamika kua tulitumia mchezaji wa kigeni itakuaje? Haiwezi kuleta nongwa katika hili?
Timu tulizocheza nazo kama taifa stars na hata simba nongwa hakuna kwa kuwa ni friend mechi
Labda wayaibue ya huko nyuma kipindi yupo mbeya city na geita gold
 
Back
Top Bottom