Nina Mil.10 Nikianza ujenzi wa nyumba itafika wapi??

Nina Mil.10 Nikianza ujenzi wa nyumba itafika wapi??

nami leo nimenufaika, wish kama kila mtanzania angepata nafas ya kuwa mwana j.f, this is more than an ordinary University.

Mwenye kiwanja bei ya kimaskini dar /moro, njia ya bagamoyo anijuze.
 
Habari wa JF , naomba msaada wa kimawazo na ushauri, Nina Mil.10 ninaplan ya kujenga nyumba yenye vyumba 3,

Je kwa hiyo pesa nyumba yangu itaishia wapi?

Kwa wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi tafadhari....

Nyumba ya vyumba vingapi? na ukubwa gani?
 
In theory kufyatua matofali kunapunguza gharama, lakini ukija kwenye practice kunaongeza gharama.

Why?

Bongo watu maadili HAKUNA. Kila unayedeal naye anatafuta mwanya wa kukudhulumu. Kufyatua matofali kuna mianya mingi sana ya kudhulumiwa kuanzia kwenye cement, maji na pia uwezekano wa kuibiwa matofali yenyewe kwa sababu yatakaa muda mrefu site.

Hapo unaona kwanza unacompromise quality ya matofali yenyewe lakini pia unaongeza mianya ya kuibiwa na vilevile unajipa mzigo wa kuyalinda matofali. Ukijumlisha na gharama za usimamizi wa shughuli ya ufyatuaji utaona umeongeza direct and indirect costs.

Utaratibu wa kununua matofali ni mzuri kama ule wa Just-In-Time (JIN).
Kabla hujaamua ni bora ufanye utafiti kuhusu kununua matofali au kufyatua matofali

Kuna baadhi ya maeneo mchanga unapatikana kirahisi na bei ni nafuu,so unaweza chagua kufyatua lakini lazima uwe na msimamizi ambaye atasimamia zoezi la kufyatua na kumwagilia matofali.Kama maji na mchanga vinapatikana site na unaye msimamizi ni bora ukachagua kufyatua,
Kama ujenzi wako ni wa kujikongoja unafyatua matofali kwa ajili ya msingi tu yakishakauka unajenga msingi kabisa ili kuondoa uwezekano wa kuibiwa matofali then unajipanga kuandaa kufyatua matofali kwa hatua inayofuatia
 
iyo 10M si uifanyie buznes mkuu? Kujenga ni woga wa maisha, tafuta ela kwanza mambo mengine yatajipa wkt ukifika

Nafikiri huu ndo ukweli ulio wazi...coz mtu unatakiwa ujenge ukiwa na mtaji wa kutosha na sio kujenga ukiwa huna uhakika hela zitakuishia wapi.Kuna nyumba tunaziona zimeishia madirishani au ktk hatua flani itakaa hivyo hata miaka 10,lakini si kwa kupenda bali hakuangalia matokeo mbeleni....Anyway mfumo wa maisha si kama hesabu kwamba kanuni lazima iwe ileile,kila mtu ana yake,tofauti inakuja kwenye mafanikio na ubora period
 
Karibu sana kinyerez mm nimejenga huku kwa msaada zaidi PM kwangu nikupe info na uzoefu nliotumia
Mkuu acha hizo lengo la kuanzishwa hii thread ni pamoja na wengine kupata ujuzi, huko PM unaficha nini? Mwaga ujuzi hapa...
 
Kama ni Tabata udongo sio mbaya na kwa laki tano kwa mita mraba vyumba vya 3m kwa 3m itaishie kwenye lenta kama wenzangu walivyoshauri. Ila matofali yatakuwa ya shs 1,200/-. Mimi nilijenga ya kwangu ya vyumba viwili kwa m10 nikabakiza ya kujenga choo cha shimo kizuri chenye paa na mlango.
 
Pamoja na kuwepo kwa wabishi wengi na watu wenye kupenda kuvunja moyo wenzao,lakini JF... Hakunaga.
 
Ushikatishwe tamaa mkuu cha msingi ni kujua unataka kujenga nyumba ya ukubwa gani? Je unafamilia au bado single? Maana unaweza kudesign ramani ambayo inakuruhusu kujenga nusu kwanza then ndo utakuwa unaendelea taratibu baada ya kuhamia. Na je una kiwanja tayari? Je kuna baadhi ya materials ulisomba hapo site au unaanza from zero?
Na kiwanja kiko maeeo gani? Nijibu nikushauri ila usikate tamaa maana hata Mimi nilihamia bila hata ya sakafu, ripu na madirisha wala milango lakini hili linategemeana na usalama wa mahali ulipo

Hakikisha hu complicate kila stage na usiige we angalia mfuko wako na pia ukitaka kuanza usikae na hela mfukoni wala bank, nenda kalipia material yote in bulk ibaki hela kiasi tu kama petty cash


afredmkohiatgmaildotcom
 
Back
Top Bottom