Mkuu Pole na napenda nikuambie haya.
Mungu ni mwenye Rehema.
Usijihesabu mkosaji mbele za Mungu ikiwa unatambua makosa uliyotenda na kukiri mbele zake toka moyoni, anasamehe. Umeshasamehewa. Jisamehe mwenyewe pia na usamehe waliokukosea. Usihukumu wengine.
Usihusishe Uchawi kwenye biashara.
Ikiwa ulitumia ushirikina katika biashara zako mafanikio uliyopata yasingekuwa ya kudumu. Shetani hukuvuta akishakumiliki anakupiga. Atakupa mafanikio ya muda kisha anakugeuka. Lakini Mungu ni mwema rejea kwake uanze upya.
Kushindwa usimamizi wa biashara.
Biashara kuwa nyingi hivyo kukosa usimamizi wa mapato na shughuli zako.
Hofu na mashaka.
Hii ni karakana ya shetani inayochakata na kuharibu mambo ya watu wengi. Hofu na mashaka ya mambo usiyoyajua na hayapo. Hapa humtegemei Mungu unategemea akili zako mwenyewe. Hii karakana imeleta majanga na vilio kwa wengi kwani ukishakuwa na hofu tayari umeshafilisika hata kabla ya kufilisika kiuhalisia. Hapa ndipo hasa wewe ndugu ulipoangukia.
Mahusiano mabaya ndani ya ndoa.
Kukosa mahusiano mazuri kwenye ndoa ni janga lingine shetani amewekeza kuharibu maendeleo na ustawi wa kazi zetu. Ukiondoka nyumbani unasononeko na kuwaza naenda kutafuta kwa ajili ya nini sasa hupati na hata ulicho nacho kinaondoka kwani haukihitaji. Hapa kuna siri kubwa shetani kawekeza.
Ni mengi ndugu ila hapo napiga kuzunguka kichaka kama nimekugusa sema hapo hapo. Ila ikiwa tunaongea ana kwa ana kupata mtiririko wewe mwenyewe utajua umeangukia wapi.
Lakini pia ikiwa kuna watu wanaanza kutoka zero na kuwa matajiri, iweje wewe mwenye uzoefu na biashara uanze kujikabidhi kwa shetani katika mfumo wa kufilisika? La! hasha. Ondoa hilo kichwani, hauna cha kupoteza, kataa shetani, chagua mafanikio na Mungu.