Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Ninaomba kusaidiwa mchango wa mawazo tatizo ni nini mpaka muda huu nimefilisika kabisa. Mwisho ndani ya miaka mitatu nimefilisika maduka 5. Ambayo nilikuwa nalipia kodi laki 5 kwa mwezi.

Nina mkosi gani au ndio majaliwa yangu au mipango ya Mungu ama shetani.

Situmii kilevi na sijawahi kuhonga hata 30000.
pole sana kiongozi ila nafikiri pakuanzia ni kuwa;
Unapokuwa na duka zaidi ya moja unatakiwa uwe mwangalifu sana kuhakikisha kila duka linajiendesha; naamaanisha kila duka liweze kugharamia gharama zake za ulinzi, kodi ya nyumba, umeme, maji, mshahara wa muuzaji na kodi ya serikali)
Nina maana unaweza kuwa na baadhi ya maduka yanakwenda kwa hasara na wewe ukaendelea kuya beba kupitia lile duka linalokupa faida; mwisho wa siku yanafirisika yote.
 
inaitwa Business management- eneo hili ni la muhimu na wafanyabiashara wengi wameshindwa hapa- kwa kifupi ww umeibiwa na wasaidizi wako- uliwaamini wamekupiga- maduka 11 - huwezi kuendesha peke yako- Business management ni pamoja ni recruiting- frequently stock count- vijana wa bongo wengi wakingundua unauza tu bila kuhesabu mali- wanakupiga mapema- pole sana Mkuu
 
Brother kwanz pole ila nazn kufeli kwako kwa 96.786%....kumetokn na kuwatumia watu (vijana) katk biashara zako na uliwaamini hukuw na Tabia za kufunga biashara (hesabu ata kwa wiki mara moja )


La II
Changamoto ya management kwako ni kaz


Ushaur
Anz upya ata kwa mtaji mdogo komaa peke ako na mke wako


Ukifungua duka jingne tumia mfumo wa super market wa kuingza bidhaa kwa mfumo wa bar code na kuuza katk mfumo huo



Pole pole na ninakutaikia kila lenye heri


Kujiajir raha ila wanao jiajir kupambn n changamoto had kutoboa
 
Huku wengi hatuna hata biashara moja, subiri waje wazee wa biashara wakupe ABC ila mkuu kwanini uongi? Utatoa wapi nguvu ya kutafuta kama hawa mabibie hawakuchuni??
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my Nokia C1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ulitembea na magubegube yenye gundu? vipi una mkono wa kutoa shukrani? Giving back to the society? Unasaidia jamii? Ulikuwa unajitoa kwa wenye uhitaji?
 
Back
Top Bottom