Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
pole sana kiongozi ila nafikiri pakuanzia ni kuwa;Ninaomba kusaidiwa mchango wa mawazo tatizo ni nini mpaka muda huu nimefilisika kabisa. Mwisho ndani ya miaka mitatu nimefilisika maduka 5. Ambayo nilikuwa nalipia kodi laki 5 kwa mwezi.
Nina mkosi gani au ndio majaliwa yangu au mipango ya Mungu ama shetani.
Situmii kilevi na sijawahi kuhonga hata 30000.
Unapokuwa na duka zaidi ya moja unatakiwa uwe mwangalifu sana kuhakikisha kila duka linajiendesha; naamaanisha kila duka liweze kugharamia gharama zake za ulinzi, kodi ya nyumba, umeme, maji, mshahara wa muuzaji na kodi ya serikali)
Nina maana unaweza kuwa na baadhi ya maduka yanakwenda kwa hasara na wewe ukaendelea kuya beba kupitia lile duka linalokupa faida; mwisho wa siku yanafirisika yote.