Nina miaka 45, nimeshafungua maduka 11 sasa nimefilisika

Nimesoma mwanzo mwisho sijaona sababu za kufilisika!
-Wateja walipungua?
-Ushindani uliongezeka?
-Gharama za biashara ziliongezeka?
-Ulishindwa kusimamia (usimamizi mbovu)?
-Au figisu/uchawi/umefilisiwa kimkakati?
 
Ulikuwa unakumbuka asilimia 2.5 ya zakka? Maana ile ni muhimu sana kwetu sisi waislamu.

Aidha kuwa na maduka mengi siyo jibu la biashara hasa kwa kwetu maana unaweka ndugu zako ambao ndiyo wanakufilisi kwa vile wanaona mali ya kaka au baba mdogo haina hesabu.
 
Haaaaa Haaaaa 😂, hili janga lilitupitia wote, isitoshe kusema kuwa hali ngumu ya biashara imefanya kuongezeka kwa wafanyabiashara wengi na bidhaa nyingi zinafanana
 
Zaka ngumu sana sadaka inawezekana
 
Zaka ngumu sana sadaka inawezekana
Hapana, zaka ni lazima ili uweze kupata mafanikio. Siku nyingine utakapojipanga vyema Inshallah, weka hiyo kama vile unavyoweka kodi ya TRA.

Bila ya hivyo utakuwa unafanya kazi ya kujaza maji kwenye ndoo mbovu.
 
Hamna hata bahresa hatoi zaka anatoa anavopenda mwenyewe kama sadaka.
 
Nilianza biashara pemba mwaka 94 nikahamia dar mwaka 2007 mambo yaliponichanganyia.
Sasa nimekuelewa na nimeelewa chanzo cha "kushindwa" kwako kwenye hiyo biashara ya maduka; ulikuwa kijana mdogo wakati unaanza hizo biashara, kimahesabu naona ulianza biashara ukiwa na miaka kumi na nane! Sasa ukianza biashara, utashinda tu! Anza usikate tamaa.
 
Nimesoma mwanzo mwisho sijaona sababu za kufilisika!
-Wateja walipungua?
-Ushindani uliongezeka?
-Gharama za biashara ziliongezeka?
-Ulishindwa kusimamia (usimamizi mbovu)?
-Au figisu/uchawi/umefilisiwa kimkakati?
Mkuu jibu hili kwanza halafu tuendelee.
 
Pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…