nina milioni 1, ninunue kifaa gani au niwekeze huduma ipi kwenye tech niingize pesa ?

nina milioni 1, ninunue kifaa gani au niwekeze huduma ipi kwenye tech niingize pesa ?

Yani siwezi kuiweka vizuri kimaneno lakini akikaa sehemu ambayo haijaendelea sanaaa anaweza kupata 10k kwa siku

Simaanishi kijijini kabisa no
Sehemu flan hv
Sio bushiiiiii
Sio town
10k hakosi nna uhakika
Mid-Towns, kama migodini hivi, huduma zote zinapatikana, kuna umeme, maji, biashara, usafiri, n.k
 
N:B: Mimi sio mdau wa kamari, forex, bitcoin.

habari zenu wana tech, naombeni mnipe ideas

Nipo mazingira ya mjini

nilitaka kununua game lakini interest imepungua

binafsi ni muajiriwa lakini ni mdau mkubwa sana wa side hustles

Nahitaji wazo au vifaa / huduma walau kuingiza elf 10 kwa siku,

niliwahi kufungua banda la games tatizo kubwa mimi ni mtumishi sishindi nliweka kijana mwanzoni nilikuwa napata napiga hela ila baada ya miezi miwili simu za wazazi zikaanza kuita wanalalamika watoto wanaiba pesa nyumbani, sheria za kufungua kuanzia jioni, wezi, n.k.
npe namba yako hapa au PM.
 
Hivi PS3, PS4, na PS5 zina bei gani kila moja ikiwa full set
It depends
Ps3 250k sasa hv sema hapo hupewi pad
Hizo ndo nlizoenda kununua mimi wakati naanza

Ps4 550k sema zinashuka zaidi ya hapo mpaka 500k saa nyingine

Ps5 sijui sijawahi fatilia ila millioni na ushee jiandae kuitema
 
It depends
Ps3 250k sasa hv sema hapo hupewi pad
Hizo ndo nlizoenda kununua mimi wakati naanza

Ps4 550k sema zinashuka zaidi ya hapo mpaka 500k saa nyingine

Ps5 sijui sijawahi fatilia ila millioni na ushee jiandae kuitema
PS3 umesema 250k, ukiongezea na TV jumla inakuwa je
 
Internet cafe
Watu wana smartphone lakini hawajui kuzitumia
Maombi ya kazi
Vyuo, mikopo (HESLB, bank)
Birth certificate
Tenda za serikali
 
Back
Top Bottom