Nina milioni 12, nahitaji ushauri wa gari gani ninunue ambalo halitanisumbua

Obesity

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
111
Reaction score
46
ninaishi maeneo yenye barabara za vumbi lakini si mbaya sana
 
Dah, Mkuu utahitaji kufafanua kidogo, au labda bado sana mkuda wa kununua hilo gari?
Unahtaji gari ya namna gani
SUV, Sedan, Pickup au Van, eleza kidogo. Unahtaji 4*4 ama? Unaangalia fuel economy ama? Utaendea safari ndefu au kazini tu?
 
Ungefafanua matumizi (biashara au kutembelea tu/family car n.k) tungeweza kukushauri vizuri......
 
mkuu nataka iwe four wheel drive na atleast itumie mafuta lita 1 kwa km 10 hivi.Nitaitumia kwa kuendea kazini na safari ndefu pia
 
mkuu sio kwa ajili ya biashara bali ni kuendea kazini na kupigia safari ndefu mara mojamoja na iwe inatumia mafuta atleast lita 1 kwa km 10

Ungefafanua matumizi (biashara au kutembelea tu/family car n.k) tungeweza kukushauri vizuri......
 
mkuu pono ni yadi gani dar ambayo ni nzuri ninaweza kupata toyota rav 4 old model ambayo haijachakachuliwa

Ugonjwa wa moyo Rav 4,nunua toyota spacio new model yenye engine ya VVT-I cc 1800-1500

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Au toyota IST

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mkuu nataka iwe four wheel drive na atleast itumie mafuta lita 1 kwa km 10 hivi.Nitaitumia kwa kuendea kazini na safari ndefu pia

Mkuu kwa hiyo budget utakuwa na wigo mfinyu kiasi, btw ningekushauri Ununue Rav4 old model au Subaru Forester. RAV4 ukipata ambayo haijasumbuliwa na mafundi wa bongo, uzuri wa hii gari ni availability ya spare parts na reliability iko nzuri (Ukinunua iliyochoka ndiyo haoo wanaokwambia ugonjwa wa moyo!). Forester ni gari Nzuri sana, na ni ngumu mno, ila spare parts zake ndiyo bei juu...lakini unapata original hvyo zinadumu mno! Unaweza kuagiza Forester kwa 9Millioni unapata ambayo haijatumika Bongo. Btw, wewe uko wapi mkuu? Kama utakuwa interested tunaweza kuwasiliana zaidi PM, au ingia fb na ulike page yetu http://www.facebook.com/groups/cardeals.tz/
 
Ugonjwa wa moyo Rav 4,nunua toyota spacio new model yenye engine ya VVT-I cc 1800-1500

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
duh,mkuu naitaka ile yenye cc1500 vvti,nipe details zake,ulaji wa mafuta,kuhimili safari ndefu na utengenezwaji wake pindi ipatapo tatizo!!bila shaka unayo
 
Nami pia naomba details mkuu ninahitaji pia
 
Back
Top Bottom