Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Mkondo wa Nungwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2019
Posts
332
Reaction score
385
Ninaomba kusaidiwa mchango wa mawazo tatizo ni nini mpaka muda huu nimefilisika kabisa. Mwisho ndani ya miaka mitatu nimefilisika maduka 5. Ambayo nilikuwa nalipia kodi laki 5 kwa mwezi.

Nina mkosi gani au ndio majaliwa yangu au mipango ya Mungu ama shetani.

Situmii kilevi na sijawahi kuhonga hata 30000.
 
Ukinionyesha vitabu vyako vya Mapato na Matumizi, nikiona na cash flow yako naweza kwambia shida ipo wapi.

Ila hivi hivi kumtafuta mchawi itakuwa ngumu sana bro.
Mkuu sikuweza kuweka kumbukumbu izo kipindi hiki cha mwisho wa kufilisika lakin nina historia nzuri tangu nianze biashara mwaka 94 mpaka nilipofilisika mwaka 2016
 
Ninaomba kusaidiwa mchango wa mawazo tatizo ni nini mpaka muda huu nimefilisika kabisa. Mwisho ndani ya miaka mitatu nimefilisika maduka 5. Ambayo nilikua nalipia kodi laki 5 kwa mwezi.

Nina mkosi gani au ndio majaliwa yangu au mipango ya mungu ama shetani.

Situmii kilevi na sijawahi kuhonga hata 30000.
Pole kwa maswahibu. Nataka kujua ukweli. Je, wakati ulioanza harakati zako za kufungua yao maduka11. Ulishawayi kutenga muda kumuomba na kumshukuru munguu imani yako? Je hicho kipato uliokua unazalisha ndani ya biashara zako. Ulishawahi kutenga angalau theluthi yake kurudisha shukran kwa kutoa Sadaka ndani ya nyumba ya mungu iliosimamisha imani yako?

Kama ndio yote ulikua unayatekeleza baci kuna njia za kukurudishia hizo mali ulizopoteza. njoo ntakusaidia utaweza . ila kama hujawahi kumkumbuka baci ujue umeshagongwa mihuri ya safari ya kupotea duniani. Siku zote utakua Binadamu wakupoteza hadi mwisho wa pumzi zako.
 
Jambo la ibada sikuwahi kulizingatia sana nilikua naona muda haunitoshi kufanya sala 5 mara nyongine zilikua zinanipita na kuhisu kutoa nilianza nilipoona mambo yamenikubali kibiashara na mzunguko ulikua mzuri lakin saiv niko bench nafanya sala zote na nimejifunza utamaduni wa kutoa kila ninachokipata.
 
Umeshamaliza kufunga maduka yote mkuu?!

Niachie hata moja nisimamie mimi.
 
Mkuu sikuweza kuweka kumbukumbu izo kipindi hiki cha mwisho wa kufilisika lakin nina historia nzuri tangu nianze biashara mwaka 94 mpaka nilipofilisika mwaka 2016
Mali bila daftari hupotea bila habari

Kama huongi basi matumizi yako na misaada unayotoa inazidi kipato chako .

Pia waweza kuwa unaibia na watu kiakili
 
Pole sana. Fanya hv kwa kifupi:

Share aina ya biashara ulizokuwa unafanya na wapi ulikuwa ukifanya.

Mfano: Umeuza mpunga, Soko la Tandale jijini DSM.

Kwa namna hii atatokea mtu mwenye uzoefu na unaweza kuokota mbili tatu
 
Maduka 11 umefilisika kizembe sana moja tu likianzakudorora inabidi ushtuke ,nakuanza kutafuta pancha ilipo uzibe upepo usitoke, tena haraka ukipunguza matumizi kwa asilimia 50 mpaka utakaporejea sawa, sasa maduka 11 yanaisha upo tu. Basi kuna mawili unanyota ya umaskini huo utajiri ulilazmisha, pili umemkosea Mungu sana, tatu uchawi, kama ni kwaakili yako timamu hayo hayapo maduka 11 yakaisha wewe ni bwege sana. Nipo kwenye shida ila siwezi kuwa na maduka matano tu alafu nifilisike eti.
 
Back
Top Bottom