Yaani makosa ninayoyaona hapo ni mengi mno, yaani natamani nikukalishe chini nikupe somo la biashara. Lakini pole tumia muda huu kutafakari ulipoanguka, fanya hivi
1.chukua kalamu na daftari anza kuandika kila kosa unalofikiri ulilifanya kwenye biashara yako mpaka ukafilisika alafu kwa kila kosa andika suluhisho lake ni lipi.... usijaribu kuanza upya bila kujua ulipokosea na utatuzi wake la sivyo utaanguka tena.
2. Kumbuka mara ya kwanza kabisa ulipoanza biashara ulianza vipi mpaka ukaweza kutoka.
3. Sasa angalia ni biashara gani ukiifanya sasa hivi itakusaidia hata kama ni ya mtaji mdogo. Anza nayo tena.
4. Usihof kuhusu swala la umri miaka 45 ni mdogo sana hasa kwa sisi waafrika. Namfahamu mtu ambaye ana miaka 67 na bado anafungua biashara mpya kila siku.
5. Anza upya ila angalia usirudie makosa