Nina milioni 3; nifuge kitu gani niweze kupambana na umasikini?

Nina milioni 3; nifuge kitu gani niweze kupambana na umasikini?

mandingo 94

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
269
Reaction score
194
Hàbar Wana JF,

Kama kichwa Cha hàbar kinavyo jieleza hapo juu mim nikijanq mwenye umri wa miaka 27 Ila bado sijatoboa maisha haya Yani umri uwo lakin bado naishi kwa wazazi ya kila kitu namtegemea mzazi wangu.

Hali hii inaniumiza Sana Ila katika harakati za hapa na pale nilipata kibarua mkoani nikafanya kile kibarua kwa muda wa miez 3 nikaweza kuweka pesa Hadi ikafika milion3 sasa nimerudi hom dar njee kidogo na jij maene ya kitunda sas nimefikilia nin nifanye na hii pesa ili niweze kuondokana na umasikini maana umasikini ni mbaya uwezi umri wangu Kuna muda nakosa hata bando la kuingia JF nakosa hapa Mia mpaka Sina chochote uwezi amani hata demu Sina yote kwasababu ya upweke na ukosefu wa kipato cha kukimu.

Hali yangu pia niweze kusema mim ni mdau mzuri tu wa ufugaji na kilimo Ila kilimo napenda ilachangamoto maana Sina hata shamba na Sina mtu nafamianae ambaye anashamba pia mim binafsi napenda Sana ufugaji wa Aina yoyote maana mimi nimfugaji mzuri tu wa sungura Toka mwaka 2013 wengi wananifaham sna kutia sungura sas ndg zangu mpaka nimekuja Yani nimepagawa cjui nin Cha kuwekeza kiasi changu icho niweze kupata faida ya kukidhi mahitaji yangu na kumsaidia mzazi wangu ambaye ni mama yangu ananitegemea Sana.

Maana nishakutana na afisa mifugo wa kata yangu ajanipa maelezo ya kutosha nin nifanye Yani anaongea kisiasa Sana kuliko utendaji kwayi wadau wa ufugaji natanguliza shukran zangu kwenu japokuwa mwandiko mbaya na umenielewa maana waswahili tunaelewana kwa Kiswahili.
 
Mkuu Kama umesema umewahi kufuga sungura it means unajua changamoto zake

Sasa Cha kufanya funga tena sungura ila Safari hii kuwa wa tofauti kidogo

Fanya hivi; wakati wa mavuno ya mifugo badala ya kutafuta wateja wa kulangua wewe tafuta kijiwe dizaini vizuri kabisa Kisha nunua jiko la gesi weird bango NYAMA TAMU YA SUNGURA INAPATIKANA HAPA..Kisha and kukaanga nyama yako Kama wanavyofanya wakaangaji wa mbuzi,nakuhakikishia utatoboa haya maisha
 
Mkuu Kama umesema umewahi kufuga sungura it means unajua changamoto zake

Sasa Cha kufanya funga tena sungura ila Safari hii kuwa wa tofauti kidogo..
Wazo lako c mbaya sna Ila bado nakusanya taarifa za kutosha kuusu malisho ya sungura mbegu Bora za nyama Mambo mengi alafu watu wa sua ushirikiano mdogo maana nilikuwa na tafuta mbegu ya majani flani hiv yanaitwa alafalaf mbaka leo sua awajanipa majibu ndiyo changamoto inaanzia hapo ilanikipata hii mbegu nitakuwa nimefanikiwa kwenye ufugaji wa sungura
 
sijawai fuga mbuzi lakin nimefatilia nyuzi nyingi sana kuhusu ufugaji wa mbuzi ,nimesoma sana sehemu mbalimbali, fuga mbuzi kama utaweza kupata eneo lenye asili ya vichakavichaka na majiani kidogo.Mbuzi hawahitaji eneo kubwa sana kuwafuga ,hawali sana,hawachelewi kukua mpaka kufikia kuuzwa na wanazaana haraka kubwa zaidi nyama yake inapendwa na wengi ,yaan ungepata eneo pembezoni mwa mji ambako usafiri usingekuwa shida mpaka huku mjini Dar ingependeza zaidi.

