Nina Milioni 12 na nina mawazo ya kufanya biashara moja kati ya hizi mbili. Naombeni ushauri

Ethan3

Member
Joined
Dec 19, 2022
Posts
42
Reaction score
52
Habari wana Jamii forums

Ee bhna katika harakati za huku na kule nmefanikiwa kujikusanya nina 12 milioni, kichwa kinawaka moto, sjui nifanye biashara gani

Nipo mkoani kwenye hii mikoa ya pwani yenye shughuli kuu za uvuvi. Nina kijana ambaye nawaza atakuwa muuzaji na mie nitakuwa msimamizi coz ile shughuli iliyofanya nikapata hiyo 12 ml bado sjataka kuiacha.

Mie nna mawazo kama mawili kichwani mwangu ambayo sjaamua nitoke na lipi

Wazo la kwanza ni duka la kawaida la kuuza vyakula kama mchele maharage na vitu vingine (maarufu duka la mangi) wazo la pili ni duka la electronics naweka na wakala (japo sjui kama mtaji huu utatosha).

Kindly naomba msaada wa mawazo si mbaya kama kuna idea nyingine nikapata.

Natanguliza shukrani sana.
 
UZA MAJENEZA SHEHE

UTANIKUMBUKA HAPA

ANDIKA TAR YA LEO
 
Kwa
Duka la mangi hawaanzagi na12M

Huanzishwa na tshs 75000/- na mkaa
Nza unatakiwa kuanza kuuza la mjomba au baba mdogo wako kwa muda usiopungua miaka minne, uonyeshe uaminifu na umakini wa hali ya juu sana+ ubahili mkali mno, kisha unajifunza kuuza bidhaa zako binafsi hapo hapo dukani kwa mjomba, zingatia kuwa kwa kipindi chote utakachokuwa unafanya kazi hapo hutalipwa, isipokuwa inapofika disemba utanunuliwa nguo na viatu vya bei rahisi, utapewa na vihela kidogo vya kunywa soda wakati unasherehekea krismas huko kwenu rombo, ukishakomaa kwenye hiyo biashara yako iliyopo ndani ya biashara ya mjomba hapo tayari utakuwa una mtaji wa tsh zisizopungua 120,000/= mtaji mkubwa sana huo, hata Mengi hakuanza na mtaji mkubwa hivyo, sasa ndiyo uanzishe duka lako, uzidishe ubahili kwa another 100% buni vyanzo vipya, uwe na side hustle kama vile ufugaji na kilimo, ukipata dili haramu calculate risk kwa chini ya dakika moja kisha execute!! Mpaka hapo utakuwa umeshaishiwa hadi na nguo zote, unashindia na kulalia overcoat tu, mwaka unaofuata watu wanaanza kukuhesabia ndugu uliowatoa kafara, ikifika hapo tambua tu kuwa "TAYARI" umeshatoboa! Utajiri wa kimangi ni tabu tupu hakyanani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…