Mkuu, tafadhali futa hiyo kauli ya kwenye red!..hapo kwenye blue fafanu.
Mambo ya kipi kianze kati ya gari na nyumba inategemea na mtu mwenyewe, mazingira aliyopo, na kazi anazofanya, lazima kila mtu ana vipaumbele vyake, na anaangalia ni kitu kipi kitafanya maisha yake yawe rahisi zaidi. Mfano mmachinga mwenye kufanya biasara ndogondogo mkoani itamuwia rahisi zaidi akijenga kwanza kibanda cha kuishi, kuliko kununua gari (gari linahitaji pesa nyingi za pamoja, nyumba unaweza kununua vitu kwa kadri unavyopata senti na baada ya miaka mitatu minne ukahamia kwako), nyumb hiyo itamrahisishia hata kupata mkopo wa kupanua biashara. Hali ni tofauti kidogo kwa wafanyakazi kama wewe kaka, wanakopa wananunua gari, baada ya miaka mitatu amemaliza kulipa mkopo mtumba wake wa gari umeshachoka anakopa tena anaenda kununua nyingine!!!!
Nachotaka kusema ni kwamba, maisha ni kama mtihani wa hesabu wenye maswali tofauti kwa akila mtahiniwa, ukiangalizia formular anayotumia mwenzio wakati swali lako ni tofauti itakula kwako. SOLVE MTIHANI WAKO.