Kuhusu mbegu nakusahauri kwa kuanza uanze na Mbuzi wa kienyeji pia uchanganye na Isiollo au galla(aina ya mbuzi wa kienyeji).Isiollo wanakuwa hataka na wanajaza nyama kwa mda mfupi,ni wagumu kupata magonjwa na wanaweza kuishi maeneo yenye hali ya hewa ngumu kama vile yenye joto kali.Ukishaelewa vizuri changamoto za ufugaji kama magonjwa na ukajua kukabiliana nazo hapo ndo utaongeza mbegu nyingine ambazo ni bora zaidi hii itategemea na uwezo wako wa kuzihudumia hizo mbegu .

Ukishaamua taarifa zingine kama za mabanda,chanjo na mengineyo zitafata

NOTE:Nashauri usiwekeze yote ,wekeza kama 1.7M hivi huku unasikilizia ,itakayobaki weka akiba ikisaidie kwenye mambo yako mengine na mambo madogomadogo ya kuendesha mradi.
 
Huo ni mtaji tosha, ungekuwa Njombe au Mbeya ungetoboa sana, yaani unatumia milioni mbili kununua ngombe dume, unakodi shamba kwa mtu unaishi hapo, ujenzi wa banda unatumia kama laki mbili tu, inayobaki ni pesa yako ya kuanzia maisha na unatafuta kabisa mfanyakazi wa kukusadia kulisha, baada ya mwezi dume wanakuwa wametoa samadi ya kutosha, unauza samadi, by that time umeshapata eneo la kulima bustani, so unajikuta unauza mazao ya bustani, huku unaendelea kuishi ile pesa yako inapungua baada ya mwaka dume wako wana miloni 4, bustani unazo unaendelea unavunja tena unachukua dume wa milioni mbili kiufupi unatoboa, kama dini ina ruhusu nguruwe anakutoa zaidi
 
1.5 M nunua Ng’ombe wa maziwa mwenye mimba anza ufugaji anao uwezo wa kutoa lita 5 mpaka 12 za maziwa. Weka makadirio ya chini Lita 5@1000 kwa Siku 5000*30 mwezi =150,000 kwa miezi 10 Ela umerudisha ya Ng’ombe.

Pesa nyingine inayobakia tafuta mifugo mingine ufunge.
Uvumilivu unahitajika
 
1.5 M nunua Ng’ombe wamaziwa mwenye mimba anza ufugaji anao uwezo wa kutoa lita 5 mpaka 12 za maziwa. Weka makadirio ya chini Lita 5@1000 kwa Siku 5000*30 mwezi =150,000 kwa miezi 10 Ela umerudisha ya Ng’ombe.
Pesa nyingine inayobakia tafuta mifugo mingine ufunge.
Uvumilivu unahitajika
Hapa nimependa ufugaji huu Ila nimetafuta Sana taarifa za kutosha nimeshindwa kuzipata Yani swali langu ng'ombe anapo zaa namuacha kwa muda gani apumzike ili nimkamue alafu nitamkamua kwa muda gani
 
Hapa nimependa ufugaji huu Ila nimetafuta Sana taarifa za kutosha nimeshindwa kuzipata Yani swali langu ng'ombe anapo zaa namuacha kwa muda gani apumzike ili nimkamue alafu nitamkamua kwa muda gani
Ng’ombe akizaa tu mwache wiki 1 au 2, maziwa ya mwanzo ya njano kwa ajili ya ndama. Baada ya wiki 1 utakuwa unamkamuwa kuangalia kama Maziwa ya njano yameisha
Ng’ombe akishika mimba nyingine utamkamua miezi 7 tu.
 
Back
Top Bottom