Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Hayo maduka yote ulifungua kwa wakati mmoja? au ilikuwaje, na wakati moja linafilisika, ulifanyaje kuminimize gharama za kuendelea kulipia kodi ya vyumba kwa ambayo pia yalikuwa yanaonyesha dalili ili walau upate pa kusimamia? Ulisoma vizuri mazingira uliyofungulia maduka? Hivi unaweza kufungua maduka yooote hayo uyaendeshe kwa pamoja, ulipe na wahudumu kwa yote hayo plus kodi bila kuwa na duka mama ambalo mengine yakisuasua lenyewe litakubeba? kwanini unafikiri matajiri wengi wenye makampuni mengi huwa wanaamua kufilisi kampuni zao kadhaa ili walau wabaki na kile kilichopo mkononi kuliko kupoteza vyote? pole sana lakini.
 
Kama kuna mtu mwenye mtaji, tuingie mkataba tufungue duka lenye garama ya sh. 5M . Naweka wadhamini na udhamini mkubwa zaidi ni duka langu lenye garama ya 10M , ndani ya miezi 12 namrudishia mtaji wake na jumla ya sh. 2M. Kama yupo aliyetayari, mimi ni mwaminifu nimelelewa katika uaminifu na naamini bila Mungu kwenye biashara hutoboi, maana Mungu hasimami na watu wenye doa la dhuluma,.
Anayeweza kunisaidia hilo 0757257810
 
Mkuu pole sana awamu iliyopita haikuacha salama mitaji yetu. Nafikiri nawe na mmoja kati ya watu wanaoendesha biashara kwa kutumia mikopo. Pia ongezeko la bei ya vitu linaharibu mitaji na mzunguko wa biashara

Mfano hivi sasa mtu unakuta alikua anapata bidhaa 10 kwa shilling 1000000 hapo inaamanisha ulikua unanua kwa shiling laki kila moja. Fikiria mfumuko wa bei usio thibitiwa bongo. Ukawa unanunua hivyo vitu 10 kwa shilingi 1200000 moja kwa moja hapo unajila mtaji huku faida yako itabaki kuwa ile ile na marejesho pale pale.

Pole sana mkuu ni vyema kuanza moja kuliko kukata tamaa
 
Maduka 11 umefilisika kizembe sana moja tu likianzakudorora inabidi ushtuke ,nakuanza kutafuta pancha ilipo uzibe upepo usitoke, tena haraka ukipunguza matumizi kwa asilimia 50 mpaka utakaporejea sawa, sasa maduka 11 yanaisha upo tu,. Basi kuna mawili unanyota ya umaskini huo utajiri ulilazmisha, pili umemkosea Mungu sana, tatu uchawi, kama ni kwaakili yako timamu hayo hayapo maduka 11 yakaisha wewe ni bwege sana,. Nipo kwenye shida ila siwezi kuwa na maduka matano tu alafu nifilisike eti.
Ndugu yote tuliyonayo ni kwa rehema na wala sio kwa akili zetu.
 
Hiyo mitaji uliipataje, kuhonga mwisho 29,000 kwa mwezi ukihonga wanne ni zaidi ya laki
Nilianza na mtaji wangu mwenywe baadae nikakop
hayo maduka yote ulifungua kwa wakati mmoja? au ilikuwaje, na wakati moja linafilisika, ulifanyaje kuminimize gharama za kuendelea kulipia kodi ya vyumba kwa ambayo pia yalikuwa yanaonyesha dalili ili walau upate pa kusimamia? ulisoma vizuri mazingira uliyofungulia maduka? hivi unaweza kufungua maduka yooote hayo uyaendeshe kwa pamoja, ulipe na wahudumu kwa yote hayo plus kodi bila kuwa na duka mama ambalo mengine yakisuasua lenyewe litakubeba? kwanini unafikiri matajiri wengi wenye makampuni mengi huwa wanaamua kufilisi kampuni zao kadhaa ili walau wabaki na kile kilichopo mkononi kuliko kupoteza vyote? pole sana lakini.
Mwaka 94 nilianza duka langu la kaseti za radio zikaja cd nikaweka nikabadili biashara mwaka 99 nikapigisha simu nikabadili biashara mwaka 2002 nikauza simu na accessory mpaka nimefilisika mwaka 2016 niko kwenye maduka ya simu tu. Nilikua nasimamia mwenyewe biashara mpaka 2010 ndio nilianza kuajiri hapo ndio biashara ilinichanganyia sana nikawa nasafiri mwenyewe kodi zote nilikua nalipa vizuri maduka 3 ndio niliyokua nikiyaendesha kwa pamoja mwaka 2010 mpaka 2015 baadae hapo ndio nikafilisika nikafungua jengine na jengine mpaka ikafika hesabu ya maduka 11.
 
Mkuu..Hujui sababu zilizopelekea ww kufilisika?

Biashara gani ulikuwa unafanya?

Maduka 11 yote yalikuwa ya biashara ya aina moja au tofauti tofauti.
 
Mkuu pole sana awamu iliyopita haikuacha salama mitaji yetu. Nafikiri nawe na mmoja kati ya watu wanaoendesha biashara kwa kutumia mikopo. Pia ongezeko la bei ya vitu linaharibu mitaji na mzunguko wa biashara

Mfano hivi sasa mtu unakuta alikua anapata bidhaa 10 kwa shilling 1000000 hapo inaamanisha ulikua unanua kwa shiling laki kila moja. Fikiria mfumuko wa bei usio thibitiwa bongo. Ukawa unanunua hivyo vitu 10 kwa shilingi 1200000 moja kwa moja hapo unajila mtaji huku faida yako itabaki kuwa ile ile na marejesho pale pale.

Pole sana mkuu ni vyema kuanza moja kuliko kukata tamaa
Ahsante mkuu sijakata tamaa ingawa umri umeende
Mkuu..Hujui sababu zilizopelekea ww kufilisika???

Biashara gani ulikuwa unafanya.??
Maduka 11 yote yalikuwa ya biashara ya aina moja au tofauti tofauti..
Maduka 9 aina moja ya simu moja kaseti na foodstuff
 
Kumbukumbu nilikua naweka nilipoanza kuajiri lakin sikuweza kuhifadhi mabuku nilichanganyikiwa sana.
Ukirudi kwenye mstari, kwanza mkumbuke Mola wako kwa kumpatia shukrani katika mapato unayopata. Pili, tengeneza mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu inaweza kuwa manual (Countebooks) lakini pia computerised (Kutunza kwa kutumia softcopy.
 
Ahsante mkuu sijakata tamaa ingawa umri umeende

Maduka 9 aina moja ya simu moja kaseti na foodstuff

Kuna kaka yangu zaidi ya miaka 27 yeye yupo na duka lake moja tu, sio Siri ana hela ila nilikaa nae. Nikamuuliza ikitokea duka kuungua moto au biashara kuanguka huoni kama utachanganikiwa?. Akaniomba nimpe ushauri nikampa nae akatoa ushauri pia kwa sasahivi anafungua biashara mbalimbali kila akiniona anataka nimpe ushauri zaidi. Ushauri isipendelee kuwa na biashara moja au ya aina moja.
Naomba ufunguke japo duka moja wewe mwenyewe unaona ulikosea wapi mpaka ukaanguka. Biashara zako zilikuwa wapi waliokuwa ukiwatuma sasahivi wao wanamiliki biashara hiohio ilio kuwa ukifanya? Unahitaji kufunguka kidogo tujuwe wapi umekosea.



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Back
Top Bottom