Usitokwe na povu kijana
incharge, vijana wengi hapa Dar including ndugu zangu tunawaona wananunua magari yaliyochoka - used, huku hawana any projects, matokeo yake baada ya muda gari linakuwa juu ya miti na kijana ameishiwa anabaki kuomba hela za kulitengeneza hilo gari. Uliza ama omba ushauri kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakuambia tu, unataka kununua gari kiwanja ama nyumba unayo? Vijana wengi wanapenda kuigana na kujiingiza kwenye hasara kisa fulani ana gari, basi na mimi nanunua gari langu.
Sasa milioni 12 kwa akili yako utanunua gari gani la maana? 98% ya magari ya hapa Tanzania ni ya kubambikiwa (used from abroad - yanasafishwa upya na kupakwa rangi kasha yanaletwa hapa ili yaoze na kuwa nuisance ya foleni jijini.